Dudu Baya: Kinachofanya Tanzania itulie tofauti na jirani zetu ni kuwa sisi tumenyimwa elimu ya haki zetu. Wenzetu wanayo

Wenye kujuwa kuhoji wamepata nini sisi hatuna, sana sana wamezika watu kwa ujinga tu mwisho wa siku serikali ni ile ile maisha ni yale yale ni wamepata. Ndio maana ziko chaguzi ni wakati wa kuchagua unayemtaka ukishindwa basi heshimu majority.
Taifa lao lina uchumi imara kuliko sisi usisahau serikali yao inawajibika kwa wananchi kuliko yetu usisahau wako far better kwenye kila kitu kuliko sisi no wonder ukiruhusu soko huria la ajira uwe na uhakika sie tutaambulia asilimia 15 tu.
Taifa letu limezalisha watu waoga wasio washindani hivyo hata takwimu za watanzania walioko nje ya nchi tunazonufaikao nao ni wachache sana kuliko wenzetu.
Ukilitazama hili kwa jicho la leo huwezi ona athari zake but ukitazama kwa mapana tunaathirika!!
 
Nadhani hujui history ya nchi yetu, Tanzania sio kwamba wametuzidi kwa bahati mbaya sisi tulijikwaa tulipoingia katika ujamaa na kujitegemea wakati wao walibaki katika misingi ya capitalism sisi kuja kurudi kwenye mifumo ya soko huria miaka ya 85 wao walikuwa mbali, sasa fanya hesabu zako baada ya sisi kuachana na ujamaa Kenya walikuwa wapi na sisi tulikuwa wapi na leo hii wako wapi na tuko wapi kama Gap liko close ina maana tunafanya vizuri.

Mtu aliyeanza kukimbia kabla yako halafu wewe unamfuata nyuma lakini kila siku unamsogelea basi unafanya vizuri. Maamuzi yaliyofanywa miaka hiyo na viongozi wetu yalitufanya turudi nyuma na mbaya tukaingia vita na Uganda. Sasa ngoka nikujibu kwanini sio waoga, hivi umewahi kujiuliza kwanini waarabu sio waoga? kwa sababu miaka hiyo mazingira waliyoishi kwenye jangwa maisha yalikuwa magumu sana ikajenga na mioyo yao kuwa migumu sana mpaka leo na ndio wa Kenya, hawa jirani zetu wana ardhi mbaya sana na nzuri iko chini ya wachache kina Kenyatta na Odinga wananchi wa kawaida hawana hii imewafanya mioyo migumu. Kenya hufanyi kazi huli chakula bongo unakula tu hata kwa jirani.
 
Kweli kabisa !
 
Mahakama zipo pia kumbuka unaweza kuwa wewe hujawachagua ila kuna watu wamewachagua kwa hiyo wana mandate ya kuongoza. unashida mahakama zipo sio kuleta fujo barabarani kuna watu wako busy kutafuta pesa.
Sawa nini dhumuni la mahakama? Kama muhimili wa kusimamia haki haufanyi kazi kwa usahihi maana yake ni kwamba unatengeneza mianya ya watu kubuni njia mbadala ya kudai haki zao.

Hapo ndipo watu wanafikia kwenye ku exercise haki ya kikatiba ya maandamano ambayo in turn huwa yanapachikwa majina yasiofaa ili tu kupora hio haki. Watu wameitwa "Magaidi", "Wahaini", "Wahuni" na "Waleta taharuki" katika namna ya kudhoofisha tu haki ya msingi. Ila cha ajabu zaidi kuna double standards katika hilo kwa maana kuna kundi likiandamana wao huwa hawaguswi ila kuna kundi likiandamana ni vipigo na kuswagwa.

Hali hii linasikitisha sana katika taifa ambalo tunajipambanua tuna amani na kutaka amani idumishwe ikiwa kuna dhuluma ya haki.
 
Hoja sio kuingia barabarani pekee hoja ni kutambua haki ya raia. Alichoongea ni kwamba watanzania uwezo wa kutambua haki zao upo chini.
Wengi wetu huishia kuonewa na kupotezea
Mbongo mtu wa kushukuru kwa kila jambo😂 ila ni upumbavu kuwa hivyo. Uwezo wa kutambua haki upo ila uwezo wa kudai haki ndio hafifu sababu huwa wengi sio wafauatiliaji.
 
Hapa unaongelea kama Kenya imekuwa USA hivi, nimekuulizia je wa Kenya wana maisha bora kuliko sisi? jibu rahisi tu. Nakwambia maisha yetu ni rahisi kuishi Tanzania ni rahisi, Kenya unaweza kulala njaa lakini sio Tz. Critical thinking yao wamefika wapi? wa Kenya wanakuja kufanya kazi kwetu sisi tupo kwetu tunakula maisha tu.
 
Unajuwa kwanini wa Mexico wana cross kuingia USA? sababu USA uchumi na mishahara mikubwa kuliko Mexico, sasa hao wa Kenya wako wangekuwa bora basi ungeona foleni misururu ya waru wakiingia Kenya lakini kwa kuwa Tz ni bora wao ndio wanakuja huku kufanya kazi. Kenya maisha magumu ndio wanabidi wafikirie ziada ku survive.
 
Wahenga walisemaga Amani ni tunda la Haki !
🙌🙏🙏 Ni muhimu Haki iwepo pande zote !
 
Kwa hiyo wewe unataka umuachie peke yake halafu wewe ujifungie ndani uwe unachungulia kwa mbali sasa huo si ndio uoga na ukosefu wa kujua haki ambao unaongelewa hapa kwenye huu uzi.
Mbona Kenya linapotokea jambo lolote watu hawaulizani maswali magumu kama unayouliza wewe hapa ila wote wanatoka kwa mara moja kwenda kusaidiana,kuulizana maswali magumu ni dalili ya uoga na kujipa excuse kwenye mambo ya kimaendeleo.
 
Huyu nae dudu baya mpumbavu mbona enz za jiwe hakua akiyazungumza haya kaongea ukweli ika mtu mnafiki hua simkubali dudu ana jnafiki wa kinge*** sana enzi za jiwe sikuwah nsikia akitoa hizi kauki
Wewe inaelekea hujaelewa kabisa hii mada.
Hii mada haiongelei kuhusu uongozi wa awamu ya 5 au 6.
Hii mada inahusu Watanzania kwa ujumla kuhusu kutojua haki zao haijalishi ni katika awamu gani ya utawala.
 
Na kingine ni uoga na ubinafsi, utasikia mtu anasema mimi nife halafu waje kula wengine! Utafikiri kwenye kundi la walaji wa sasa na yeye yumo!
Yaani yuko tayari kula ugali dagaa na maharage kila siku lakini si kujitolea kwa ajili ya watu wengine😀
 
Mahakama zipo pia kumbuka unaweza kuwa wewe hujawachagua ila kuna watu wamewachagua kwa hiyo wana mandate ya kuongoza. unashida mahakama zipo sio kuleta fujo barabarani kuna watu wako busy kutafuta pesa.
Na kama Mahakama hazifanyi kazi yake ipasavyo yaani inasikiliza upande mmoja kwa upendeleo utafanyaje?
 
Tumbo tupu halina kitu ila bado ana uwezo wa kushabikia simba au yanga kwa nguvu zote. Badala ya kutafuta kiini cha njaa yake. Wanasiasa ndio wanaosababisha hali ngumu ya maisha na tunacheka nao tu. Hatujui haki yetu.
 
Sasa wewe unataka mimi nitoke barabarani kuiga watu au kufuata ngama ngoma ya mdundiko hujui inaenda wapi. Hizo haki unazoongelea hapa haki gani hizo? Mimi sina shida yoyoye napata nachotaka kisheria labda ondoa sentence za kijumla haki zetu uwe specific haki gani? Ya Kenya mimi hayanihusu sio kwetu kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…