DStv hawataonesha michuano ya AFCON mwaka huu, Azam Tv atangaza kurusha mechi zote

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kuna barua mtandaoni inatembea ya kampuni ya Multichoice (DStv) kuhusu kutokuonyesha matangazo ya michuano ya Afcon mwaka huu ambayo itafanyika huko Ivory Coast baada ya kukosa haki za matangazo.

Kwa upande wa pili, AzamTv wametangaza kuonyesha mubashara mechi zote za Afcon yaani mwanzo mwisho.

Kongole sana kwa Azam TV hakika soka la Afrika mnalitendea haki.
 
Tangazo la biashara hili..
Lipia.
 
DStv wameanza kupoteza umaarufu wake waliojizolea kipindi cha nyuma hasa hapa tanzania baada ya AZAM TV kufanya mapinduzi makubwa, AZAM TV nikama wanautaka ufalme wa matangazo ya televisheni kwa sasa hapa bongo,
 
Leseni ya Azam ni kurusha Tanzania tu
 
Sidhani kama ni kweli DSTV wameandika hayo, hiyo barua imekaa kipropaganda kwa 100%.

Katika hali ya kawaida, kituo cha Tv kikosa haki ya kurusha matangazo fulani huishia kukaa kimya, wateja wenyeji watachambua mchele na kujiongeza.
 
ITV haijawahi kuonesha bure EPL ni Uefa. DTV then (sasa Chanel Ten) iliwahi kuonesha baadhi ya mechi
I see! Ina maana nimechanganya madawa? Nakumbuka miaka hiyo nilikuwa naangalia sana kina Michael Owen na enzi za kocha Wenger wakati Arsenal inacheza kama mashine. Ilikuwa ni DTV kumbe! Labda kumbukumbu yangu ni mbaya, lakini nakumbuka kuangalia kwenye channel ya ITV, mashindano yote, i.e. PL na UEFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…