Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Flight time kwa ndege kubwa kama boeng ni 7 min tu..Duuh flight time from JNIA to Zanzibar is almost 25 minutes... Sasa iweje hiyo surface distance Ununio to Zanzibar iwe 20 km tu??
Umeshakunywa chai?Kwa sababu mmenunua videge huku deni la taifa likizidi kuongezeka ndio mnaamini mnaweza kujenga daraja bara na Zenji. Kweli nyie wapuuzi ndio walewale mliosema heri waTanzania wale majani lakini ndege ya rais inunuliwe wakati huo huo mkijisahaulisha kuwa ccm inapokea mabilioni ya fedha kama ruzuku lakini bado inaiba fedha za hao hao wananchi benki Kuu kugharamia uchaguzi.
Mkuu, waliotowa wazo la hilo daraja ni Diaspora ya Wazanzibari, yaani Wazanzibari walioko nje ya Zanzibar, na Waomani nao wamo sasa watanuna kivipi?..kweli kumbe Bara mpaka Kisiwa cha Zanzibar ni 23miles au 35km
yanawezekana hayo ya daraja la 36km
lkn wenzetu hasa waOman watanuna hao!!!! maana visiwa vyao
nimeikuta mahali hii kitu
![]()
14 Things to Know Before You Go to Zanzibar
Getting lost in Stone Town and getting on Swahili time: smart travel on the Spice Islands.roadsandkingdoms.com
Yetu macho Tuone kama kuna ukweli wowote hapoHilo lingine linawezekana ila la daraja hebu tuache dunia ipite
Kuna shighuli gani inayohitaji daraja hapo?Nilikua nawasoma sehemu Diaspora wa Kizanzibar wanaoishi nje ndo wamechangishana na kuamua kujenga hilo Daraja...
Kwenye chanzo nimeona walikua na Machaguo 3....
-Daraja la Chini ya Maji.
-Daraja la juu lenye Nguzo.
-Daraja la kuelea Majini.
Kwa sababu ya Changamoto mbalimbali wakaamua watajenga Daraja la kuelea, niliona mpaka mchoro wao, nadhani Ilikua youtube.
Mimi huwa sinywi chai.
Madawati tu yameshidikana watoto wanaandikia chini...walimu wanahaha hali ni mbaya..hawajapanda madaraja.... Priorities bado ni tatizo kwa nchi yetu.
UJENZI DARAJA LA DAR HADI ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani (TDC Global) Mhe Norman Jasson amesema kuwa Watanzania waishio nchi za nje (#Diaspora) wapo kwenye mkakati wa kujenga daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na sasa wanasubiri baraka za serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa daraja hilo.
Daraja hilo litakuwa na njia tatu, moja ni kupitisha magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuja Dar es Salaam na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.
Mapendekezo matatu ya ujenzi wa daraja hilo yametolewa ambayo ni moja, kujenga daraja la kupita ndani ya bahari, pili daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa nchi Kavu na kusafirishwa na meli na kisha kuunganishwa.
Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji Dar hadi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko.
Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu.
Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.
Diaspora wameamua kujenga daraja hilo kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli ili kurahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar na watalii waweze kusafiri hata kwa baiskeli.
Mwandishi toka Zanzibar
View attachment 1300633View attachment 1300634View attachment 1300635View attachment 1300636View attachment 1300637
Mpango umefikiaHuu mpango umefikia wapi?
Mpango umefikia pale ulipofikia ule wa Rais Ali Mwinyi wa kujenga tunnel kutokea Feri na kuibuka Kigamboni.Huu mpango umefikia wapi?