Dr Shein: Tunaandaa rasimu ya kuwatambua Watanzania wanaoishi nje kisheria, tutajenga Daraja la Zanzibar - Bara

Dr Shein: Tunaandaa rasimu ya kuwatambua Watanzania wanaoishi nje kisheria, tutajenga Daraja la Zanzibar - Bara

Saivi nasikitika wanyamwezi na wamasai walivoifanya zanzibar kupoteza haiba yake. Dah kwa hali hii Wasukuma si watakuja kwa miguu Zanzibar. Mwenyezi mungu jaalia huu mpango wa Daraja usifanikiwe
 
Kwa sababu mmenunua videge huku deni la taifa likizidi kuongezeka ndio mnaamini mnaweza kujenga daraja bara na Zenji. Kweli nyie wapuuzi ndio walewale mliosema heri waTanzania wale majani lakini ndege ya rais inunuliwe wakati huo huo mkijisahaulisha kuwa ccm inapokea mabilioni ya fedha kama ruzuku lakini bado inaiba fedha za hao hao wananchi benki Kuu kugharamia uchaguzi.
Umeshakunywa chai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli kumbe Bara mpaka Kisiwa cha Zanzibar ni 23miles au 35km
yanawezekana hayo ya daraja la 36km
lkn wenzetu hasa waOman watanuna hao!!!! maana visiwa vyao
nimeikuta mahali hii kitu
Mkuu, waliotowa wazo la hilo daraja ni Diaspora ya Wazanzibari, yaani Wazanzibari walioko nje ya Zanzibar, na Waomani nao wamo sasa watanuna kivipi?..

Please think before you write..be wise
 
Daraja la Bara mpaka Zanzibar litakuwa na urefu gani na linatakiwa kwa sababu gani?

Litagharimu fedha kiasi gani na zitatudishwaje na lini?

Tunaelewa kwamba kuna madaraja kama matano tu duniani yenye urefu wa bara mpaka Zanzibar au zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua nawasoma sehemu Diaspora wa Kizanzibar wanaoishi nje ndo wamechangishana na kuamua kujenga hilo Daraja...

Kwenye chanzo nimeona walikua na Machaguo 3....
-Daraja la Chini ya Maji.
-Daraja la juu lenye Nguzo.
-Daraja la kuelea Majini.

Kwa sababu ya Changamoto mbalimbali wakaamua watajenga Daraja la kuelea, niliona mpaka mchoro wao, nadhani Ilikua youtube.
 
Nilikua nawasoma sehemu Diaspora wa Kizanzibar wanaoishi nje ndo wamechangishana na kuamua kujenga hilo Daraja...

Kwenye chanzo nimeona walikua na Machaguo 3....
-Daraja la Chini ya Maji.
-Daraja la juu lenye Nguzo.
-Daraja la kuelea Majini.

Kwa sababu ya Changamoto mbalimbali wakaamua watajenga Daraja la kuelea, niliona mpaka mchoro wao, nadhani Ilikua youtube.
Kuna shighuli gani inayohitaji daraja hapo?

Gharama zitarudishwaje? Lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madawati tu yameshidikana watoto wanaandikia chini...walimu wanahaha hali ni mbaya..hawajapanda madaraja.... Priorities bado ni tatizo kwa nchi yetu.
 
Ulikuwa utawala wa porojo na misifa sana.
Madawati tu yameshidikana watoto wanaandikia chini...walimu wanahaha hali ni mbaya..hawajapanda madaraja.... Priorities bado ni tatizo kwa nchi yetu.
 
Huu mpango umefikia wapi?
UJENZI DARAJA LA DAR HADI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani (TDC Global) Mhe Norman Jasson amesema kuwa Watanzania waishio nchi za nje (#Diaspora) wapo kwenye mkakati wa kujenga daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na sasa wanasubiri baraka za serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja hilo litakuwa na njia tatu, moja ni kupitisha magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuja Dar es Salaam na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.

Mapendekezo matatu ya ujenzi wa daraja hilo yametolewa ambayo ni moja, kujenga daraja la kupita ndani ya bahari, pili daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa nchi Kavu na kusafirishwa na meli na kisha kuunganishwa.

Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji Dar hadi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko.

Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu.

Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.

Diaspora wameamua kujenga daraja hilo kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli ili kurahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar na watalii waweze kusafiri hata kwa baiskeli.

Mwandishi toka Zanzibar
View attachment 1300633View attachment 1300634View attachment 1300635View attachment 1300636View attachment 1300637
 
Back
Top Bottom