Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Lets be realistic and base our arguments on the existing fact and not on someone's opinions or thinking.First we have to ask our selves why the Public debate to the Presedential canditadates was not entertained in anyway? Why running away from it.If at all we all knew that, what we all need is to see who has good policy and arguments that can lead Tanzania to the next level.
 
Badili jina ujiite bingwa wa pumba,unaweza toa tafiti zote ambazo Slaa ameshindwa?
Acha unazi wewe kesho unaweza zima TV yako na usiwaongelee watz wewe kama wewe ndo humpendi Slaa bse huu sehemu ya mafisadi
 
Watanzania walio wengi wameonyeshwa kukerwa na kitendo cha Dr slaa kuandaliwa mahojiano maaalumu ITV ambayo yanatajwa kuwa ni moja ya mbinu ya propaganda kwani kuna tetesi kuwa hata watakaopiga simu kuuliza maswali katik kipindi hiko watakuwa wafuasi wake , kutokana na hilo watanzania wengi wanasema watampuuza Dr slaa ambaye anaonyesha kutapatapa baada ya kura zote za maoni kuonyesha yupo nyuma ya kikwete na hata upepo wakisiasa unamvumia vibaya kwani anaonekana ni rais wa magazetini tu lakini hawezi kushinda hivyo watanzania wamepania kumpuuza padre huyo wa kanisa katoliki.

Kumbe ni tetesi nilidhani una uhakika na hilo
 
Natamani ningelikuwepo TZ. Nasikitika kuwa sitapiga kura. Ila hawa watu wanaohusisha dini hata kama ni mwanacahadema/ccm waalaaniwe. Naomba amani iwepo siku ya uchaguzi nasiku za kamapni zilizobaki. I see the future is comming. Ukiwa ndani ya CCM unapiga kura kwa sababu tu Unapata maslahi fulani. Ukiwa mwananchi wa kawaidi unahitaji mabadiliko. Naomba tujiulize.
1. Kwanini watoto wa wanasiasa wetu hawasomi shule za kati?
2. Kwanini wanawapeleka watoto wao nje ya nchi kusoma shahada ya kwanza?
3. Mi nipo hapa Ughaibuni, nimewakuta watoto wa Kibosile wa BOT ada tu kwa mwaka dola US$25000/ wapo watatunikajiuliza hizi hela wanapata wapi?
4. Kama unaweza kuuza madini ukapata vyandarua je huyo mtanzania anakili timamu?
5. Je tunahitaji raisi ambaye hasemi lolote kuhusu rushwa?
 
Watanzania walio wengi wameonyeshwa kukerwa na kitendo cha Dr slaa kuandaliwa mahojiano maaalumu ITV ambayo yanatajwa kuwa ni moja ya mbinu ya propaganda kwani kuna tetesi kuwa hata watakaopiga simu kuuliza maswali katik kipindi hiko watakuwa wafuasi wake , kutokana na hilo watanzania wengi wanasema watampuuza Dr slaa ambaye anaonyesha kutapatapa baada ya kura zote za maoni kuonyesha yupo nyuma ya kikwete na hata upepo wakisiasa unamvumia vibaya kwani anaonekana ni rais wa magazetini tu lakini hawezi kushinda hivyo watanzania wamepania kumpuuza padre huyo wa kanisa katoliki.

Kama Dr. Slaa atapuuzwa basi utuletee huyo anayetangaza utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kwanza kabisa Dr. Slaa haogopi midahalo tofauti na wenzako ambao wanaogopa mdahalo. Kwanini mgombea urais anaogopa kuulizwa na wapiga kura? Badala ya kuzungumzia hilo unaleta hoja zisizo na mshiko kabisa.

Mwulize Kinana alivyogarazwa jana katika mahojiano yaliyoendeshwa na Statv. Kinana alitaka hoja ya wizi wa kura ipuezwe lakini Dr. alifafanua kuwa lina ushahidi wa kimahakama. Tafadhali uwashauri wenzako washiriki midahalo hata kama wanaogopa kuumbuliwa.
 
Watanzania walio wengi wameonyeshwa kukerwa na kitendo cha Dr slaa kuandaliwa mahojiano maaalumu ITV ambayo yanatajwa kuwa ni moja ya mbinu ya propaganda kwani kuna tetesi kuwa hata watakaopiga simu kuuliza maswali katik kipindi hiko watakuwa wafuasi wake , kutokana na hilo watanzania wengi wanasema watampuuza Dr slaa ambaye anaonyesha kutapatapa baada ya kura zote za maoni kuonyesha yupo nyuma ya kikwete na hata upepo wakisiasa unamvumia vibaya kwani anaonekana ni rais wa magazetini tu lakini hawezi kushinda hivyo watanzania wamepania kumpuuza padre huyo wa kanisa katoliki.

we uko hivi
 
Dr Slaa is confident and determined for the presidency,ntakuwa pembeni ya TV yangu nikimwangalia.
CHONDE CHONDE CCM msijije kata umeme
 
CCM hawakubali Slaa azungumze na wananchi kwa masaa matatu.

Kwa taarifa yenu umeme wa grid ya taifa utazimwa kwa visingizio vya ajabu, Watanzania wengi wasipate furusa hiyo.

Bora umenikumbusha mkuu kuliko kuikosa kwa umeme kukatwa ngoja nijinunulie kijenerat kidogo cha wachina kinafaa
 
its a do or break for slaa! will he sway the swing voters his way? or will it be one mistake one goal? either way he has a presidential gravitas!
 
Nadhani hapo Dr Slaa afanye majumuisho ya mambo, mateso, unyanyapaa wotee alioukuta mikoani kama Shy watu wanakula dagaa mwaka mzima, mwanza samaki hawaliwi na wenyeji, kila kona kero kibao. Leo ndo mambo hadharani yaani kama ni makombora 20 ayalipue yote na amwage sera kama kawa.
 
Ndugu zangu wanaJF, kama kawaida yetu haipiti siku bila kufanya chochote kwa ajili ya taifa letu changa katika nyanja mbali mbali. Na leo tena tunayo fursa kubwa na ya kipekee kabisa kuchangia chochote katika kuendeleza nchi yetu kidemocrasia.

Maswali yangu ambayo nafikiria yakijibiwa vizuri basi nchi yetu itaondokana na hii hali ya umimi, ufisadi, uchu wa madaraka, kupotea kwa uzalendo si kwa viongozi tu hata kwa wananchi wenyewe, kuacha kuabudu vichwa vya magharibi na kujiona sisi wenyewe tunaweza, tunaweza, tunaweza tunaweza bila hata ya utegemezi.

1. Dr Slaa azungumzie nini zaidi wakati wa kuongea na watanzania kwa ule muda wa masaa mawili ( 2 hours) jiji dar es salaam?

2. Ni muda mwafaka kwa Dr Slaa kuyaweka wazi makombora 20?

3. Ni muda mwafaka kwa Dr Slaa kueleza kwa kina ni jinsi gani sera ya chama chetu mbadala itatekelezeka?

4. Ni namna gani basi Dr Slaa akabiliane na hao wapinzani wake akijua kuwa yeye anaanza wanaokuja hawajui watasemaje juu ya maada zake atakazozisema?

WanaJF ni hayo tu kwa leo, naomba kuwasilisha.
 
hivi hii kitu haina link yoyote tuweze kuifuatilia?
 
Wadau wa karibu watupe Link kama ipo tufuatilie tulio mbali.
 
Mi sina wasiwasi na DR yaani atafunika, na huu mdahalo utazaa kura nyingine nyingi sana kutoka kwa wafuasi wa ccm
 
Wadau wa karibu watupe Link kama ipo tufuatilie tulio mbali.
Ushauri kwa Dr Slaa

Go to the point!!! Hakuna haja ya makombora, Dr Slaa anakubalika tayari na hana haja ya kutafuta zaidi, he just need to make a case kwa Watanzania, more importantly kuwaconvince independent voters kwa nini yeye anafaa kuwa raisi wa JMT.

Asikubalika kuyumbishwa na maswali ya uchokozi, ambayo yatamfanya atoke nje ya mstari na kupoteza composure yake. Kuna viswali chokozi vitaulizwa kumpima kama atahamaki na kukurupuka na kupoteza utu wake, please Dr Slaa uwe macho na maswali hayo na jaribu kuyajibu kwa uwazi na ukweli. Tafakari swali kabla ya kutoa jibu!! Kumbuka wanataka kujustify the only life line waliyobaki nayo dhidi yako kuwa "unakarupuka"!!

Jaribu kujibu kila swali utakaloulizwa, usiache au kukwepa swali, na check na muuliza swali kama atakuwa ameridhika na jibu lako.

Toa mifano na sometimes tumia parrables, na ikibidi uchekeshe wahudhuriaji. Ninachotaka hapa ni kuwaonyesha watanzania kuwa uko bold lakini pia kuna time you can be social. kucheka, funny etc

Epuka mitego ya udini ukabila na personal life. Kumbuka wewe ni mkatoliki na ni vyema ukasimamia imani yako lakini bila kuudhi au kushambulia imani za wengine.Usiwape nafasi watakaokuuliza kuhusu ukabilia, udini, na maisha yako binafsi, wape majibu ya jumla na usiingie kwa undani.

Weka bayana na kwa njia nyepesi kueleweka ni nini dira ya taifa utakaloliongoza, naamini kama mkatoliki dira ya kusamehe na kuanza upya ni dira itakayowaondolea hofu wale waliotenda madhambi na watafarijika na kukukubali. Ili uweze kufanya maajabu katika kipindi cha miaka mitano, nakushauri uzungumzie nia ya kusamehe-reconciliation, na kuanza upya kuganga ya mbeleni kuijenga nchi upya katika mwelekeo mpya.

Wape mfano ambao Obama amekuwa anautoa huko Marekani kwenye kampeni za uchaguzi wa November. Kwamba CCM ni kama Republican ambao wamekuwa dereva wa Tanzania kwa takribani miaka 50 wamelitumbukiza gari la Tanzania kwenye shimo refu, sasa Chadema na wanamageuzi wengine waliamua kujitosa kuingia shimoni humo kuliopoa hilo gari letu japo limepondeka pondeka lakini bado linafaa kwa kuwa limebab shehena kubwa ya madini, misitu, samaki,wanyama, ardhi nzuri, etc. Wapinzani wamesota toka kuingia mfumo wa vyama vingi kuliopoa hilo gari, Chadema na wengine wamesota huku CCM wakizidi kulisukumiza chini zaidi na zaidi huku wakinyofoa kila wanachoona kinafaa kwa matumbo yao kama magogo, madini,samaki etc. Wanakaa juu ya bonde wakiwaangalia wapinzani wakihemea juu kulitoa gari. Wanakula mvinyo huku wakiwahadaa, kuwango'nga wapinzani na kuwaibia kura kila wakati wa uchaguzi. Wakati mwingine kuwapiga mawe na kuwanyunyuzia maji ya kuwasha ili washindwe kulitoa hilo gari shimoni. Sasa gari hili limeshatoka shimoni na limewekwa kwenye mstari ulio sawa tayari kuanza safari ndefu kukimbia kuwaletea maendeleo ya kweli Watanzania, loh , wale wale ccm waliolitumbukizamo bila aibu wala soni wanataka kuwapokonya tena ufunguo wa gari wapinzani hapo tarehe 31 October.

Dr Slaa , tell wananchi wasikubali kuwapa ufunguo CCM hapo October 31, with very simple reason, CCM hawajui kuendesha gari na watalitumbukiza tena shimoni right after election. BUT wawape Chadema ridhaa ya kuongoza hili gari walipeleke kule watanzania wanakotaka kwenda, lakini Chadema hawatawanyima lift CCM , CCM wakae tu kwenye siti ya nyuma ya gari litakaloendeshwa na dereva mpya DR Slaa likiwa na plate number ya CHADEMA. Tumia huu mfano kufunga mdahalo wako. I tell you Dr Slaa kama unasoma hapa utawakoga Watanzania walio wengi na wataelewa vizuri sana with that simple example.

La mwisho, waeleze Watanzania kuwa JK anawaogopa. Hata makanisani wachungaji na mapadre wana madarasa ya dini ambayo waumini wanapata fursa kuuliza maswali magumu, lakini pia wana wakati wa kuhubiri pasipo kuuliza maswali. JK amechukua njia ya kuhubiri sera, bila kuwakabili wananchi wapiga kura wake aweze kujibu maswali magumu. Huko ni kuwaogopa wapiga kura, na kiongozi wa jinsi hiyo hatufai

Alll the BEST Dr Slaa, Mungu akutie nguvu uuonyeshe ulimwengu kuwa kuna watanzania wenye akili na upako wa kuliongoza taifa letu
 
Anaona gere.

Uchagani kuna lami, maji, umeme, viwanda, vivutio vya utalii. Yet, HAWAITAKI CCM

CCM katu haileti vivutio vya utalii na uelewe kwamba CCM haina mpango wo wote na maamuzi ya Serikali. Serikali yo yote hata iwe ya TLP au chama gani ina mpango kazi wake. Tusiandikie humu kwa ushabiki wa vyama.
 
Ni vema Dr.Slaa akagusia wimbi la umwagaji damu linalosababishwa na wafuasi wa CCM akitolea mfano, Maswa Magharibi, Hai na pia azungumzie ununuzi wa shahada 185 uliofanywa na viongozi wa CCM.Hii iatasaidia kuelimisha jamii ielewe uozo wa chama cha JK NA SERIKALI YAKE wanavyojaribu KUBAKA DEMOCRASIA
 
Wadau wa karibu watupe Link kama ipo tufuatilie tulio mbali.
Kama atakuwa itv mnaweza kumuona live. ingia www.tv4africa.com then dowload player halafu lipa fees kidogo tu ya uero kama 5.58 kama dola 7 hivi then enjoy live itv for a full month na utamuona mpendwa wetu dr slaa bila shida, popote duniani utamuona
Kama una shida nijuliseh nikupe maelekezo zaidi mkuu
Ni vizuri ukalipa kwa paypal, is more secure
 
Tusisahau kazi ya kuhakikisha ushindi kwa chadema si ya Dr Slaa pekee yake. Sisi wote ambao tunapenda kuona Dr Slaa anakuwa Rais popote pale tulipo tuendelee na kampeni za nguvu katika hii wiki moja iliyobaki kwa kuwashawishi ndugu, jamaa, marafiki, majirani n.k. umuhimu mkubwa wa wao kumpigia kura Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema ili kuing'oa thithiem madarakani.
 
Back
Top Bottom