Haifai Rais kuchukua nafasi ya Hakimu au Jaji kugawa haki, huna uhakika suala la huyo bibi yako lilikwisha kwa sababu haki ilikuwa upande wake au watu walitimiza tu matakwa ya Rais bila kuangalia haki iko wapi.
Huo Mfumo wa Kangaroo courts ni dalili ya mhimili dhaifu sana wa mahakama.
Wewe acha hizo Rais hatoi uamuzi, ujasoma mambo ya uongozi nini? Kinachofanyika ni Rais kusaidia huyo mama kusikilizwa kwa haki. Yaani humu kuna mtu anaweza andika jambo mpaka unajiuliza hivi watu wanaufahamu kweli? Au wamekalia ushabiki? Asilimia kubwa ya Jamiiforums watu wamekaa kichawa. Hawachanganui mambo kwa hoja na kuangalia dunia inavyokwenda.
Pengine wengi hawajui mifumo ya utendaji kazi katika kiserikali. Na pia kama wanajua wapo kiushabiki au kichawa zaidi. Kwa taarifa yako, wananchi wengi wanaonewa. Na wengi wanapoteza haki zao. Nimeshuhudia haya. Na siongoi tu najua.
Mfano mfupi, kuna mzee mmoja ni kipofu au asiyeona. Alizurumiwa nyumba yake iliyokuwa eneo zuri sana na tajiri mmoja mkubwa. Huyu mzee alikuwa anaumwa wakajua atakufa. Hakuwa na watoto. Majirani ndo walimsaidia. Hivyo akasainishwa mkataba kwa kuweka dole gumba wakati akiwa mahututi.
Kaja kuzinduka baada ya miezi, anaambia alilidhia nyumba kuuzwa. na bei ya nyumba ati imeuzwa kwa millioni 5 tu. Akashangaa! Kesi kwenda mbele yule mzee alishindwa huyu tajiri alikuwa anaonga fedha nyingi. Eneo ni nzuri la beach. Hakimu alikuwa anakula rushwa saana. Akidai hawezi ingiliwa. Suala lile lilikatiwa rufaa.
Huyu tajiri alozurumu akapiga simu akitaka kutoa milioni mia moja hili anaefuatilia hili suala na kumsaidia huyu mzee aache.
Bahati mbaya huyu mbwana alikwenda masomoni.
Kilichotokea huko nyuma mzee alibambikwa kesi, akaenda jela, huyu jamaa akachukua nyumba akavunja na kujenga mjumba wa kifahari. Na maeneo hayo kuna Port ndogo. kesi ikamalizwa ki namna.
Ni mengi tu. Katika moja ya utafiti wangu wakati nafanya shahada ya uzamili nilipendekeza serikali kuanzisha chombo maalum cha kusikiliza malalamiko. Kenya walianzisha nadhani miaka michache ilopita.
Tanzania hii watu wananyang'anywa maeneo, wanateswa, wanaingizwa ktk chumba inachomwa pilipili, wanateswa, maeneo yao na mifugo vinachukuliwa. Na huu ni mtandao mkubwa. Kuna viongozi wakubwa wanahusika. Basi tu mtu kama huko mjini unadhani mambo ni mazuri.