Hana hoja hapo, sababu ameongea uongo tena kwa ujinga wake.
Kwanza Uislamu ndio dini pekee ambayo imekuja kuondoa ubaguzi, na kuonyesha ya kuwa mbora mbele ya Allah ni mchamungu.
Anasema Allah aliye juu :
13. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
(al-Hujurati : 13)
Hapo hakuna cha uarabu Wala uafrika.
Kingine ama kuhusu lugha, lazima iwe Kiarabu ili kuleta usawa na kuwaleta watu wote pamoja. Sababu Mtume alikuwa muarabu, na aliletwa akiwa katika jamii ya waarabu, ili wamuelewe kwanza ilibidi itumike lugha ya Kiarabu. Ajabu ya Kiarabu Leo hii unakuta muafrika anamfundisha Kiarabu muarabu mwenyewe.
Lakini Uislamu umekuja na msamiati ambao Waarabu walikuwa hawaujui waarabu kabla, bali Sheria na taratibu. Bali Kuna baadhi ya tamaduni ambazo Uislamu ulizichukua kutoka kwa waarabu, sababu ni nzuri na walikuwa wameshastaarabika.
Kadhalika katika Hadithi, Mtume wa Allah, amani ya Allah iwe juu yake anasema :
Abu Huraira reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “
Verily, Allah does not look at your appearance or wealth, but rather He looks at your hearts and actions.”
Source: Ṣaḥīḥ Muslim 2564
Lakini laiti kama Uislamu ungekuwa ni Uarabu basi waarabu wote wangekuwa Waislamu.
Kingine, lazima utumie lugha ya Kiarabu ili dini ihifadhike na isichafuliwe kutokana na makosa, ndio maana katika sababu zilizopelekea vitabu vingine kuwekewa mikono ya watu ni kuweka lugha zao katika vitabu vyao.
Kwahiyo kwa ufupi tunahitimisha ya kuwa Umar Johnson hakuwahi kuujua Uislamu ajabu akawa anauongelea.