Hata kama Ruge angekuwa hakosei hilo bado kuna mengine mengi ambayo angekuwa anakosea tu yeye kama mwanadamu. Unamaanisha wote aliowakosea walitakiwa watafute vyombo vya habari kutangaza waliyokosewa na Ruge baada ya kufa??
Ishu hapa sio usahihi au kutokuwa sahihi kwa alichokisema Dudubaya, ila ni kitendo cha kutumia media kutangaza mambo yaliyomuumiza yeye binafsi kwa jamii nzima baada ya mhusika kufariki. Huu sio ubinadamu. Na nawashangaa ambao bado wanasapoti huu upuuzi.
Lakini pia kuna jambo lingine hatujaliangalia:
Kuna kitu kinaitwa Law of natural justice. Mtu hachukuliwi kama mwenye kosa bila kupewa nafasi ya kujitetea au kujibu tuhuma. Kipindi chote cha uhai wa Ruge hakuwahi kufungua mdomo kuwajibu waliokuwa wanamtuhumu mabaya. Huenda ni kwa jinsi alivyoumbwa maana ma genius huwa hawanaga kawaida ya kuongea ongea. Ila huenda kama Ruge angeamua kufungua mdomo kujibu huwezi jua nini kingetoka kinywani mwake; huenda angetuonesha upande wa pili wa watoa tuhuma wana makosa gani pia na kukufanya uwaone wao ndo hawafai! Ila kwa kuwa hakuwahi kusema na bahati mbaya hawezi tena kusema kwa kuwa amefariki basi si busara kuendelea kumtuhumu maana hana tena nafasi ya kupata haki yake ya 'natural justice'
Mwisho mkumbuke Ruge hakudeal na muziki tu. Vipi kuhusu maisha ya watoto 150 aliosaidia kupatikana hela ya upasuaji wa mioyo yao?? Vipi kuhusu wahanga wa mafuriko huko Kilosa aliookoa maisha yao?? Vipi kuhusu bodaboda aliowafungulia SACCOSS na kuwawekea milioni 60?? Vipi kuhusu mamalkia wa nguvu?? Vipi kuhusu vijana aliowasaidia kupitia FURSA, Vipi kuhusu...................the list is so long!
Yaani umsikilize na kuungana na Dudubaya na wenzake ambao hujajua hata wao walikosea wapi kumsema mabaya Ruge usahau haya mazuri kibao aliyoyafanya Ruge?? Ukijichunguza vizuri utagundua kuna mahali unakosea sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app