DRC imeingia makubaliano na Marekani pamoja na China ufanyikaji wa majaribio ya kinga ya Corona nchini mwao

Waje huku tuwape vijana wa ufipa tutawapa bila mkataba

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Dawa za kutibu binadamu huwa zinajaribiwa kwa binadamu, mnataka majaribio yafanyike wapi?
Kwa wanadamu wenye matatizo,ilo tu huwez fikir & nyinyi ndo mnatufanya Afrika tuonekane utumbo,mmekuwa YES MAN kwny kila ki2,ulaya watu wanakufa 500+ kila siku,kwnn wasianzie huko?

Ni kwmb kwny majaribio ya chanjo lzm wapandikize maambukiz kupima nguvu ya chanjo,Je ni wote watapewa chanjo NO,Je ambao hawajachanjwa huoni watakua kwnye hatari ya kuugua corona pindi watakapo kuja in contact na maambukiz?

Je hawa wanafanya majaribio wako tayari kutake risks za side effects za majaribio yao au ndo watatutelekeza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi China wametumia nn kumaliza tatizo ? Walifanya test wapi?

Ila China na US wana maslahi makumbwa Congo
 
Nani ametoa hizo tahadhari?
 
Wacongoman mnajifanyaga wajanja mara papaa mobimba, kumbe na nyie ni wapuuzi kiwango cha lami. Wewe watu wanapinga majiribio kufanyika africa, nyie ndo mnatuangusha mnajipeleka kufanyiwa majaribio. Labda tuanze kuwaita guinea pigs.
Wametuangusha sana WaAfrika
 
Licha ya Waafrika wengi wakiwemo Watu mashuhuri kama Eto’o na Drogba kupinga mawazo ya Maprofesa wa Ufaransa Jean Mira na Locht ya kupendekeza Afrika kutumika kama sehemu ya kufanyia majaribio ya utafiti wa kinga ya corona, Congo imesema ipo tayari majaribio yafanywe nchini humo.

Mkuu wa kikosi kazi cha kupambana na corona katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema Nchi hiyo imejiandaa na ipo tayari kwa jaribio lolote linalolenga kupata kinga ya corona itakayosaidia Duniani>> “njia pekee ya kuzuia corona ni kupata kinga kama tulivyofanya kwenye Ebola”

“Tayari tumechaguliwa kufanyiwa majaribio ya kinga ya corona, kinga inazalishwa Ufaransa,Marekani, Canada au China, tupo tayari kwa majaribio tena nafikiria yaanze mapema na isizidi July kama itachelewa sana August”-Jean-Jacques Muyembe, Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Biolojia Congo
#MillardAyoUPDATES

Source Millard Ayo Fb page.

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
#Say no to lockdown.
#Say no vaccine test for COVID-19 To fellow Africans
 
Hawa viongozi wengine sijui wanawazaga nini? Wazungu wanatuchukulia sisi Kama nyani, that's why hata majaribio wanataka kuyafanyia kwetu.

Kwani kati ya bara letu na mabara mengine ni wapi wameathirika zaidi? Kwanini majaribio yasifanyike huko walikoathiriwa zaidi?

Naamini mzee wetu na timu yake hawataruhusu hilo hapa home.

Mungu ibariki Tanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jameni inafanyiwa wapi hii nijitolee kuwa wa kwanza Afrika kufanyiwa uchunguzi, wanaopinga nawaona bogus sana full mipumbavu. Afrika hii tunahitaji kinga kwa haraka sana kabla hiki kirusi hakijatinga kwenye mitaa ya mabandani, maana kikifika huko itakua ndio basi, kiama.
Mataifa ya Afrika hatuwezi kwenda lockdowns wanazofanya wazungu kwao, wao wana uwezo wa kupeleka canned food kwa watu wao, wana uwezo wa mambo mengi, sisi hapa Afrika wacha hata chakula, kuna mitaa maji yenyewe tabu, huduma za jamii kuzipata mabandani ni balaa, vijijini kule ndio usipime. Acheni unafiki, waachieni wazungu watuletee kinga na tiba, maana hata wanasanyi wetu leo hii wamelala tu hamna lolote, hawachangii kwa chochote, na wao wanasubiri mzungu agundue dawa.
 
Tino,
Kitu fulani kinaanza kuingia kichwani mwangu.Nadhani COVID-19 ni coverup ya 5G kuhusika na mauaji ya watu,huku juhudi nyingi zikifanywa kutuaminisha kwamba COVID-19 is a viral disease.Na sasa inaanza kudhihirika kwamba Marekani na China wanahusika katika conspiracy ya COVID-19, because why the alliance.Kama kweli China wanaamini Marekani ndio waliowarushia hilo zengwe,si kingepigwa,mbona kimya,tens urafiki ndio unazidi?Lao hawa ni moja,hamna lolote.We must have critical thinking.

Halafu huyo kiongozi wa Congo naye poyoyo kweli,hivi anajua kweli hatari itakayowakumba watu wao kwa kupewa hiyo chanjo?Yaani anaona kawiini.Nadhani hajui kwamba hiyo ni sumu,maskini wee,kweli usichokijua ni usiku wa giza.
 
Wametuangusha sana WaAfrika
Sana,yaani dah!Mbona Africa hatuna shida,si hiyo chanjo ingeanzia huko Marekani na Ulaya kwenye matatizo zaidi?Yaani Wakongomani mapoyoyo kweli kweli,can't they see the danger ahead of them.Aibu sana.
 
Naamini kuna mataifa mengine yatakubali kimya kimya.
Maadamu watapewa pesa lazima wakubali tu.

Japo hiyo chanjo kufanyiwa majaribio huku Africa naona ni vizuri maana ikifanikiwa tutakuwa na uhakika wa kuendelea na maisha ya kawaida bila hofu kwani huu ugonjwa ukisambaa sana huku Africa hatutaweza kuudhibiti.

Ukisema nchi za Africa zifungie raia wao majumbani basi njaa itawaua isitoshe hawa wanausalama watatumia hicho kigezo kutesa wananchi hivyo ni bora chanjo ije ianzie huku.
 
Wapo wengi sana hawana hasara kwa raia zao wakifa.

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
Kwa hiyo we should stay home for our
entire life ili tu kuikwepa Corona?
Haohao waliowatajia preventive measures za corona ndio haohao wanatafuta chanjo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…