Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

HAPO KWENYE ST NAPO?
Mkuu labda anaweza kuapply ka Advanced Diploma yake katika utawala wake, ingawa kabobea katika maswala yake ya dini
 
kura yangu haipati mpaka anifanulie hasa udokta wake atautumia vipi wakati yeye ni dokta wa maswala ya dini?
Kwani huko kwenye dinin alikuwa anaongoza ng'ombe?
Au mtu anayekuwa kiongozi wa nchi hapaswi kuwa na elimu ya dini?
 
Hatuaangalii elimu ya mtu ila tunaangalia uwezo wa mtu katika kufanya kazi! hasa katika kusoma na kuelewa na kutoa mapendekezo yanayojenga. sasa kikwete ameitumiaje elimu yake kuuinua uchumi wetu ambao unazidi kudidimia?
 
neno labda ndio silitaki, sipendi nijaribu. Lkn bado mtu huchukuliwa kwa elimu yake ya juu na sio chini
lakini mkuu wewe unautambua u Dr wake? na siataa wala kwa mujibu wa katiba na si PhD yake, nini hasa wasi wasi wako katika hii PhD ya huyu muheshimiwa
 
Wenger,

Nadhani si vema kuikataa kura ya Malaria Sugu. Malaria Sugu kwenye Jamvi hili tunamjua wote kama mchokozi. Na wakati mwingine uchokozi wa aina hiyo ni mzuri. Hatuhitaji kutukanana. Kama yeye hatatoa kura yake hiyo ni haki yake wala tusimlazimishe. Na mimi nadhani hata kura yake tunaihitaji, hakuna kura ya mtanzania tunayoikataa, kura ni kura, kura haina sifa ya ubaya au uzuri bora ni kura halali. Thanksa wote, Thanks Malaria Sugu.
 
Malaria Sugu najua jinsi mbu wanavyokuwezesha ukadumu. Sisi tunafikiri njia pekee ya kuondoa malaria ni kuua mbu zote.
Hata hivyo uwanja wa kwanza wa kumpata rais ni asili yake. Kama anakubalika katika jamii yake basi huyu ana sifa ya msingi ya kukubalika.
Lakini sisi watanzania hatumchagui mtu kwa dini yake wale kabila lake wala proffession yake. Bali tunamtaka mtu ambaye atatuwezesha kupeleka jahazi la nchi hadi Kaanani.
 
DK SLAA NASHUKURU KWA MAJIBU
LKN NINA KISWALA KIDOGO TU

nasikia baadhi ya magazeti yansema umetumwa na wakatoliki kugombea. na mimi nikiunganisha phd yako na habari hiyo hua nahsi kuna ukweli jee kama muhusika unanitoa wasiwasi gani?
Malaria Sugu,
Kwanza neheshimu mawazo, maoni, michango na uchokonozi wako wote humu JF, na swali kama hili nilijua litakuja, na tena baada ya kuzinduliwa kwa kampeni rasmi,tarumbeta zitapigwa kama sio baragumu litalia kuwa huyu ndiye chaguo lengwa la ule waraka ili kupanda mbegu za sumu ya udini. Ningekuwa mshauri wa Chadema, ningewashauri kuangalia oparation ya Mahakama ya Kadhi ilivyooparate chini ya Mwingereza, na kuitumia modus oparandi hiyo kuwapa Waislamu kile wanachokitaka baada ya kuhadaiwa mwaka 2005 na wakatoa kura zao kwa matumaini ya kupata wanachokitaka,kumbe ilikuwa ghilba tupu, kwa kufanya hivyo, mtawakata vilimiliminwatu watu wa type ya Malaria Sugu na makuwadi wao wa kutaka kupandikiza mbegu za sumu ya udini.

Ushauri wangu binafsi kwako wewe Malaria Sugu, hakuna ubishi, chaguo lako linaeleweka bayana, ila pia twende kwenye ukweli, hebu pima genuine merits ya Dr. Slaa na hilo chaguo lako, ushabiki tuweke pembeni, nakushauri endelea kushabikia huku huko unakoshabikia, mikutano hudhuria, t-shirt na kofia vaa, pesa pokea na pilau kula, ila siku ya kupiga kura, nakuomba sana sana sana, piga kura yako kwenye ukweli wa nafsi yao kuhusu ukombozi wa taifa hili na sio kwenye ubatili kwa miaka mitano mingine.
 
Kwa taarifa yenu wote mliona na mashaka kuwa jimbo la karatu linarudi ccm baada ya dr.slaa kugombea urais, mfute hayo mawazo, anakuja mtu ambaye atashinda kwa kura zaidi ya alizopata dr. Mwaka 1995. Mimi ni mkazi wa karatu tunajua mbunge wetu ni nani kama chadema watampitisha basi ushindi wa chadema hapa ni hakika na jk hapati diwani wala mbunge hapa karatu. Msituone wairaqw wa karatu hatuna cha kusema mtusemee. Tuna watu wengi wenye sifa kama slaa, tunaomba mpigieni kura slaa tubadili nchi kiuchumi. Tumesikia mengi kuwa anaundiwa zengwe kuwa ana udini katumwa na katoliki jamani mnasahau wosia wa baba wa taifa? Dini ya mtu inatuhusu nini? Ni mtanzani mchango wake ameuonyesha kwa miaka 15 mnataka nini kwenye dini yake? Wengine wanahoji mbona mkewe ccm kwani nyie mwataka nini kwa mkewe. Siasa siyo vita jamani, tunajenga nchi moja tusigombee fito.
Nawasilisha mwenyekiti kwa niaba ya wana karatu.

Heshima kwako Jeneral Qoyo,
Nimependezwa na msimamo wako. Umesema kweli maana wairaqw tunamsimamo wa dhati. Watu hawakumbuki enzi za mwl Nyerere na Chief Sarwat. Wairaqw hawababaishwi na propaganda za CCM; Kwa bahati mwaka huu tutampeleka mtu mwenye kuvaa viatu vya Dr Slaa. Acheni uwoga. Siyo Karatu tu mwaka huu hata Mbulu ushindi ni kwa CHADEMA. Mwaka 2005 kati ya kata 16 JIMBO LA MBULU CHADEMA walipata kata 6 CCM KATA 10; Mwaka huu uwezekano ni mkubwa wa CHADEMA kuchukua kata nyingi;

Tusubiri mabadiliko makubwa
 
Chadema kama chama hawajaweza kulisemea iwe bungeni au nje bunge swala la mahakama hata kidogo kwa ghilba tu za watu kama PAdre SLAA unafikiri watalisema wakati huu ..ukweli ni kwamba hawawezi kwakuwa ni WAKATOLIKI PURE! na maagizo ya maaskofu hawana jeuri ya kukiuka..

SLaa hana uwezo wa kumsaidia muislamu na mahitaji yake wala hana habari nazo (out of touch)..mahitaji ya waislamu yataletwa na wenyewe tena kwa nguvu....na wala si chadema

BIG NO TO PRIEST

We Tumain, usianze kutuletea ujahidina wako hapa kwa uteuzi wa Dr. Slaa kwa kumuita padri, mara katumwa na maaskofu mara ohh..
Kama Rais ni Muislamu, Makamo wa Rais Mislamu, Rais wa Zanzibar Muislamu, Waziri Kiongozi Muislamu, IGP Muislamu, mkuu wa TISS Muislamu, etc etc, top cream yote hiyo haijaweza wasaidia kupata hicho mtakacho, mpaka kwenye ilani japo ni kiini macho lakini kiliwekwa, hamjaamka tuu na kukubali mabadiliko?!.

Dr. Slaa is more than what he is, yeye ni kwa maslahi ya Taifa.

Natamani sana Wakala wa Mkemia Mkuu, wamfanyie DNA Prof. Lipumba ili kuthibitisha wale Wanyamwezi wa Zanzibar ni ndugu zake wa kinasaba, conclusion iwe kumbe Prof. Lipumba ni Mzanzibari, memorandum ya ushirikiano kati ya CUF na Chadema iandikwe na kusainiwa, Dr. Mgombea, Prof. Mgombea mwenza, au Juma Duni,
October 31, itakuwa kwisha kazi, kama kumsukuma mlevi, na mahakama yenu ya Kadhi mnapewa ndani ya miezi 6 tuu, jee bado mnataka nini?.
 
Malaria Sugu pole sana. Kwa dhima ya jina lako ninajiridhisha kuwa Mbu wamekufanya ukaendelea kuwepo na kutamba sana. Lakini kwa hakika malaria imetesa na kuua wengi. Kwa sasa tumeamua kutafuta ufumbuzi wa kudumu dhidi ya malaria kwa kuanza mkakati wa kuua mbu wote na mazalia yake.

Malaria unahoji shule na udini wa Dr. Slaa. Sina uhakika kama umetumwa lakini ninajua ili malaria iwepo lazima kuna mbu kapuliza plasmodium. Kwa hakika wachambuzi makini wanaamini kuwa rais bora lazima kwanza akubalike kwake. Hili la Dr. Slaa kukuballika kuanzia kwenye dini yake hadi kwa waislamu linatupa picha kuwa amepata sifa ya kwanza kabisa ya urais ya KUKUBALIKA. Hata hivyo sisi watanzania makini hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake wala proffession yake. Tunachamgua na kumpigia debe mtu ambaye atatuwezesha kuifikia KAANANI yetu.

Dr. Wilbroad Peter Slaa ndiye!!!
Naam Tanzania mpokee rais wako akufikishe Kaanani.
MAFISADI KWETU MWIKO
 
Wapenzi wengi wa chama chako wana sifa ya kutuweza kuvumilia mawazo mbadala hasa yanakuhusu wewe na background zako za KIKANISA na UDINI (kielimu na kimalezi)....

Naamini hustahili kura hata moja kutoka kwa MUISLAMU mwenye chembe ya IMANI kwakuwa kitakachofuata baada ya hapo ni kufunikwa kwa uislamu Tanzania na kuingiza ukatoliki maana ndiko ulikobobea (PhD) ...

Sorry nenda kanisani kaongoze kwenye urais unataka kuleta maafa na mgawanyiko mkubwa katika..ushauri tu kwa ajili ya Tanzania yetu..

Je mahakama ya kadhi ikipatikana matatizo yatakuwa yameisha????

mahakama ya kadhi sio tatizo, tatizo ni elimu. Nimetoka tanga na Unguja juzi hali inasikitisha.
unguja vijana hawataki shule na kila mtu ana mke zaidi ya mmoja na watoto kibao.
tanga vijana wengi hawataki shule na wanawake wanaolewa mapema sana. vijana wengi wavivu na hawapendi kujishughulisha. Sasa hivi wageni kutoka mikoa mingine wanaenda wanafanya biashara pale pale wanajenga na watu wa tanga wanaanza kulalamika na kusema kuwa wageni wanachukua biashara zetu na wake zetu
 
Dr Kitila
naona mmetupelea MASHINE, mwaka huu ni defrao tuu! Ni kujipanga vizuri tu kipindi hiki kifupi cha kampeni. Mola awape hekima na nguvu zaidi.
 
kura yangu haipati mpaka anifanulie hasa udokta wake atautumia vipi wakati yeye ni dokta wa maswala ya dini?

Kikwete ana degree ya uchumi, je imesaidiaje katika maendeleo ya nchi? Mbona ni bora hata ingeongozwa na aliyesoma degree ya kucheza mziki pale fine and performing art? Kwa sababu pamoja na uanauchumi wake, uchumi wa nchi umekwenda kombo. Ameshindwa na Mkapa aliyesoma kiingereza na kiswahili na bado akafanikiwa kujenga uchumi imara wa nchi, akafanikiwa kupunguza mfumko wa bei kutoka asilimia 27 hadi asilimia 5. Kikwete ameingia, ndani ya miaka mitano tu kaongeza mfumko wa bei kutoka asilimia 5 hadi 14. Huo uchumi wake umeisaidiaje nchi?
Kwa taarifa yako kinachoongoza si umesomea nini bali ni intellectual capacity ya mtu. Uwezo wa kuchambua mambo na kuyapangilia ipasavyo.
Take care!
 
hata kwa waislam. nipe ushahidi?
Mkuu hebu anza na chama tawala waulize kama wameshindwa tangu 2005 kuwaletea waislam hicho mlichokitaka je baada ya uchaguzi wataweza? Kumbuka JK ndo mdini kwani huyu mgombea wake mwenza ni watatu na wote ni waislamu na wameshindwa kuwaletea hicho waislam mlichokitaka.Sasa ni zamu ya waislam kugeukia upande mwingine...........DR SLAA NDIO TUMAINI LETU WOTE WAISLAM,WAKRISTU NA WAFANYAKAZI.
 
We Tumain, usianze kutuletea ujahidina wako hapa kwa uteuzi wa Dr. Slaa kwa kumuita padri, mara katumwa na maaskofu mara ohh..
Kama Rais ni Muislamu, Makamo wa Rais Mislamu, Rais wa Zanzibar Muislamu, Waziri Kiongozi Muislamu, IGP Muislamu, mkuu wa TISS Muislamu, etc etc, top cream yote hiyo haijaweza wasaidia kupata hicho mtakacho, mpaka kwenye ilani japo ni kiini macho lakini kiliwekwa, hamjaamka tuu na kukubali mabadiliko?!.

Dr. Slaa is more than what he is, yeye ni kwa maslahi ya Taifa.

Natamani sana Wakala wa Mkemia Mkuu, wamfanyie DNA Prof. Lipumba ili kuthibitisha wale Wanyamwezi wa Zanzibar ni ndugu zake wa kinasaba, conclusion iwe kumbe Prof. Lipumba ni Mzanzibari, memorandum ya ushirikiano kati ya CUF na Chadema iandikwe na kusainiwa, Dr. Mgombea, Prof. Mgombea mwenza, au Juma Duni,
October 31, itakuwa kwisha kazi, kama kumsukuma mlevi, na mahakama yenu ya Kadhi mnapewa ndani ya miezi 6 tuu, jee bado mnataka nini?.
Bila kumsahau Mzee mwenye hati miliki ya CCM Yusuph Makamba. Mkuu Pasco hii PHD ya JK na Karume ni za nini kweli?
 
NI UJINGA SANA NA NI UPUUZI kumuona mtu hafai kugombea kutokana na dini yake. Kama watu hawatamchagua Kikwete kwa kuwa ni muislamu itakuwa ni ujinga na akili finyu. Na kama wakimchagua kwa kuwa ni muislamu utakuwa ni ujinga zaidi. Same applies to Dk Slaa. UDINI ni UJINGA. We are Tanzanians first, baadaye ndio zinakuja dini zetu na makabila yetu. lakini kwanza baada ya kuwa watanzania.
 
kura yangu haipati mpaka anifanulie hasa udokta wake atautumia vipi wakati yeye ni dokta wa maswala ya dini?

kwanza kura yako haitasaidia..bora ukae nayo uendelee kumkampenia kilaza wenu JK
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom