Dubai tumesaini nao mikataba ya maendeleo zaidi ya 30. Watanzania wanaopenda Maendeleo tumieni fursa alizotuletea Rais Samia

Maswali ya ajabu sana haya!
Sasa kma hicho kiwanda hukioni ndiyo tuache kujihangaisha kukitafuta?

Nenda kawaulize hao hao akina Samia na wote walioongoza nchi hii ukimwondoa kwenye orodha hiyo Mwalimu Nyerere, kwa sababu yeye tunajua juhudi alizofanya viwanda hivyo viwepo, na vilianzishwa.

Ninajua utakuja na swali,sasa viko wapi? Nitakuachia wewe swali hilo kwa sasa kama unataka kuhangaisha kichwa chako, bila ya kuingiza siasa mbovu au hayo mambo mengine ya "ulevi" unayofahamika kuwa nayo; na ndiyo yanayokusumbua sana na mihangaiko hii ya sasa.

Ukipenda kuyaweka hayo yote pembeni, tukajadili maswala ya maendeleo ya waTanzania, tutafanya hivyo kwa nia safi kabisa.

Kama hakuna "kiwanda cha sindano" Tanzania sasa hivi, hiyo haiwezi kamwe kuwa sababu ya sisi ku'aspire' kuwa na kiwanda hicho milele, eti tu kwa vile tutatafuta mtu wa kuja kukijenga kiwanda hicho; hata kama ni kwa masharti yasiyokuwa rafiki kwetu.

Ngoja nimalize kwa kukuliza swali: Hivi wewe unaona waTanzania tunakosa kitu gani hasa cha kuweza kujenga na kukiendesha kiwanda cha namna hiyo uliyoeleza wewe, kwa muda wote huu, miaka zaidi ya 60 toka tupate uhuru?

Na unategemea hicho kiwanda tutakuwa na uwezo wa kukipata na kukiendesha kwa ufanisi lini, baada ya miaka 60 mingine inayofuata?

Kwa nini tusiweke juhudi zetu zote sasa hivi, hata kwa msaada wa hao wageni wanaokuja kuwekeza hapa, tujijengee uwezo wa kuyafanya mambo kama haya sisi, tunapopungukiwa tuwaite waje kutuunga mkono kwa juhudi zetu?

Samahani, nilitaka kuuliza swali moja, lakini yakawa yanaongezeka, na bado yapo mengi tu.

Kama kuna makosa ya uandishi, fahamu nilitiririka tu, sikuwa na muda wa kurudi nyuma kufanya masahihisho.

Mashir
 
Swali moja tu, siyo maswali. Lakini tazama lilivyo kutowa povu kujibu.


Sasa jibu, kipo au hakuna?
 
Kulipoibuka tu sakata la Bandari na wewe ukaibuka, Je, wewe ndo wale mliopanda bombadia na kuwa mmoja wao waliopokea 6 M?
Huyu ni Hezbollah, mdini na yupo wazi na zaidi yupo kimkakati kutetea ujinga unafanywa kisa tu ni dini

Yupo active na muanzisha THREADS mfululizo kuhusu DP WORLD
 
Swali moja tu, siyo maswali. Lakini tazama lilivyo kutowa povu kujibu.


Sasa jibu, kipo au hakuna?
Naona unataka tuzungushane tena, na ukitaka hivyo, nipo vizuri tu, tutakwenda kwa pamoja.

Tumia akili. Soma yaliyoandikwa na jiongeze.
 
Kwa nini wews mtanzania unatetea maslai ya Dubai na sio maslai ya nchi yako Tanzania?

Kama mtanzania unashindwa kuona firsa za kiboashara za Bandari zetu utaona fursa za kibiashara za Dubai🤣
 
Huu "ulevi" mimi sina muda nao kabisa.

Ukitaka tulewe pamoja, lete ile kitu inaitwa "Tanzaniaa', Basi.
Tena iponkwenyensura inayoitwa hivyo hivyo. Jina kubwa hilo, jisomee uufurahishe moyo wako👇🏾

 
Kati ya hao wote, hakuna hata mmoja aliyekwenda kuuza kipande cha nchi hii, kama anavyofanya huyo mama.
Propaganda zisizotumia akili hizi.
Nineryniwa hiibkwa whatsapo, ni jibu tosha kwako 👇🏾

kama WALISEMA MKAPA ANAUZA NCHI KWA MAKABURU HII INAYOUZWA KWA MWARABU NI IPI?

Sisiwengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?
The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
 
Haujambo mrembo...🙋‍♂️
 
Niamini.
Sitanii, huo ulevi mimi sina kabisa; kwa hiyo ni kazi bure kunihimiza jambo ambalo halinichukulii muda kabisa.
Kazi kwako, nilitaka kukyfahamisha jina lako hilo zaidi ya miaka 1400 limetajwa kwenye Qur'an. Hakika Qur'an ni muuijiza.


Kama hutaki sikulazimishi, kuwa na amani
 
AlhamduliLlah sijambo.


Unajuwa kuwa mama Samia alisaini mikataba 36 ya kuwaletea fursa Watanzania?
He...kumbe..🙊
Basi utanisimulia vizuri nikirudi nyumbani toka safarini kipenzi
 
He...kumbe..🙊
Basi utanisimulia vizuri nikirudi nyumbani toka safarini kipenzi
Unajuwa kuchamba? Jibu hili swali 👇🏾

Your browser is not able to display this video.
 
TRA hawafanyi vizuri tunapoteza makusanyo mengi sana na wezi wamezidi TUWAITE WAWEKEZAJI, TANESCO toka imetengenezwa hasara hasara WAWEKEZAJI Waje hapa,Vyuo vyetu graduates siwaelewi hata kujieleza binafsi tatizo TUWAITE WAWEKEZAJI Tunachelewa sana, TANAPA na Wizara ya Utalii na maliasili hapa hata kagame anashangaa Rwanda kuizidi Tanzania Mapato ya Utalii TUWAITE WAWEKEZAJI, Mamlaka za Maji waziri anafukuza tu wakurugenzi TUWAITE WAWEKEZAJI tumechelewa, Vipi majeshi yetu yanatija kweli tunaachwa nyuma sana ona wenzetu walipo TUWAITE WAWEKEZAJI. WAWEKEZAJI njooni
 


Hatutaki kelele!
 

Attachments

  • 69480.jpg
    14.9 KB · Views: 2
Sijasoma andiko hilo refu uliloweka hapo, ila ninachokiona ni kuwa hutaki kuelewa ninachokieleza mimi, au unajifanya tu huelewi.

SAWA. Hata kama uwekezaji huo wote ulifanyika na kuleta manufaa Tanzania, hiyo ndiyo iwe sababu ya sisi kutojibidisha, tubadilike, nasi tufanye mambo yetu kwa ufanisi?
Hapa ndipo ninaposhindwa kukuelewa kwa nini hutaki kuliona hilo.

Ni dharau isiyokuwa na kifani, kuhitimisha kwamba Tanzania hakuna lolote tunaloweza kulifanya sisi wenyewe.
Ninamdharau yeyote mwenye mawazo ya kipumbavu namna hiyo.

Kwa mtu kama wewe, uliyeoshwa akili na kuwa nyeupe kabisa, akili isiyotaka kufikiri vingine mbali ya hizo nyimbo mnazoimbishwa huko mashuleni; hata akili ya kujua tatizo la hayo yote unayodhani waTanzania hawayawezi yanaanzia wapi, na hawa viongozi aina ya huyiu Samia ndio wamekuwa nyenzo za kueneza ujinga huu.

Badala ya kujishughulisha na kunyoosha na kuondoa uozo huo unaozuia ufanisi wa kazi za waTanzania, hawa viongozi ndio wanakuwa waenezi wa kuwakatisha tamaa wananchi wao?

Kama hujui tatizo ni nini (viongozi), siku zote utaendelea kuwalaumu waTanzania bure.
Makosa yapo kwa hao viongozi wanaoshindwa kuhakikisha kuwa juhudi za waTanzania hazihujumiwi.
In fact, ni hao hao wanaowahusudu ndio wanaohusika na hujuma kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…