Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
MH RAISI DR. W. Slaa nakuona hapa janvini

HONGERA kwa kupeperusha bendera ya chama chetu.

hii na wewe baada ya kuteuliwa na kamati kuu umefurahi kama mimi?
 
Naona kuna tu wana wadharau/under-estimate uelewa wa Watz, na uwezekano wa watanzania kuwapigia wapinzani bila kufanya uchambuzi wa kutosha.
CCM (JK) mwaka 2005 alishinda kwa mtazamo kwamba ni kijana, wa kisasa tofauti na viongozi wetu walipita, hivyo kulijenge dhana kwamba atakuwa tofauti, kinyume cha hapo watu walisha ichoka CCm.
Pili fedha nyingi iliyo tumika pia ilipeperusha mwelekeo wa watu wengi.
Tatu kutokuwepo na Kiongozi wa upinzani aliyekuwa ameridhisha watu kutokana na utendaji wake, na mapungufu mengine walio nao wapinzani kama Radio, TV na watu wa kutosha katika kugombea nafasi za Ubunge na propaganda machine zao kuwa na mapungufu kutokana na hali ya watanzani kuogopa kujihusisha na wapinzani.
Sasa miaka mitano baada ya uchaguzi, tumaini la watu JK amedhirisha kwa mba uwezo wake ni mdogo, pili madudu mengi yalio tokea katika jamii, na ufahamu huo ni wazi utazidisha vugu vugu la watu kutoipigia CCM, mafanikio aliyo pata Dr slaa katika kipindi hichi cha miaka 5 na kabla ya hapo ni plus nyingine.
Pili muamko wa wasomi wengi kuwaelemisha watu kuchagua upinzani unakua kila siku, sasa za ushabiki wa kumfuata tu mtu unapungua/umepungua na wengi wanao mfanyia JK ni wanafiki na yeye mwenyewe anajua hilo.
Kutokea kwa mgombea mwenye sifa zifaazo kama Dr Slaa kuna amsha ari na matumaini ya kuondoa uongozi mbovu mbovu, ndio maana leo hii unasikia watu Kilwa wana mzungumzia Dr Slaa, kama hawana mwamko huo wangemuongelea?
Kinachotakiwa Sasa ni Propaganda machine ya Chadema kufanya kazi kisayansi zaidi, kutumia wasomi wengi zaidi kufikisha ujumbe kila sehemu, iwe mjini au vijijini, na kutafuta wagombea makini kwa nafasi za uongozi, ikiwezekana hata kuwa-approach watu nje wale walio tayari ndani ya CHADEMa, eg wanaweza kumfuata Dr Sengondo Mvungi na kumuomba agombe jimbo fulani eg huko Same/Mwanga ikiwezekana hata hapo ubungo kama Mwanyika hawezi kutoa upinzani wa kutosha, tafuta Mtu mwingine nk nk.
 
Hata mm namuona mh Slaa akizisoma post zetu! Nasubiri majibu yake na nn anatushauri ili kampeni ifanikiwe!
 
Kura yangu, Ya Mke wangu na Ukoo wangu kwa Dr. Slaa
 
Jamani Karatu yangu! Bila huyu msee sioni nani anawesa pale bwana dha! Hifi kama Slaa nataka kupighania hii raisi ya Tansania nani tena itakuwa bunge yetu. Mimi naona mawaso yangu ni bora tu tuendelee ifi ifi paka hapo taona kuwa sasa nafaa kupighania hiyo cheo. Kama Slaa naondoka sisi atapata shida bana.
Mi staki kabisa hii ndughu akapigane huko bana dha!
 
Jamani Karatu yangu! Bila huyu msee sioni nani anawesa pale bwana dha! Hifi kama Slaa nataka kupighania hii raisi ya Tansania nani tena itakuwa bunge yetu. Mimi naona mawaso yangu ni bora tu tuendelee ifi ifi paka hapo taona kuwa sasa nafaa kupighania hiyo cheo. Kama Slaa naondoka sisi atapata shida bana.
Mi staki kabisa hii ndughu akapigane huko bana dha!

bange ... ooooppsssss .... what did u say again?
 
drslaabc.jpg


Ndugu pamoja na salamu zenu kwa Dr Wilbroad Slaa,

Mpeni nguvu ya kuanza kampeni sasa, kwa kutuma SMS zisizopungua 100

yenye neno CHADEMA kwenda 15710.

Kwa wateja wa zain na voda

Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Go Dr Slaa!
Kwa mara ya kwanza na kwa damira safi nitapiga kura yangu ya kuchagua Dr Slaa kuwa the next President! Mzee wa Kasi zaidi alidhani mteremko! Mbinu za ushindi zinatakiwa waeleze wananchi kinagaubaga watakuelewa na CCM tutaiong'oa
 
Ni Dr slaa tu ndiyo anaweza kuuondoa ufisadi hapa nchini -- akina JK na CCM yake wameshindwa kabisa!!! Nitampigia kura huyu Dr.
 
Je kuna aliye kwambia kwamba wengi wa ccm watashinda? labda kama wewe umekuwa Sheikh Yahya

duh! Mpo wengi hapa JF wa sampuli ya kukomalia kitu!. Unauliza swali la wazi hivi? Mimi nadhani Slaa kaingia choo cha kike. Mshaurini arudi kiumeni. Bungeni
 
Umefika wakati wa watu kusimama wahesabiwe kwani msitari tayari umechorwa, ama uko upande wa status quo au mabadiliko. Sasa sio muda tena wa kulialia au kutanguliza hofu, ni muda wa kila moja wetu kusema hapana imetosha na hatuwezi kuendelea kuwa watazamaji na huku taifa linateketea. Humu JF tunashuhudia wapiganaji wa kweli wakijitokeza wazi wazi na kuchukua msimamo huku wenzao, wale asilimia 70%, wakisubiri waone kwanza upepo unaelekea wapi. Hongera Dr. Slaa, sisi wengine hatuna hata wasi wasi kwani twajua Mkwere kenda na maji na huko Uspania saa hizi madaktari wako kazini kumzindua mtu kwani kimbunga chastua ati !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom