Dubai: Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Uwekezaji ya thamani ya Trilioni 17

Dubai: Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Uwekezaji ya thamani ya Trilioni 17

Kwa kutumia tu mfano wa Zimbabwe kuhalalisha wawekezaji inaonyesha ulivyo na upeo mdogo kuhusu maendeleo ya nchi. BTW unaona unavyokinganya mwenyewe kuwa waliondoka na Zimbambwe ikafa? Huoni hii ni sababu ya msingi kabisa ya kuona kuwa nchi inatakiwa ijijenge yenyewe ili isitegemee wageni wanaoweza kuondoka muda wowote?
Zimbwabe hawakuondoka,walifukuzwa.Ni kama Idi Amin,alivyowafukuza wawaekezaji,Mseven akawarudisha.
 
Kwa ujumla Samia anafanya vema katika uwekezaji. Hakuna nchi iliwahi kuendelea bila kuvutia mitaji toka mataifa mengine.

China ilikiwa hohe hahewakati wa Mao na sera zao za kujifungia. Walipoamua kufungua milango kwa wageni kuwekeza China, uchumi wa China ulikua kwa kasi hadi kufikia 12% kwa mwaka. Mpaka leo China ndiyo inayoongoza kwa kuvutia uwekezaji mkubwa toka Ulaya Magharibi na America.

Kipindi cha miaka 6 ya awamu ya 5 ilikuwa miaka ya hasara kubwa kwa Taifa katika nyanja zote. Tunaomba Mungu alilinde Taifa letu isije kutokea hata mara moja tena kupata mtawala katili na primitive, muuaji wa uchumi kama Rais wa awamu ya 5.
Wewe mpumbavu tu,takwimu zipi zilizosema Magufuli aliua uchumi? Kwa mala ya kwanza kipindi cha Magufuri ndio Nchi hii iliingia uchumi wa kati kutoka chini kabisa, Magufuli ndiye alipereka Tanzania kuwa ktk Nchi 10 bora Africa,tena Magufuli kafanya kazi hiyo ktk kipindi kigumu cha corona, Wakati mataifa Mengi uchumi wao uliyumba.Wewe naona baba ya Yako alikuwa fisadi akatumbuliwa na Magufuli ndiomaana ulikuwa na chuki sana nae
 
Mikataba iyo inahusu maeneo ya Kilimo, Madini, Biashara, Utalii na Uzalishaji wa Viwanda
Hili eneo wangeachiwa wananchi na graduates wa SUA na vyuo vingine vya kilimo na wawezeshwe mitaji ili wawaajiri watanzania wenzao badala ya wageni ambao wengi wamelalamikiwa kwa utoaji mishahara duni
 
Hili eneo wangeachiwa wananchi ila wawezeshwe mitaji
Hakuna tija bila competition. Wananchi wanatakiwa kujifunza kupitia ushindani namna ya kulima kwa ubora na kuongeza thamani ya mazao yao kwa ajiri ya kuuza kwa faida na kujiongezea kipato

Hata wakipewa mtaji bila kujifunza kupitia competition hawawezi kuleta mabadiliko!
 
Jamani amkeni amkeni

Huko Dubai mambo ni moto balaa! Leo hii Rais wa JMT Mhe Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mikataba zaidi ya 30 ya uwekezaji Tanzania yenye thamani ya fedha za Tanzania zaidi ya Trilioni 17 na itakayotoa ajira kwa Watanzania za moja kwa moja zaidi ya laki 2.

Mikataba iyo inahusu maeneo ya Kilimo, Madini, Biashara, Utalii na Uzalishaji wa Viwanda

Hongera sana Mhe. Rais kwa jitihada hizi. Mungu akubariki kwa kweli. Haya ndo maendeleo tunayotaka Watanzania

Kutoka Nyasa, ziwani
Lord denning
Mikataba ingekuwa inawekwa wazi ili wenye nchi na kiulipa kodi waione na kutoa mawazo yao kuiboresha
 
Mikataba ingekuwa inawekwa wazi ili wenye nchi na kiulipa kodi waione na kutoa mawazo yao kuiboresha
Bunge ndo wawakilishi wa wananchi! Mikataba ikihitajika itaenda Bungeni
 
Hili eneo wangeachiwa wananchi na graduates wa SUA na vyuo vingine vya kilimo na wawezeshwe mitaji ili wawaajiri watanzania wenzao badala ya wageni ambao wengi wamelalamikiwa kwa utoaji mishahara duni
Biashara akiimiliki mzalendo ndio mshahara utakuwa mkubwa?. Umedanganywa miaka mingi juu ya sera za uzawa mpaka umeona ni kweli.
 
Sawa ila tunaomba utukumbushe ile mikataba ya kikwete na raisi wa china ni upi umetekelezwa maana nasikia ilikua ishirini na zaidina tuakaambiwa itaibadilisha tanzania lakina maisha ndo yanazidi kua magumu.
Mkataba kuibadilisha Tanzania ni matokeo ya juhudi zetu pia. Ukiwa una nia ya kuiba au ya kuhujumu ufanisi wa shirika, usitegemee kuona maendeleo.

Tumejiweka zaidi kisiasa bila ya kuangalia uhalisia wa nchi yetu ilipo na inakusudia kufika wapi.
 
umejiweka zaidi kisiasa bila ya kuangalia uhalisia wa nchi yetu ilipo na inakusudia kufika wapi

KWELI VIONGOZI WETU HAWANA VISION!!! Kweli wanakwenda kukopa huko nje na wanafanikiwa; mfano ni hayo mamillions waliyoleta TADB[ benki ya wakulima] je mama amefanya due diligence ya hiyo taasisi na kuona kama hao aliowakabidhi hayo mabilioni wana INTERGRITY na capacity ya kuweza kumanage hizo fedha mpaka yakapatikana matokeo yanayotarajiwa?
Hapo ndipo tunaposhindwa kutokuwa makini na matumizi ya rasilimali tulizokuwa nazo halafu tunapiga kelele kulalamika. Pale TADB mama anatakiwa afanye due diligence ya kina kuona kama historia na utendaji ya wale waliopo inakidhi matarajio yake!!! Je wameajiri financial analysts wakutosha wenye weledi na sio wa upendeleo? Usije ukajikuta unawapa mchwa gunia la nafaka!!!!
 
Biashara akiimiliki mzalendo ndio mshahara utakuwa mkubwa?. Umedanganywa miaka mingi juu ya sera za uzawa mpaka umeona ni kweli.
Ndiyo maana nikasema wawezeshwe kwamfano kule Mbarali kwenye kilimo cha mpunga, Njombe kilimo cha parachichi na mbao nk
 
Jamani amkeni amkeni

Huko Dubai mambo ni moto balaa! Leo hii Rais wa JMT Mhe Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mikataba zaidi ya 30 ya uwekezaji Tanzania yenye thamani ya fedha za Tanzania zaidi ya Trilioni 17 na itakayotoa ajira kwa Watanzania za moja kwa moja zaidi ya laki 2.

Mikataba iyo inahusu maeneo ya Kilimo, Madini, Biashara, Utalii na Uzalishaji wa Viwanda

Hongera sana Mhe. Rais kwa jitihada hizi. Mungu akubariki kwa kweli. Haya ndo maendeleo tunayotaka Watanzania

Kutoka Nyasa, ziwani
Lord denning
Nchi inauzwa mazuzu yanashangilia
 
Unaonekana una stress sana za maisha! Ondoka kwenye iyo saccos Chadema
Stress ndizo zilizoifanya Urusi kuwa tishio Kwa usalama wa mabwanyenye Wanyonyaji wa nchi za magharibi.

Hujajua kinachoondelea katika ulimwengu wa kiroho.
Sisi wengine tunaipenda sana nchi yetu mana ndio maana tunawachukia sana waovu wanaotumia hila kuiba Mali za umma au kuwabeba waovu wenzao wasio na sifa. Unamhujumu na kumfunga na kuvuruga uchaguzi ili watu kama Mbowe , Heche, Wenje, Msigwa ,Lema na kumpiga Lisu risasi Kisha unatuletea bungeni wabunge wa hovyo wale Kodi yetu Kwa Kupiga makofi Kwa mambo ya hovyo halafu unategemea tushangilie TU Kwa sababu hatuna stress.
Vita inayokuja ni kati ya wema dhidi ya waovu.
Usijifariji kuwa inatumia CCM kukwapua Mali za umma siku zote. Utaaibika siku Moja kufumba na kufumbua utaumia sana kuliko wale uliowaumiza wakiwa na stress.
Kamuulize Sabaya atakuambia kuwa CCM ni Chama TU kama vyama vingine na sio Mungu.

Tulimuelewa Ndugai pamoja na madhaifu yake , nchi isiuzwe. Hatuwezi kuwaruhusu Wageni ngozi nyeupe kuja kuwekeza kwenye ardhi yetu kuja kulima mahindi na maharage na mpunga . Bora tuwaite ndugu zetu wa Kenya kuliko wa Asia na wazungu .
Subiri Iko siku utajua hujui.
 
KWELI VIONGOZI WETU HAWANA VISION!!! Kweli wanakwenda kukopa huko nje na wanafanikiwa; mfano ni hayo mamillions waliyoleta TADB[ benki ya wakulima] je mama amefanya due diligence ya hiyo taasisi na kuona kama hao aliowakabidhi hayo mabilioni wana INTERGRITY na capacity ya kuweza kumanage hizo fecha mpaka yakapatikana matokeo yanayotarajiwa?
Hapo ndipo tunaposhindwa kutokuwa makini na matumizi ya rasilimali tulizokuwa nazo halafu tunapiga kelele kulalamika. Pale TADB mama anatakiwa afanye due diligence ya kina kuona kama historia na utendaji ya wale waliopo inakidhi matarajio yake!!! Je wameajiri financial analysts wakutosha wenye weledi na sio wa upendeleo? Usije ukajikuta unawapa mchwa gunia la nafaka!!!!
Kamba ya mtu ndiyo itakayodetermine kiwango Cha ulaji.
Kosa kubwa sana Kwa kutoa Lugha Ile. Ile Lugha inaibua ushindani mkubwa sana wa kihalifu alimradi ni kamba TU imefanya mtu afikie kilichoko Mbele yake.

Mama anaweza akwa ni Kiongozi Bora sana lakini amezungungukwa na watu wanaotakiwa kusimamiwa Kwa mkono wa Chuma.

Huwezi ukamfunga Mbowe na kuwaacha wezi wanaokwapua Mali za umma kwenye maofisi ya umma Kwa kusingizio Cha urefu wa kamba. Mbowe Hasimamii fungu lolote la maendeleo na Hana mkataba wowote na wawekezaji au manunuzi hivyo kuendelea kupoteza muda wa kupambana na wapinzani kama Mbowe ni kuwapa muda na nafasi nzuri mchwa na panya na Mbuzi wanaokwapua na kutafuna keki ya Taifa. Wanashindana kupanga ujanja wa Kupiga dili.
Karne hii yenye teknolojia na vifaa vya kisasa haiwezekani Daraja lijengwe kila mwaka linabebwa na maji utadhani limejengwa na matope .

Barabara inajengwe Kwa kiwango Cha Changarawe na kila mwaka wakati wa mvua za masika Eneo la km 3 linabaki makorongo na matope na magari yanashindwa kupitia. Km 3 zinawekwa matope kila mwaka na wazabuni wanafanya ni Eneo lao la urefu wa kamba za apigaji wa Halmashauri na Sasa TARURA. Hakuna anayejali kuweka Lami hizo km 15 au hata kuzijenga Kwa mawe na Sementi ili kuondokana na bajenti ya kila mwaka kuweka udongo barabarani na kuezuliwa na mvua. Unakua ni mzunguko wa Kupiga pesa za Umma. Hakuna anayejali mana ni urefu wa kamba yake na kila mmoja anaangalia kamba yake ifike mbali zaidi.
 
Back
Top Bottom