DSM ngumu, inahitaji RC wa viwango fulani. Nashauri Antony Mtaka aletwe hapa atatusaidia sana, vinginevyo bora hata Makonda arudi

nadhani,
bila chuki binafsi, upendeleo, urafiki na mapenzi binafsi kwa viongozi hawa wa mikoa,

nadhani dar es salaam ni tulivu mno na yenye kupiga hatua zaidi za maendeleo kwa sasa, huenda kuliko kipindi kingine chochote kilichopita hususani katika maeneo ya usalama, miundombinu, elimu, maji, afya n.k

mnyonge mnyongeni,
ila haki na maua yake apewe bila chuki binafsi, licha ya kua ni binadamu mwenye mapungufu na madhaifu kwa maneno na matendo kama walivyo wengine 🐒
 
Hapa nakukatalia katu!
Kuna mikoa ya makabila mengi na mingine ni kama kabila moja, hivyo Kagera ni kwa Wahaya japo kuna Wahangaza, Moshi ni kwa Wachagga japo kuna Wapare, Mbeya Wanyakyusa japo kuna Wasafwa, Iringa Wahehe japo kuna Wabena.

Hata Wasukuma japo ni kabila moja, ndani yake kuna vikabila.
P
 
Babu @pascalmayalla nani kakuambia Kilimanjaro ni mkoa mlaini .... Nani kakudanganya?? ILA CHALAMILA ULEVI UNAMSUNBUA ANAROPOKA HOVYO. Aache pombe.
Chalamila akiongelewa vibaya huwa nachukia Sanaa.
Mbona yupo vizuri TU. Na kwenye hizi thread msema mabaya yake na mazuri yake pia.
 
Kwa Mara ya kwanza nakubaliana na wewe gentleman 😊

Mimi sijaona ubaya wa chalamila anywhere linalo zungumzwa hapa sijui ni kwa Nini.
 
Eti kilimanjaro ni mkoa mlaini, tangu lini bwana Pasikali?
 
Africa ita endelea kua katika kundi la developing countries na katu hatutofikia kwenye developed countries
Tunaitaji watu aina ya TRUMP ili tuendelee na hao watu ndio Kama THE LATE JPM, watu Kama CHALAMILA watu Kama makonda .
Sijaona ubaya wa chalamila anywhere zaidi ya maneno ya ukweli mtupu kusema watu wachangie huduma za afya in the hard way ( refer nenda kwa mmeo akussidie kujifungua) chalamila yupo sahihi.
 
Hata mimi naona kama wewe, sioni kosa lolote kwa Chalamila

Nina watoto watano hakuna hata mmoja mke alijifungua bure akiwa hospitali tena mara zote ni hospitali za serikali
 
Hata mimi naona kama wewe, sioni kosa lolote kwa Chalamila

Nina watoto watano hakuna hata mmoja mke alijifungua bure akiwa hospitali tena mara zote ni hospitali za serikali
Sahihi mkuu..labda chalamila kutumia lugha ngumu ndio tatizo?? .maana tumezoea kudanganywa na maneno matamu matamu.
Ni muhimu Sanaa kuchangia huduma maana mimba sio dharula ama ugonjwa ni kujiandaa..naamini tupo sahihi kwa huu mtazamo.
 
Na waliosoma naye wanasema alikuwa n mtukutu mno na mvuta bange
The late JPM pia kabendera kamtuumu kuvuta bange. Kama Bangi inaleta maamuzi na kutengeneza viongozi wakubwa wazuri wenye maamuzi Basi Bangi ni nzurii na ivutwe na viongozi wote ili tupate viongozi Bora.
 
Siwez ongera habari za dar wakat sikai dar wala sjui ni faida au hasara gam watu wa dar wanapata kutoka kwa uyo Rc

Ila nlikua nauliza tu kwann serikal isiwe inaajiri wazawa ktk baadhi ya nafasi
Kwann isiajiri mtu wa dar kua Rc au Dc hii inaweza saidia kuleta maendeleo haraka lakin hii ya kuchukua mtu wa tabora unampeleka kua kiongozi Ruvuma
 
Mjomba wangubChalla ni ropo ropo huwa naamini hashirikishi ubongo na fikra zake akiwa anaongea....huyu anafaa propaganda za chama....lakini kuwe na mtu kumdhibiti DSM angetolewa ....yaani bado hajakomaa kwenye uongozi ...jazba na mihemko yake....
For sure, zile shughuli za kubwatuka bwatuka ilifaa angekuwa chamani.
 
Chalamila akiongelewa vibaya huwa nachukia Sanaa.
Mbona yupo vizuri TU. Na kwenye hizi thread msema mabaya yake na mazuri yake pia.
Sawa... Endelea kuchukia maana hamna namna atasafishika uropokaji wake. Mazuri yake yaseme wewe, hamna anayekuzuia ..
 
Umeongea Point Kubwa Mkuu... Ila Hapo Shida Wala Sio Chalamila... Shida Aliyewateua Anajua Na Alijua Kabisa Uwezo wa Chalamila Ni Mdogo Sababu Alishaboronga Hapo Nyuma. Ila Kwa Kua Uongozi Wetu Ni Kujua Huyu Mtoto Ndugu Au Rafiki Wa Nani Ndio Unakula Shavu... Hapa tutamlaumu Mama!! Baada Ya Kujua Uwezo Wake Mdogo Siku Ya Kumuapisha Bado Alim'term Kama "Mwanangu" Kumaanisha Anambeba Tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…