DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

Azam quality ya picha itatuhamisha DStv naona kuna low quality picture,DStv Wana HD,pia azamu Wana mavipindi ya hovyo nje ya mpira,DStv Wana documentary za utafiti baharini,upishi 175 na 174 hii na zile animal channels na TNT movie na multchoice movie zote na African magic zote,Azam wakaze boot,quality is a number one factor.
Brother Kwa hiyo unachopenda wewe unataka dunia nzima tupende?
 
Hilo la kupunguza vifurushi haliwezekani mkuu kumbuka leseni ya kuonyesha EPL wanalipia zaidi ya USD Mil 900$ kwa mwaka sasa unadhani hizo hela za kulipa watatoa wapi?...

Tena unaambiwa Premier League Production wameipunguzia sana DSTV gharama za Kurusha ligi yao wangeweka bei sawa na vituo vingine huko Duniani Kama Sky Sports, Bein Sports Canal Sports nk labda ni asilimia 1% tu ya waafrika wangemudu kulipia DSTV
Why canal a afford kulipia bei kubwa alafu package yake ya epl iwe cheaper?
 
Voda mi nilisajili Router ya 5G ni unyama sana speed ya 50Mbps. Kwa kuanza unalipa deposit ya 300,000 kisha unafunguliwa data mwezi mzima. Upon renewal unalipia laki na nusu kila mwezi kwa muendelezo. Ila nzuri sana hata kwa wale wenye ma smart TVs zinaweza kuwa na uhai kupitia hizo routers.
Ndio ni yule yule tu kwenye avatar picha yako lakini ile ya mwanzo tuliizoea sana. Ja rule!
images.jpeg
 
Wafanye Compact 40,000/- waone wateja watavyoongezeka.
Mimi nilikuwa nalipia Shangwe 34000/- walivyopandisha 37000/- huku hawaonyeshi CAF SUPER LEAGUE WALA CAF CHAMPIONS LEAGUE, nikawana matapeli tu. Sasa nalipa 24000/- ili wife aangalie HUBA nami LA LIGA tu.
Kwanza Arsenal inavyofungwa hata hamu ya EPL sina
Kwa kweli DSTV imebakia ya wamama kuangalja Huba tu. AZAM inaoneyesha michezo mingi. Na hivi hawaoneshi AFCON wanaendelea kujipoteza.
 
Hata Azam litawakuta jambo sio muda
Decoder zote wanatakiwa kuendana na technology changes,sasa hivi internet inachukua kasi mno wasipoendana na streaming plus kupunguza bei ya visimbuzi watajimbiwa wengi sn,Azam kinachombeba ni local channels
 
Shida hapa kati walipandisha vifurushi.... Alafu ukicheza mtu anapati huduma nzuri tu Azam


Sikujua kuwa GoTV iko chini ya DSTV
Wako pamoja, wote wako chini ya multichoice.. GOtv alikuja kuchukua wateja wasioweza kulipia vifurushi vya bei ghali za DStv kwani ana vifurushi vya bei nafuu lakini pia alikuwa anatumia mfumo wa antenna badala ya dish kama Azam na huduma yake mpya ya ving'amuzi vya antenna..
 
Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado Multichoice ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
Star times ndio analijulia soko la Tanzania na Afrika vizuri
 
Tafuteni pesa mazee acheni kulalama, huwezi kujiliwaza eti kuhama DSTV kwenda Azam, pamoja na changamoto zote zinazosemwa DSTV ni next level. Pesa yako
Dstv kwa wengine sisi sio next level
Teknolojia imeenda mbele sana
Bila Dstv kuna maisha tena zaidi
 
Last week wamenipigia simu wanauliza vipi mbona hutazami runinga? Nikawauliza umejuaje? Wakasema vipimo huku vinaonesha, nikasema kwani lazima nitazame runinga yako hamna zingine? Wakasema basi kama una changamoto tuambie tuzitatue, nikasema huku ninakopata huduma ni mtelezo hamna shida, wakasema kwanini hutazami DSTV? Nikawaambia mmetunyonya vya kutosha nikakata simu
Mfano pia wengine wanatumia canal
Hawawezi kukumbuka Dstv
 
Back
Top Bottom