Dubai tumesaini nao mikataba ya maendeleo zaidi ya 30. Watanzania wanaopenda Maendeleo tumieni fursa alizotuletea Rais Samia

Wapo wajinga kwenye jamii yoyote cha muhimu ni kuachana nao. Kazi yao huwa ni kulalamika na kulialia umaskini hata pale fursa zinapoletwa miguuni mwao.
 
Mnatumia nguvu kubwa kuwauzia waarabu mali asili zenu... Ukishindwa wewe kuendesha jambo fulani liache atakayekuja atalimudu... What if watangulizi wangeamua kuuza mali za Tz kwasabab hawakuwa na uwezo wa kuziendesha..?
Mnatumia nguvu kubwa kujaribu kumchafua Rais wetu lakini wenye akili timamu wanaelewa anafanya nini kwa malengo gani.

Nyinyi mlioamua kuwa na akili negative bakini nazo tu hakuna wa kuwazuia.
 
Eeeeh na wewe kujifanya CCM kunoga.
 
Hakuna anayepinga kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya serikali ya JMT na ile ya Dubai. Bali kuna maeneo yenye mguso wa kisheria ndani ya IGA yana ukakasi. Hakuna anayepinga kuhusu uwekezaji huu wa DP World. Bali kuna maeneo yenye kulalamikiwa, ambayo kabla ya kujifunga katika sheria za kimataifa yanapaswa kuwekwa sawa. Huwezi kwenda katika HGA hali kukiwa na utata kuhusu ukomo wa mkataba, eneo la kimamlaka la mwekazaji, na suala zima la usalama wa nchi yetu.
 
Mbona hujaitaja hiyo mikataba au MOU kwamba ni nini na nini kinahusika?
 
Na amejtahidi kuuweka uwazi lakini hofu tu ya baadhi ya watu muhimu kuboresha vipengele vyenye utata.
Kuna watu walikuwa na hofu kama hii wakati hayati Mkapa alivyoleta FDI za SA lakini nyingi zinafanya vizuri mpaka leo
Taja moja
 
Vile Visiwa ni Vya RA meli zake ndio zinapeperusha Bendera huko Duniani!
Sivijuwi.


Natamani huu mkataba ubadilihwe. Vifungu vyote vya sheria, Mpewe nyie. Muuandike upya mwnazo mpaka mwisho, halafu mama awapeleke DP World wakajenge gateway port Zanzibar kama walivyofanya London gateway port.
. Ndani ya mwaka mmoja kitu tayari, bandari ya Dar ibaki kuokea mizigo kutoka Zanzibar tu.

Unafikiri meli ipi ya nje itakuja hapa ikiwekwa DP World Zanzibar gateway port? Ambayo meli ikifika tu tu ndani ya masaa mawili matatu mzigo umeshshashushwa. Unawangoja mapoyoyo mkau chukuwe. Zanzibar kiulaini watakuka hela zao za kuegesha makontena yenu tu.

Mama ni mwema sana hakufanya hayo. Lakini, lisemwalo lipo.
 
Nipe connection na Mbarawa basi nipige fedha za maana. Niko tayari Kuslimu. Niletee na ile kofia pendwa
 
Wewe unatumia ngapi? Na zinahusu nini? Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
 
Zanzibar imeelemewa na Raia ukiiomgezea majukumu Visiwa vitazama ndio sababu Waunguja Wenye akili akina Hamad Rashid wamejiapiza kamwe Muungano hauvunjwi!

Kanisa Moja Takatifu la Mitume
 
Nipe connection na Mbarawa basi nipige fedha za maana. Niko tayari Kuslimu. Niletee na ile kofia pendwa
Mbarawa hana connection za biashara, wewe lucifer watu hawasilimu kwa pesa, huo ni ujinga.


Uliza kiheshima tukuelekeze ende wapi, ukamuone nani. Useme sasa hivi unafanya biashara gani, kama huna cha kufanya sema huna kazi tukuelekeze wapi pa kwenda.


Tafadhali asitume mtu pm huwa sijibu.


Unataka kuuliza uliza hapa hapa jukwaa la wazi wengi wafaidike. Mwenye kisu kikali ndiye mla nyama.
 
Fursa tunazo waTanzania wenyewe.
Hakuna mtu mwingine yeyote toka nje atakayetuletea maendeleo hapa.

Huku ni kukosa akili kichwani.
 
Zanzibar imeelemewa na Raia ukiiomgezea majukumu Visiwa vitazama ndio sababu Waunguja Wenye akili akina Hamad Rashid wamejiapiza kamwe Muungano hauvunjwi!

Kanisa Moja Takatifu la Mitume
Hakuna anaongelea kuvunjwa muungano. Zanzibar ina nafasi kubwa sana haikuelemewa wala hata kukunwa bado. Tazama Singapore, kijikisiwa kidogo tu na bafo kinakuwa mpaka leo.


Mimi ni Mtanganyika, siyo Mzanzibari lakini nakwambia uungano ukivunjika hasara kwa Tanganyika. Kumbuka hilo.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…