RIP Dr. Mvungi!
Ndg Watanzania wenzangu, kila kukicha tunashuhudia mauaji ya watanzania wenzetu wasio na hatia, tena raia wa kawaida! swali la kujiuliza ni; Kama ujambazi umeongezeka sana hapa nchini ni kwanini wananchi wa kawaida tena wale wanaoonekana kupingana na serikali ndio wanaumizwa? Kwanini mtu kama Lukuvi, Wassira, Pinda tusisikie wamejeruhiwa? wengine watakuja na hoja mufilis kuwa hao viongozi wanalindwa, je vp kuhusu Nape, Nchemba, Ridhiwan, Sendeka na wahuni wengine wa CCM na serikali yao?
Kumbe hawa wahuni wanalindwa na kodi zetu alafu asante yao ni kuwadhuru na kuua raia walipa kodi wa nchi hii?
Ndg zangu watanzania, mtakumbuka kuwa hapajawahi kutokea mauaji ya kinyama ya aina hii unaofanywa na serikali ya ccm katika awamu zote isipokua hii ya huyu FISADI KIKWETE!-shame on him! Hivi huyu mbumbavu hudhan yeye hatokufa? Atakua Rais maisha? Hato-face mkono wa sheria?
Hata Kikwete acheze vipi kete ya mwisho ya kuwapatia wananchi KATIBA eti kama ndio zawadi, nasema hatokwepa mkono wa sheria aslani! DR. MVUNGI sio mtu wa kumpoteza katika kipindi hiki muhimu sana kwa nchi yetu kuelekea kupata Katiba mpya!
DR. mvungi, nenda salama, pumzika kwa amani lakini usijali, maana umewa-grom wengi, tupo mia mamilioni wenye mtazamo kama wako. Walidhani wakikuondoa katika uso wa hii dunia, basi watafanikiwa kumbe kazi ndio kwanza imeanza!
Tumejawa na hasira, Hasira ya kusonga mbele daima kurudi mwisho! Kifo cha DR. Mvungi shujaa wetu, kiwe ni alama ya ukombozi wa taifa mama Tanzania kutoka kwa wakoloni weusi ccm!
Kifo cha DR. Mvungi, ni ishara ya kuzaliwa mamilioni kama MVUNGI. We are very, very close! Tusikate tamaa!!