Naona kuna tu wana wadharau/under-estimate uelewa wa Watz, na uwezekano wa watanzania kuwapigia wapinzani bila kufanya uchambuzi wa kutosha.
CCM (JK) mwaka 2005 alishinda kwa mtazamo kwamba ni kijana, wa kisasa tofauti na viongozi wetu walipita, hivyo kulijenge dhana kwamba atakuwa tofauti, kinyume cha hapo watu walisha ichoka CCm.
Pili fedha nyingi iliyo tumika pia ilipeperusha mwelekeo wa watu wengi.
Tatu kutokuwepo na Kiongozi wa upinzani aliyekuwa ameridhisha watu kutokana na utendaji wake, na mapungufu mengine walio nao wapinzani kama Radio, TV na watu wa kutosha katika kugombea nafasi za Ubunge na propaganda machine zao kuwa na mapungufu kutokana na hali ya watanzani kuogopa kujihusisha na wapinzani.
Sasa miaka mitano baada ya uchaguzi, tumaini la watu JK amedhirisha kwa mba uwezo wake ni mdogo, pili madudu mengi yalio tokea katika jamii, na ufahamu huo ni wazi utazidisha vugu vugu la watu kutoipigia CCM, mafanikio aliyo pata Dr slaa katika kipindi hichi cha miaka 5 na kabla ya hapo ni plus nyingine.
Pili muamko wa wasomi wengi kuwaelemisha watu kuchagua upinzani unakua kila siku, sasa za ushabiki wa kumfuata tu mtu unapungua/umepungua na wengi wanao mfanyia JK ni wanafiki na yeye mwenyewe anajua hilo.
Kutokea kwa mgombea mwenye sifa zifaazo kama Dr Slaa kuna amsha ari na matumaini ya kuondoa uongozi mbovu mbovu, ndio maana leo hii unasikia watu Kilwa wana mzungumzia Dr Slaa, kama hawana mwamko huo wangemuongelea?
Kinachotakiwa Sasa ni Propaganda machine ya Chadema kufanya kazi kisayansi zaidi, kutumia wasomi wengi zaidi kufikisha ujumbe kila sehemu, iwe mjini au vijijini, na kutafuta wagombea makini kwa nafasi za uongozi, ikiwezekana hata kuwa-approach watu nje wale walio tayari ndani ya CHADEMa, eg wanaweza kumfuata Dr Sengondo Mvungi na kumuomba agombe jimbo fulani eg huko Same/Mwanga ikiwezekana hata hapo ubungo kama Mwanyika hawezi kutoa upinzani wa kutosha, tafuta Mtu mwingine nk nk.