DSM ngumu, inahitaji RC wa viwango fulani. Nashauri Antony Mtaka aletwe hapa atatusaidia sana, vinginevyo bora hata Makonda arudi

Niliwahi kushauri huko nyuma (2022), soma hapa: Serikali ijaribu sera ya madaraka mikoani, yaweza kabisa kuibadili nchi yetu ndani ya kipindi kifupi juu ya kubadili sera ya madaraka mikoani ingafaa sana kuwapata watu wa aina ya huyo unaempendekeza.

Watu hawa RC na mameya wa majiji ni watu ambao wapaswa kuchaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura.
 
Sawa, Bro. Mayalla, lakini PR engagements zako na RC Mtaka zimekujengea conflict of interest na kutia doa recommendation yako ya yeye kuhamishiwa Dar!
 
Mtaka ni Next Generation
Huyu Raper wa Kinyaru hana chochote anachofanya Dar
Jiji chafu, huduma za kijamii zimedorora yeyw yupo tu
 
Hiyo haitatofautisha wabunge na Wakuu wa mikoa

Hawa wawe wanaomba kazi wanafanya interviews Kwa panels of experts na kuchujwa na kupewa contracts
Kuna tofauti kubwa. Mkuu wa mkoa ni chief executive wa mkoa. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, na aspect moja ya kazi yao ni kuisimamia Serikali.
 
Hao wakuu wa mikoa walipaswa kuchaguliwa na wananchi kwenye chaguzi na si kuteuliwa na raisi.
Naunga mkono hoja, hawa ni sawa na magavana, walipaswa kuchaguliwa na wananchi, hiki kinachoendelea kwa hawa kuteuliwa ni muendelezo wa the colonial legacy tuu, na Tanzania hatujawahi kupata leaders of change, transformational leaders kuondoa huu ujinga wote wa colonial legacy, mfano baada ya kuwa na wakurugenzi wa halmashauri, ma DC ni wa nini?!. They are totally redundant, they are wastage of time, money and resources!.

Yule Blaza wangu angeendelea, angeachana na ujinga wa colonial legacy!, alianza anza kwa kuiweka kando katiba!.
P
 
Watendaji wa chini hutenda vile ambavyo humtazama kiongozi wa juu anatenda, akitenda vema nao watatenda vema, mkuu akitenda kimzaha nao watatenda kimzaha mzaha..Kwa wakati huu daslam hata akiletwa malaika kuongoza atapiga blaablaa tu...btw Mtaka ni kiongozi mzuri.
 
Sawa, Bro. Mayalla, lakini PR engagements zako na RC Mtaka zimekujengea conflict of interest na kutia doa recommendation yako ya yeye kuhamishiwa Dar!
Mkuu Pucha, Pulchra Animo , sijawahi kuwa na PR engagement na RC Mtaka, bali ni kwenye news asignments tuu, he is a doer!. Enzi za JPM he was the best RC, ndio akapelekwa Dodoma!.

Kwa serikali nawafanyia pure news, ila kwa makampuni ndio kuna PR!.
P
 
Mnataka wapinzani wawe wenye viti wa kamati ya ulinzi na usalama ili wachukue nchi kiulaini sio ? 😁 uwo ni mtego ambao ccm hawatoingia kamwe
 
Una upendo na wasukuma wenzako.Huna dhambi.
 
Acheni kumsagia kunguni chalamila,

Pale Muhimbili ikiwa maiti yako itakufa na deni haupewi uwo mwili kwenda kuupunzisha mpk ulipe deni la watu mnaona ni sawa tu,

ila ajabu ni mama mzazi kurudishwa hospt ikiwa atakosa glavu kwani ile mimba iliingia kwa bahati mbaya au?
 
Sawa aliyepo hafai kabisa na hii ni shida ya kimfumo kwani mfumo CCM uliopo ni mbaya sana kwa maendeleo yetu.
 
Chalamila ni mgonjwa wa muda mrefu akili yake imelika kiasi fulani Ila nyie mnaona Kama mwenye masihara Ila kichwani hayuko sawa I know him personally.
 
Kosa lipo kwa mteuaji. Sijui huwa anatumia vigezo gani?
 
Rais mwenyewe anasema kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake na kifo ni kifo tu, unategemea nini kwa wateule wake?
 
Kuna huyu mkurugenzi wa mabasi ya mwendokasi mh Waziri Kindamba.. Yule mwamba mikoa yote aliyopita alifanya mabadiliko chanya. Songwe aliipandisha sana kimapato na maendeleo, Tanga chini yake ilishaanza kuja juu. Ajabu katolewa kule na katika sababu alizotoa mama eti jamaa ni mkali.,lakini Chala anaachwa pamoja no upuuzi wake wote. Nchi ya ajabu sana hii!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…