TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Hii imeniuma sana... This was planned ...na sio majambazi wa kawaida..hawa wametumwa ili kufifisha juhudi za kupata katiba mpya...yule comedian wa jeshi la polisi anasema wamekamatwa...lakini huwezi kukamata wauza gongo kisha ukawapa hii kesi...
Watanzania tubadili namna ya kufikiri matukio...tufikiri in 3 way dimension..kwanini documents zae zimetoweka..laptop nk...
Hakuna atakaye baki duniani...wamepanga ila Allah yupo...
R.I.P Dk Mvungi....
 
Tukisema sana tutaja kufuru,namuombea mwenyezi mungu amlaze mahali pema. Hakika pengo lako hakuna atakae liziba. R.I.P DR MVUNGI.
 
Vibaka 9 waliohusika wamekamatwa na vijana wa kamanda Kova. Wamekutwa na mapanga pamoja na baadhi ya vitu walivyopora ikiwemo Simu ya marehemu Dr. Mvungi.

Kova asilete sarakasi wapelekwe mahakami hao watu na tujue walikuwa wanataka nin kwenye laptop.
 
frankly speaking hatuna waziri wa mambo ya ndani huyu mh ametumikia ccm kwa muda mrefu amesoma akiwa ccm ameoa akiwa ccm kazi ameanzia ccm umoja wa vijana tutegemee nini kipya kutoka kwake lazima atumikie shetani wake ona walivyokuwa wanatoa taarifa za watuhumiwa ,taarifa ilitoka kwa kuchelewa sana as if walikuwa wanasubiria kitu na toka lini waziri akawa msemaji wa matukio badala ya kova kulikoni
 
Mkuu, samahani, hapo ccm imeingiaje?

CCM inahusika kwa ushahidi wa mazingira. Mwenyekiti wake ndiye Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama. CCM ndicho chama kinachopinga kwa nguvu zote mapendekezo mengi ya tume ya katiba, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa wao kuwa wahusika katika kumjeruhi na kumsababishia kifo marehemu.
 
Nadhani inabidi wafe watu wenye kuaminika na kuheshimika na watawala ili system itengenezwe au iandaliwe kulinda wananchi lakini pia iache kutumika na chama tawala na ifanye kazi independently. Chama kimeshika hatamu ikapitiliza, Haiwezekani TISS, PCCB and other security organs wawanyenyekee viongozi wa chama zaidi kama Mwigulu, Nape, Kinana etc wakati waajiriwa wa wananchi wote pasipo itikadi
 
Na alaaniwe aliyemuumiza dr mvungi. Rest in peace mvungi
 
Machozi hayatafaa kuifuta damu yako!!!!!
Uzalendo na ukweli ndio urithi kwa Taifa lako!!!!
Hatuishi humu milele nasi tupo nyuma yako!!!!!!
Hakika hatutolala kwa kusoma kazi zako!!!!!
Hatuwezi kukulipa ila kumuomba mola wako!!!!


Pumzika kwa amani umemaliza kazi yako!!!!
 
MSIMAMO WA DK MVUNGI WA KUONA WA TANZANIA MASKINI WANAPATA KATIBA MPYA ITAKAYOKIDHI MAHITAJI YAO IMESABABISHA KIFO CHAKE... Nakulilia kwa uchungu sana dk.. Upole wako, na utu uliojawa na hekima, KWA NINI WAMEKUUA?
 
Wauaji hakika wameshindwa ku'conceal sababu yao ya msingi ya kuua!

Nia haikuwa fedha, wala simu wala bastola, wala valuable nyingineyo.

Walitaka Laptop na Maisha ya Dr tu!

Pumzika kwa amani Dr Sengondo.
 
Wakati tukito pole kwa ndugu na familia ya dk mvungi, naitaka serikali isilete usanii kwa watuhumiwa, kama ilivyotokea kwa waliotaka kumuua dr ulimboka
 
Back
Top Bottom