Wadau wa karibu watupe Link kama ipo tufuatilie tulio mbali.
Ushauri kwa Dr Slaa
Go to the point!!! Hakuna haja ya makombora, Dr Slaa anakubalika tayari na hana haja ya kutafuta zaidi, he just need to make a case kwa Watanzania, more importantly kuwaconvince independent voters kwa nini yeye anafaa kuwa raisi wa JMT.
Asikubalika kuyumbishwa na maswali ya uchokozi, ambayo yatamfanya atoke nje ya mstari na kupoteza composure yake. Kuna viswali chokozi vitaulizwa kumpima kama atahamaki na kukurupuka na kupoteza utu wake, please Dr Slaa uwe macho na maswali hayo na jaribu kuyajibu kwa uwazi na ukweli. Tafakari swali kabla ya kutoa jibu!! Kumbuka wanataka kujustify the only life line waliyobaki nayo dhidi yako kuwa "unakarupuka"!!
Jaribu kujibu
kila swali utakaloulizwa, usiache au kukwepa swali, na check na muuliza swali kama atakuwa ameridhika na jibu lako.
Toa mifano na sometimes tumia parrables, na ikibidi uchekeshe wahudhuriaji. Ninachotaka hapa ni kuwaonyesha watanzania kuwa uko bold lakini pia kuna time you can be social. kucheka, funny etc
Epuka mitego ya udini ukabila na personal life. Kumbuka wewe ni mkatoliki na ni vyema ukasimamia imani yako lakini bila kuudhi au kushambulia imani za wengine.Usiwape nafasi watakaokuuliza kuhusu ukabilia, udini, na maisha yako binafsi, wape majibu ya jumla na usiingie kwa undani.
Weka bayana na kwa njia nyepesi kueleweka ni nini dira ya taifa utakaloliongoza, naamini kama mkatoliki dira ya kusamehe na kuanza upya ni dira itakayowaondolea hofu wale waliotenda madhambi na watafarijika na kukukubali. Ili uweze kufanya maajabu katika kipindi cha miaka mitano, nakushauri uzungumzie nia ya kusamehe-reconciliation, na kuanza upya kuganga ya mbeleni kuijenga nchi upya katika mwelekeo mpya.
Wape mfano ambao Obama amekuwa anautoa huko Marekani kwenye kampeni za uchaguzi wa November. Kwamba CCM ni kama Republican ambao wamekuwa dereva wa Tanzania kwa takribani miaka 50 wamelitumbukiza gari la Tanzania kwenye shimo refu, sasa Chadema na wanamageuzi wengine waliamua kujitosa kuingia shimoni humo kuliopoa hilo gari letu japo limepondeka pondeka lakini bado linafaa kwa kuwa limebab shehena kubwa ya madini, misitu, samaki,wanyama, ardhi nzuri, etc. Wapinzani wamesota toka kuingia mfumo wa vyama vingi kuliopoa hilo gari, Chadema na wengine wamesota huku CCM wakizidi kulisukumiza chini zaidi na zaidi huku wakinyofoa kila wanachoona kinafaa kwa matumbo yao kama magogo, madini,samaki etc. Wanakaa juu ya bonde wakiwaangalia wapinzani wakihemea juu kulitoa gari. Wanakula mvinyo huku wakiwahadaa, kuwango'nga wapinzani na kuwaibia kura kila wakati wa uchaguzi. Wakati mwingine kuwapiga mawe na kuwanyunyuzia maji ya kuwasha ili washindwe kulitoa hilo gari shimoni. Sasa gari hili limeshatoka shimoni na limewekwa kwenye mstari ulio sawa tayari kuanza safari ndefu kukimbia kuwaletea maendeleo ya kweli Watanzania, loh , wale wale ccm waliolitumbukizamo bila aibu wala soni wanataka kuwapokonya
tena ufunguo wa gari wapinzani hapo tarehe 31 October.
Dr Slaa , tell wananchi wasikubali kuwapa ufunguo CCM hapo October 31, with very simple reason, CCM hawajui kuendesha gari na watalitumbukiza tena shimoni right after election. BUT wawape Chadema ridhaa ya kuongoza hili gari walipeleke kule watanzania wanakotaka kwenda, lakini Chadema hawatawanyima lift CCM , CCM wakae tu kwenye siti ya nyuma ya gari litakaloendeshwa na dereva mpya DR Slaa likiwa na plate number ya CHADEMA. Tumia huu mfano kufunga mdahalo wako. I tell you Dr Slaa kama unasoma hapa utawakoga Watanzania walio wengi na wataelewa vizuri sana with that simple example.
La mwisho, waeleze Watanzania kuwa JK anawaogopa. Hata makanisani wachungaji na mapadre wana madarasa ya dini ambayo waumini wanapata fursa kuuliza maswali magumu, lakini pia wana wakati wa kuhubiri pasipo kuuliza maswali. JK amechukua njia ya kuhubiri sera, bila kuwakabili wananchi wapiga kura wake aweze kujibu maswali magumu. Huko ni kuwaogopa wapiga kura, na kiongozi wa jinsi hiyo hatufai
Alll the BEST Dr Slaa, Mungu akutie nguvu uuonyeshe ulimwengu kuwa kuna watanzania wenye akili na upako wa kuliongoza taifa letu