Mkuu Mg3,
Be realistic na acha siasa za JF za kwenye internet....wala sio siri kwamba CHADEMA haija enea nchi nzima na itachukuwa karne kadhaa kuenea. Hili halipingiki. Kampeni za miezi kadhaa kamwe haziwezi kuwashawishi wanavijiji wampigie kura Dr Slaa ambapo kwao neno CHADEMA ni msamihati wa kichina.
Nasikitika sana kwamba CHADEMA wanaishi katika Tz yakufikirika. Tz ya internet, Tz ya JF. Inasononesha kuona kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wanakesha JF badala ya kukesha mikoani na haswa vijijini wakijaribu kumomonyoa nguvu ya CCM. Wala sitashangaa kusikia kwamba uamuzi wa CHADEMA wa kumuua Dr Slaa kisiasa ulikopwa hapa JF.
Tatizo sio kwamba CCM haiwezi kuondolewa madarakani, tatizo ni kwamba HAKUNA UPINZANI wa kuiondoa. Upinzani wa kweli unaanza na kuimarika bungeni na sio IKULU kama CHADEMA wanavyotaka tuamini. Cha ajabu vyama vya upinzani tangu vianze vimekuwa "vikiua" wabunge makini kwa kuwafanya wagombee urais, na matokeo yake CCM inaendelea kujiimarisha. Ebu fikiria bunge ambalo lingekuwa na watu kama Lipumba, Seif Sharif, Mrema, Dr Slaa, Zitto, Mbowe, Marando, na vigogo wengine wa upinzani CCM ingekuwa katika wakati gani? CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinasahau kwamba umaarufu na ukomavu wa viongozi wao umetokana na kushiriki kwao katika Bunge na sio vinginevyo.
Kama kweli wana JF tupo hapa kwa maslahi ya kujenga nchi yetu na sio kujenga interests zetu, na kama kweli tunataka kuiondoa CCM madarakani kwa kuleta upinzani wa kweli ni lazima tuupinge uamuzi wa CHADEMA kumtoa Dr Slaa Bungeni. Kwasababu upinzani bado hauna nguvu katika maeneo mengi ya nchi silaha pekee tuliyonayo ni kuwa na wabunge wengi na makini Bungeni.