Dubai: Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Uwekezaji ya thamani ya Trilioni 17

Dubai: Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Uwekezaji ya thamani ya Trilioni 17

Nchi gani duniani imeendelea bila foreign investors?
Nchi zote zilizoendelea. Halafu wewe unataka ku-mislead mjadala huu kwa kuingiza mambo ambayo sikusema. Nisikilize tena: Nimesema wawekezaji wa kigeni wanatakiwa, lakini siyo kwa njia anazotumia rais wetu za kuzunguka kila sehemu akibembeleza na kupiga magoti. Kuwe na utaratibu wa kuwapokea. Huwezi kukurupuka na kusema bila wawekezaji nchi haiwezi kuendelea na unapiga vigelele kila unapoingia mkataba kama ninyi mnavyofanya. Wawekezaji wanakuja kwa faida zao na wanaweka maslahi yao mbele. Msiwe na mawazo kama ya waswahili wa Pwani.
 
Hiyo mikataba ya kusainiwa kwenye Expo imejadiliwa kwa undani kweli? Au ndiyo mwendo wa enzi za upigaji za fisadi Kikwete watu wanasaini mikataba kwenye restaurant?
Ni mikataba gani ya kipigaji ambayo Kikwette aliingia? Au mumebakia kukaririshwa propaganda za Mwendazake?

Yeye aliamua kudhalilisha kazi za watangulizi wake kuwa zilikuwa za kifisadi. Ila ilikuwa ni uwongo tu. On the contrary yeye akaishia kupatikana na Audit Query ya Tshs 2.4 Trillion
 
Jamani amkeni amkeni
Huko dubai mambo ni moto balaa! Leo hii Rais wa JMT Mhe Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mikataba zaidi ya 30 ya uwekezaji Tanzania yenye thamani ya fedha za Tanzania zaidi ya Trilioni 17 na itakayotoa ajira kwa Watanzania za moja kwa moja zaidi ya laki 2.

Mikataba iyo inahusu maeneo ya Kilimo, Madini, Biashara, Utalii na Uzalishaji wa Viwanda

Hongera sana Mhe. Rais kwa jitihada hizi. Mungu akubariki kwa kweli. Haya ndo maendeleo tunayotaka Watanzania

Kutoka Nyasa, ziwani
Lord denning


Watanzania wengi tuna tabia ya kupotosha sana. Memorandum of understanding sio mkataba wa uwekezaji bali ni mkataba wa kuongea zaidi kuhusu jambo fulani kwenye hili ni uwekezaji. Uwekezaji unaweza ukawa zaidi ya hapo au usiwepo kabisa. Hii ni tofauti na mkataba wa uwekezaji ambao kila kitu kiko tayari
 
Kwa kutumia tu mfano wa Zimbabwe kuhalalisha wawekezaji inaonyesha ulivyo na upeo mdogo kuhusu maendeleo ya nchi. BTW unaona unavyokinganya mwenyewe kuwa waliondoka na Zimbambwe ikafa? Huoni hii ni sababu ya msingi kabisa ya kuona kuwa nchi inatakiwa ijijenge yenyewe ili isitegemee wageni wanaoweza kuondoka muda wowote?
Nchi gani ya kiafrika ambayo imeendelea kutegemea wawekezaji wa ndani ambao sio wazungu au ngozi nyeupe ya nje? Afrika kusini iko juu sababu ya wazungu nipe mfano mmoja tu wa nchi yeyote ya kiafrika ambayo uchumi uko juu kwa kutegemea ngozi nyeusi

Tanzania uchumi wetu wa ndani unategemea ngozi nyeupe wahindi,waarabu na wapemba ndio big taxpayers

Exports tunategemea soko la wazungu sio la nchi za waafrika wenzetu ngozi nyeusi

Mama Samia yuko vizuri
 
Nyota ya Rais wetu inang'aaaaaaaaaa sanaaaaaaaaa.
Mungu amlinde na maadui na wasio mtakia mema, wenye wivu na roho mbaya ya kishetani.
 
Hajui wala hana uwezo wa kujua mikataba kama hiyo. Hawa ni wapumbavu wanaopiga kelele kwenye level za chini ili mradi mkono uende kinywani.
Wapumbavu ndio wanaoamini kila kilichosaini hakina makosa. Huku Afrika ikididimia kwa ukosefu wa uzalendo na uaminifu kwa mali za umma. Wapumbavu wengi wanaishia kupewa kofia, viberiti na kushangilia

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Nchi gani ya kiafrika ambayo imeendelea kutegemea wawekezaji wa ndani ambao sio wazungu au ngozi nyeupe ya nje? Afrika kusini iko juu sababu ya wazungu nipe mfano mmoja tu wa nchi yeyote ya kiafrika ambayo uchumi uko juu kwa kutegemea ngozi nyeusi

Tanzania uchumi wetu wa ndani unategemea ngozi nyeupe wahindi,waarabu na wapemba ndio big taxpayers

Exports tunategemea soko la wazungu sio la nchi za waafrika wenzetu ngozi nyeusi

Mama Samia yuko vizuri
Aiseee

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kwa ujumla Samia anafanya vema katika uwekezaji. Hakuna nchi iliwahi kuendelea bila kuvutia mitaji toka mataifa mengine.

China ilikiwa hohe hahewakati wa Mao na sera zao za kujifungia. Walipoamua kufungua milango kwa wageni kuwekeza China, uchumi wa China ulikua kwa kasi hadi kufikia 12% kwa mwaka. Mpaka leo China ndiyo inayoongoza kwa kuvutia uwekezaji mkubwa toka Ulaya Magharibi na America.

Kipindi cha miaka 6 ya awamu ya 5 ilikuwa miaka ya hasara kubwa kwa Taifa katika nyanja zote. Tunaomba Mungu alilinde Taifa letu isije kutokea hata mara moja tena kupata mtawala katili na primitive, muuaji wa uchumi kama Rais wa awamu ya 5.
 
Fungua nchi Mama Samia. Nchi inahitaji mitaji toka nje ili izalishe ajira. Cha msingi ni kukwepa mikataba ya kitapeli na kifisadi.
Namwunga mkono sana Rais Samia katika mtazamo wake wa kujenga uchumi. Kitu pekee anachonikwaza kwa kiasi kikubwa ni kumbambikia kesi Mbowe na Makomandoo. Hilo linaua mazuri yake yote, maana ukiwa kiongozi hata ufanye mazuri gani kama unadhulumu watu haki zao, wewe unakuwa ni uzao wa shetani.
 
dah sijui kama tutaitekeleza hiyo mikataba, Maana Putin tayari ameshawasha Manyuklia yake huko anasubiri kupress button tu dunia iimbiwe parapanda..
 
Hata JK alisaini na rais wa China mikataba mingi lakini mpaka leo hakuna utekelezaji
Kanyaboya/ boshen tupu
Afadhali hao Wachina hawakuja. Hakuna watu wa hovyo katika uwekezaji kama Wachina. Wachina ni waganga njaa, siyo wawekezaji.
 
Hiyo pesa ni nyingi Sana..mikataba gani hiyo....na uwekezajo gan huo..the only problem with her is that she never think beyond the next meal.
 
dah sijui kama tutaitekeleza hiyo mikataba, Maana Putin tayari ameshawasha Manyuklia yake huko anasubiri kupress button tu dunia iimbiwe parapanda..
Hivi wachawi wako wapi!?? Kwanini wasimpige Putin Radi tu
 
Back
Top Bottom