TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Kwa jinsi baadhi ya watu wanavyoandika kwa kejeli, ni wazi waliomuua hawakuwa majambazi......ndo maana polisi wamekamata mapanga lakini laptop haisemwi. Something is very wrong somewhere....
RIP Dk S. Mvungi.....

Eti na simu wamekamata pia daaah
 
"Dr Sengondo Mvungi Is NO MORE, Allah ailaze Roho Yake Mahali Pema Peponi " - From SA Milpark Hospital

Source: Hussein Bashe Tweet todat at 16:51

R.I.P Dr. Mvungi, mchango wako kwa dunia ulikuwa ni mkubwa na utakumbukwa daima.
 
Kutoka Hospitali ya Milpark jijini Johannesburg Afrika Kusini;
Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Mwanasiasa
Dr. Sengondo Mvungi amefariki dunia hospitalini hapo leo majira ya saa tisa alasiri. Mwenyezi Mungu aimpuzishe roho yake mahali pema peponi.
Pole kwa familia, chama, Kamati ya Katiba na Watanzania wote.
 
Dah! Walimu wangu mbona wanafariki kiaina hivi?

Kwa mujibu wa Mwananchi, Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Chanzo: Dk Mvungi afariki dunia - Matukio ya Kusisimua - mwananchi.co.tz

Rest in Peace Dr.
 
Ooh, Dr. Mvungi,
Uliponambia ndoto yako ya kuona taifa linakuwa na katiba mpya unaiona ikitimia wakati wa uhai wako, sikujua kuwa hayo ndio maneno ya mwisho kwangu kutoka kwako...
Machungu ya kukupoteza yananielemea. Nakuombea kwa Mungu akupe pumziko jema milele, amina.

Poleni wanafamilia,
Poleni Tume ya Katiba
Poleni Chuo Kikuu cha Bagamoyo
Poleni watanzania wenzangu wote.

Maneno yako yanahuzunisha sana...
 
we acha tu ndugu yangu,waliosema ng,ombe wa masikini hazai hawakoskosea...RIP MWAKILISHI WA TAIFA KWENYE TUME YA KATIBA MPYA
 
Duh, am crying, I cant resist my tears! Namkumbuka wakati nafanya kazi pale UDSM, alivyokuwa akiniona kwa mbali na kuniita kwa sauti yake Nyembemba, na pole, huku akinitania NITAFUTE JIMBO, NCCR itanipika,! R.I.P Dr. Mvungi
 
Apumzike kwa amani Dr. Walaaniwe waliokatisha maisha yake.
 
yaani tuendako ni shimoni, kwani mvungi ni msaada sana kwa taifa letu
sisemi kwasababu ya msiba ila liukweli alikuwa na mchango mkubwa sana kwa taifa letu.
Mungu Amlaze Dr. sengondo mahali panapomstahili
 
Kwa kweli kitengo cha sheria kimeumia, tena sana.

Dah! Walimu wangu mbona wanafariki kiaina hivi?

Kwa mujibu wa Mwananchi, Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Chanzo: Dk Mvungi afariki dunia - Matukio ya Kusisimua - mwananchi.co.tz
 
Kwa hali ilivyo sasa ya ufisadi TZ mtu anaweza kuuwawa ili ile budget ya Mazishi ya wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba itumike ili kuhalalisha matumizi yake. TZ sina imani nayo tena hasa kwa mambo ya usalama wa raia
 
Back
Top Bottom