DStv hawataonesha michuano ya AFCON mwaka huu, Azam Tv atangaza kurusha mechi zote

DStv hawataonesha michuano ya AFCON mwaka huu, Azam Tv atangaza kurusha mechi zote

Yaan TBC na quality Ile kama tv za mbao miaka ya 80 ' waachane kabisa na afcon wao waonyeshe ziara za mama tu Mpira chakwanza ni quality HD ya maana. Kama ni kweli DStv kazingua asee
Mkuu utakuwa unatumia tv ya star x LED na king'amuzi cha startimes cha antena kile kisicho na port ya hdmi
 
I see! Ina maana nimechanganya madawa? Nakumbuka miaka hiyo nilikuwa naangalia sana kina Michael Owen na enzi za kocha Wenger wakati Arsenal inacheza kama mashine. Ilikuwa ni DTV kumbe! Labda kumbukumbu yangu ni mbaya, lakini nakumbuka kuangalia kwenye channel ya ITV, mashindano yote, i.e. PL na UEFA.
Uko sahihi .
Dstv walionesha epl yote bure...mechi zote.. halafu itv na wao wakapigania wakaja onesha mechi zote za EPL buree kabisa.
Wanaobisha ni wale miaka hiyo hawakuwa na TV...
Wengi walianza nunua TV baada ya itv kuonesha mipira...wakati TV ya kwanza kuonesha afcon nchini ni CTN... January 1994 Rashid Yekini akawa mfungaji Bora hapo itv haipo... ITV ikaibuka June 1994 wakalazimisha Sana waoneshe world cup hadi Mengi akaja kudai wahindi wamemtishia maisha ...akimaanisha CTN na Dtv ..😀those were the days
 
Ni Uefa. EPL ni DTV ndo alikoibukia Dr Leaky
Dtv alikuwa kidedea Sana kwenye michezo....itv walijaribu Sana kushindana na Dtv kuna siku waligombania pambano la mike Tyson ...itv wakapata kashfa walionesha recorded na sio live😀
Itv pia aliwahi onesha EPL baadae ..Dtv ndo walikuwa Baba lao...
Lakini afcon ya 1994 January ilioneshwa na ctn...itv akaja onesha world cup June 1994 baada ya Mengi kufanya fitina na kuishawishi FIFA kuwa itv ndo local channel ya taifa...itv ilijulikana kama ndo TV ya taifa...Mengi akaanza kuweweseka kuwa wahindi wanataka kumua. Serikalini ikampa ulinzi .. where is Pascal Mayalla ...
 
Nani anakudanganya Azam yupo Tanzania,Kenya, Uganda,Rwanda,malawi na Zimbabwe.
Kwa hiyo mpaka miaka 10 ijayo atakuwa karibu nchi nyingi za africa yupo nimesahau na nchi ya zanzibar.
ukishaweka nchi ya Zanzibar basi Tanzania inakuwa haina maana tena bali Tanganyika
 
Yaan TBC na quality Ile kama tv za mbao miaka ya 80 ' waachane kabisa na afcon wao waonyeshe ziara za mama tu Mpira chakwanza ni quality HD ya maana. Kama ni kweli DStv kazingua asee
Dstv huwa wanataka monopoly...
Wakiona cha wote wanajitoa. Hovyooo
 
I see! Ina maana nimechanganya madawa? Nakumbuka miaka hiyo nilikuwa naangalia sana kina Michael Owen na enzi za kocha Wenger wakati Arsenal inacheza kama mashine. Ilikuwa ni DTV kumbe! Labda kumbukumbu yangu ni mbaya, lakini nakumbuka kuangalia kwenye channel ya ITV, mashindano yote, i.e. PL na UEFA.
UEFA ilikuwa ikirushwa ITV baadae wakaja channel ten.

EPL ilikuwa ikirushwa mubashara DTV
img_2_1704342279745.jpg
 
Kuna barua mtandaoni inatembea ya kampuni ya Multichoice (DStv) kuhusu kutokuonyesha matangazo ya michuano ya Afcon mwaka huu ambayo itafanyika huko Ivory Coast baada ya kukosa haki za matangazo.View attachment 2861137

Kwa upande wa pili, AzamTv wametangaza kuonyesha mubashara mechi zote za Afcon yaani mwanzo mwisho.View attachment 2861138

Kongole sana kwa Azam TV hakika soka la Afrika mnalitendea haki.
Azam wanajitahidi kuonesha matangazo ya mpira lakini wanazingua kwenye baadhi ya mambo, wanapeleka kamera chache viwanjani, kama mtu unafuatilia matangazo ya mpira Mapinduzi Cup utakuwa umeshapata kero hii, kuna upande mpira ukiwa unachezwa unaona vivuli tu, hakuna raha ya kuangalia unatamani mpira uwe unachezwa upande mmoja ili uone.... wajirekebishe .
 
Back
Top Bottom