Amekufa kutokana na kazi ya kuhuisha roho ya taifa? Ina maana hao waliomvamia wamefanya hivyo kwa sababu ya ujumbe wake wa katiba? Kwani Mvungi ni nani hadi awe na sababu ya kuuawa na asiwe Warioba au jaji Ramadhani?
Hali ya ujambazi ni ya kutisha nchi nzima, na watu wanakufa kila kunapokucha, sema tu kwamba huku mitaani kwetu tukifa, wanaonekana wamekufa panya tu, si polisi wala viongozi wa serikali wanaojitokeza kuonyesha japo maskitiko yao kutokana na kitendo hicho. Juzi tu nilikuwa majohe huku maeneo ya pugu, ujambazi uliopo huko unatisha. Nenda maeneo ya Chanika na rudi ukonga, hadi huko mbezi na kimara. Watu wanazika kila siku kutokana na kuuawa kwa mapanga au risasi. Ila sema tu kwa kuwa hakuna serikali basi tumekuwa tukijizikia ndugu zetu kimyakimya, na hakuna yeyote anayekamatwa kuhusiana na matukio hayo. leo kwa kuwa ameuawa Mvungi tunasema ameuawa kutokana na kazi yake. Hawa wengine wanaokufa kila siku wenyewe huwa wanauawa kutokana na nini? kwanini tusikubali tu kuwa usalama wa nchi hivi sasa ni mbaya? Tukubali ukweli kwamba hali ya nchi yetu ni mbaya, na tunahitaji kuchukua hatua makini kukabiliana nyao na si kusingizia halbari ya kazi yake.