Dr.slaa afunguka kuhusu posho - uzalendo wa DK SLAA ukowapi???

Dr.slaa afunguka kuhusu posho - uzalendo wa DK SLAA ukowapi???

@Rarphryder, Ritz,MSALANI, Salome__,etc Dr Slaa kawakosea nini, mmewekwa rasimi ili kumdharirisha Dr wetu???
Kwani viongozi wa MaCCM, Nape, Kinana, Mangula hawalipwi posho na mishahara, mbona mnamshupalia Dr Slaa???
Wacha hizo, character assisination zenu, mtu mzima Unalipwa kumtukana mwenzako!!
Mnachosha sasa na unafiki wenu!!
 
Katika tahrifa yahabari iliyorushwa na ITV jana usiku, Dr.Slaa alisikika akisema kuwa CDM wataandaa maandamano iwapo serikali itadhinisha nyongeza ya posho kwa wajumbe wa bunge la katiba.

Naomba kumwuliza Dr.Slaa kwa nini asiwaagize wabunge wa CDM wagome kuchukua nyongeza ya posho badala ya kutumia gharama na muada kuandaa maaandamano. CDM wamekuwa na utaratibu wa kugomea shughuri ambazo hawakubaliani nazo. Wamewahi kutoka bungeni mara kibao hata wakati Raisi alipohutubia bunge kwa kigezo kuwa hawamtambui ingawa wakati wa mchakato wa katiba walimtambua na kwenda ikulu.

Je kauli hii ya Dr.Slaa inaonesha dhamira ya kweli ya CDM kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma au ni kauli tu kwa ajili ya kampeni za ubunge Kalenga?
Lema alimshambulia ZZK kuwa ni mnafiki kwa kupinga kuchukua sitting allowance bungeni na chama hakikutoa tamko lolote kupinga kauli ya Lema which means either wao ndio walimtuma au hata kama hawakumtuma then aliwakilisha maoni ya chama.

Kauli ya Dr. Slaa kupinga ongezeko la posho ikiwa na maana ya kupinga matumizi makubwa ya fedha za umma je inapingana na waraka wa Lema na kukubaliana na ZZK?
 
Kama hamjui siasa msitupotezee muda huku jukwaani, kwani hamjui kuna mambo ya faragha a.k.a chumbani na mambo ya hadharani ?

Kwa hiyo mlitaka dokta aongee mbele ya umati wa watu kuwa anaunga mkono posho ?

Unafikiri kwa mfano suala la kujikopesha ruzuku lilipofikishwa kwa wanainchi na wambea, lilimpendeza babu ?............ishu kama hizo kwenye siasa tunaita mambo ya faragha a.k.a ya chumbani.......lakini unapoenda jukwaani au hadharani lazima utoe povu kupinga ufisadi...........

Na hiyo ndio siasa.....
 
ritz 1 ahahahaha POSHO NI SERA ya serikali ya ccm,ndio maana JK KILA SIKU ANASAFIRI kwenda ulaya ili apate posho,hili suala lingewezwa kumalizwa na utasshi wa walio madarakani tu ila mtamsingizia ZZK au DR slaa ila ukweli ni kuwa serikali nzima ya CCM chini ya utawala wa JK na PM Pinda ndio vinara wa posho katika hili taifa
 
siasa bwana swala la katiba ni la mda litaisha sijui slaa ..atahamia kwenye mada gani ya kulets ukombozi kwa watanzania walikuwa wamejikabidhi roho zao kwa chadema wakitegemea hoja na utekelezaji wa nguvu..
..hahahaaaa...

.jipange chadema
 
Kwan kugomea kuchukua kutatusaidia vip watanzania wakati bado zitaendelea kutolewa na wengine watachukua?
Watanzania tuamke tuseme imetosha wajawazito wanakufa kwa kukosa vifaa tiba huku hawa wahuni wachache wanaendekeza ulafi Dom
 
dr anazidi kuwaangaisha na tumegundua mpango wenu wa kushusha imani na hadhi ya dr kwa wananchi wa tz.mtahangaika sana lkn vuuuuuuuuuuuuumbiiiii
 
Dr slaa padri alie acha upadri kwa kashifa tusitegemee kauli ya ukweli kutoka kwake
 
Kama hamjui siasa msitupotezee muda huku jukwaani, kwani hamjui kuna mambo ya faragha a.k.a chumbani na mambo ya hadharani ?

Kwa hiyo mlitaka dokta aongee mbele ya umati wa watu kuwa anaunga mkono posho ?

Unafikiri kwa mfano suala la kujikopesha ruzuku lilipofikishwa kwa wanainchi na wambea, lilimpendeza babu ?............ishu kama hizo kwenye siasa tunaita mambo ya faragha a.k.a ya chumbani.......lakini unapoenda jukwaani au hadharani lazima utoe povu kupinga ufisadi...........

Na hiyo ndio siasa.....

Daaaanh haya umesomeka!!!!!
 
Akiwahutubia wananchi leo mjini iringa katika uzinduzi wa kampeni za jimbo la kalenga DK slaa amesema atazunguka nchi nzima kupinga posho kuongezeka zaidi ya laki tatu. nimestuka huyu amesahau ndani ya chama chake mh lema alijitokeza wazwazi kumpinga mh Zitto kuhusu suala la posho vilevile mbunge selasini aliweka wazi kuwa anaunga mkono suala la posho kuongezeka likamalizikia kwa shibuda aliesema anashangaa mtu kukataa posho.

Wabunge hwawa walidai watachukua posho za bunge licha ya chama kuweka msimamo wa kupinga posho lakini sikusikia hata siku moja akiwakemea au kuwaandikia barua kutoa onyo kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama.

Cha kushangaza nikuwa DK slaa alipoombwa kugombea uraisi alikumbuka posho za kibunge na kuweka masharti ya kulipwa km mbunge ndipo agombee. je uzalaendo wako kimsingi ukowap juu yaposho na maslahi binfsi.

Source: ITV News
Huyu babu hajitambui ni wa kumsamehe tu.
 
Huyu dr slaa nampata vizuri sna.ni mtu makin sna.PASCO MWANAKIJIJI WANALIFAHAMU HLO.WATZ TUKIMKOSA DR SLAA 2015 TUTAJUTA
 
DR. SLAA ATOA TAMKO KUHUSU POSHO ZA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA MPYA.
Katibu mkuu wa CHADEMA,Dr Slaa,akiwa kwenye mkutano wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,jimbo la Kalenga,Grace Tendega,aamua kutoa msimamo wa chama kuhusu posho za wajumbe wa bunge maalum la katiba mpya,
460%3E_3559850.jpg

Ananukuliwa akisema,
"CHADEMA hatutakuwa tayari kwa wajumbe wa bunge maalum la katiba mpya kuongezewa posho zaidi ya shilingi 300,000/= (laki tatu),kwakuwa hela hiyo inawatosha kula,kulala na kufanya kazi zao vizuri wakiwa Dodoma.Na endapo watazidishiwa,kama chama,watazunguka kwa maandamano nchi nzima kwaajili ya kupinga upandishwaji wa posho hizo.Kupandishwa kwa posho hizo itakuwa maajabu kwa taifa hili."

Dr Slaa ametoa kauli hiyo jana tarehe 23-04-2014,akiwa jimbo la Kalenga.
 
Soma hapa kujua alichosema kwa niaba ya CHADEMA

Save Societies: DR. SLAA ATOA TAMKO KUHUSU POSHO ZA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA MPYA.
 
Huyu naye ni mnafiki tu. mbona yeye analipwa mshahara wa Mbunge ilhali si mbunge? Kwani angelipwa hata milioni tatu kwa mwezi zisingemtosha?
 
Akiwahutubia wananchi leo mjini iringa katika uzinduzi wa kampeni za jimbo la kalenga DK slaa amesema atazunguka nchi nzima kupinga posho kuongezeka zaidi ya laki tatu. nimestuka huyu amesahau ndani ya chama chake mh lema alijitokeza wazwazi kumpinga mh Zitto kuhusu suala la posho vilevile mbunge selasini aliweka wazi kuwa anaunga mkono suala la posho kuongezeka likamalizikia kwa shibuda aliesema anashangaa mtu kukataa posho.

Wabunge hwawa walidai watachukua posho za bunge licha ya chama kuweka msimamo wa kupinga posho lakini sikusikia hata siku moja akiwakemea au kuwaandikia barua kutoa onyo kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama.

Cha kushangaza nikuwa DK slaa alipoombwa kugombea uraisi alikumbuka posho za kibunge na kuweka masharti ya kulipwa km mbunge ndipo agombee. je uzalaendo wako kimsingi ukowap juu yaposho na maslahi binfsi.

Source: ITV News

Akili ni nywele; kila mtu ana zake! you seem to know the words BUT you miss their meaning!
 
Kama hamjui siasa msitupotezee muda huku jukwaani, kwani hamjui kuna mambo ya faragha a.k.a chumbani na mambo ya hadharani ?

Kwa hiyo mlitaka dokta aongee mbele ya umati wa watu kuwa anaunga mkono posho ?

Unafikiri kwa mfano suala la kujikopesha ruzuku lilipofikishwa kwa wanainchi na wambea, lilimpendeza babu ?............ishu kama hizo kwenye siasa tunaita mambo ya faragha a.k.a ya chumbani.......lakini unapoenda jukwaani au hadharani lazima utoe povu kupinga ufisadi...........

Na hiyo ndio siasa.....
Mambo ya posho hayo.
 
Back
Top Bottom