Fedha zikiingia nyingi ni jambo jema lakini itakua ni kosa kubwa sana kama atawaacha Mbuzi wale fedha za umma kulingana na kamba zao.
Binadamu hawezi kamwe kuridhika na kuwa mwadilifu bila ama kudhibitiwa au yeye Mwenyewe kujidhibiti kutokana na kumwogopa Mungu. Je, Mbuzi tulio nao wanamuogopa Mungu? Je, hawatafuti mapesa Kwa ajili ya zinaa ,ulevi, kujilimbikizia Mali, uhuni Mwingine , kujiandaa na rushwa za uchaguzi n.k. Sasa unawezaje kuwaachia Mbuzi wa aina hii kamba bila kuwadhibiti ikiwezekana kuwatia gerezani Kwa uhujumu uchumi?
Mama alikosea sana akipowapongeza wake wanaotumia vema urefu wa kamba zao kula. Hakupaswa azungumzie kauli Ile inayobariki vitendo vya ubadhirifu na rushwa ndani ya mifumo.
Alipaswa akemee TU vitendo vya rushwa na kuonyesha wazi kukerwa na kuvichukia kuliko kitu chochote. Hata kama ni ndugu wa kuzaliwa kama ni mla rushwa hafai kukalia kiti Cha umma.
January amesemwa sana kuwa sio msafi. Ridhiwani amezungumzwa . Hakuna haja ya kuwabeba kama kweli Wana historia mbaya.
Taifa la Tanzania litapata Heshima na baraka kama tutaonyesha Kwa vitendo kuchukia vitendo viovu kama vile rushwa ,Ushoga, matumizi mabaya ya madaraka,uonevu, uhalifu dhidi ya binadamu, kukwepa Kodi ,madawa ya kulevia, mauaji , ulevi wa kupindukia hasa Kwa viongozi,uzinzi wa kulaghai na ubakaji hasa Kwa viongozi wa umma n.k.
Hatuwezi kujenga Taifa bala kudhibiti Wala rushwa na wanaotumia vibaya Mali za umma na ofisi za umma.Hii nchi haijaumbwa na mtu anayekufa Bali imeumba na Mungu wa milele. Kauli za kula Kwa urefu wa kamba Kwa nchi zenye watu wema wanaohitambia haifai kabisa na inaweza kutumika kujinyonga kisiasa badala ya kuzunguka kula Mali za umma.
Kwa Nini wale Kwa urefu wa kamba wakati Wana mishahara na stahiki zao za kisheria .Hivi kula Kwa urefu wa kamba Kwa Waziri wa maliasili,madini, fedha n.k kinaweza kuwa sawa na Mawaziri kama wa habari na michezo.? Bila shaka mambo hayo ndiyo yanayosababishwa watu wanakwapua Kwa kushindana na kutafuta fursa za kuiba Mali za umma. Ardhi atakulaje kama sio kuuza viwanja viwili viwili au kupima viwanja Kwa viwango vidogo na kuficha idadi sahihi huku viwanja vikikosa maeneo ya wazi na ya michezo Kwa Wakazi. !!
Sijafurahishwa na kauli Ile. Watu wote kuanzia wanye dini za Kumtaja Mungu mwenye haki na mtawala wa vyote tunapaswa kumuomba Mungu atutendee haki Kwa kuwaondoa watawala waovu kwenye nchi aliyoiumba.
Mali za umma zikiliwa basi wanaoweza kusoma albadiri wasome waliozila wavimbe matumbo wapasuke kama mayai viza. Na wasikubalike katika jamii. Wapotee na kumbukumbu zao zisisimuliwe Kwa mema Bali laana na ubaya uwe juu ya vizazi vyao.
Tusikubali kuwaombea wezi na walafi eti Mungu awabariki ,; hapana !! Hawataacha na hawataona ubaya wa kutafuna Mali za umma kwenye nchi maskini kama hii.
Dunia Sasa ni kati ya wema dhidi ya ubaya.
Wakijaribu kula Mali za umma basi watakutana na mkono wa Mungu . Ndio kazi hasa ya albadiri na Sala nyingine za kuwalaani waovu
Wawekezaji waje kufanya biashara ila wasifanye nchi yetu kuwa ni Shamba lao la bibi. Tungewekeza baada ya kukopa hatungepata shida ya kuwakaribisha watu kuja kuwekeza kwenye kilimo wakati wapo Watu wanaiba fedha za umma na kwenda kujenga manyumba makuuuubwa ya kulala tuu watu Wawili mana hata watoto hawana. Tungebana majizi tukawatumia Wafungwa, JKT, vyama vya ushirika vya kisasa vinavyoundwa na wasomi sio wanasiasa waliovalishwa vikofia na kufanya vyama vya ushirika Kwa lengo la kampeni wakati wa uchaguzi. No. Tuunde vyama vywa ushirika Kwa Vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT Kwa kuwapa mashamba waliyotaanzisha wakati wa mafunzo Kwa ajili ya kilimo ,mifugo n.k. sio kwenda kukimbia kwenye matope bila faida ya kiuchumi. Wafungwa wanawekwa magerezani mijini wanalala na kula na kufanya mambo ya kijinga na kufundishana ujinga zaidi na uhalifu zaidi badala ya kupelekwa kwenye maeneo yenye mashamba na ujenzi wajenge barabara za mitaa,walime ,wachimbe mitaro ,wafanye usafi kwenye bustani za Mahospitali na maofisi ya umma.
Afrika Bado hatuoni kuwa tunaweza kujiendeleza bila kuwategemea wakoloni wetu wanaodhani kuwa waliletwa Duniani kuja kututawala na kutunyonya. Hapana. Tunaweza kujitegemea Kwa kuwabana majizi na wahuni wa ndani na kuzalisha Kwa kiwango kikubwa. Hakuna haja ya Kununua juisi na asali Toka Dubai . Eti tunaagiza biscuit Toka China. Ni laana kabisa. Kuna wakati Unaona Bora Putin aamue Moja tu ili tumsubiri Masihi aje aunusuru ulimwengu uliojaa viongozi waovu wanaobebana kutokana na urefu wa kamba zao.
Mbowe sio gaidi ni mfungwa aliyefungwa ili Mbuzi wapate nafasi kubwa zaidi ya kula na hata kukata kamba wale bila kuzuiwa.