Duh, walokole mnatuchosha - mnatuboa na mada zenu!

Dini za mapokeo zinawapagawisha kiasi cha kuwashangaza hata hao waliowaletea dini zenyewe
 
Dini za mapokeo zinawapagawisha kiasi cha kuwashangaza hata hao waliowaletea dini zenyewe
Kama walioacha uzinzi, umalaya, ufisadi, ujambazi, rushwa, uuaji, matusi, ulaghai, uonevu, baada ya kumwamini Yesu, wamepagawishwa; je, wanaofanya matendo hayo maovu tuwaiteje?
Ungetafakari kwanza hilo, usingewabeza wanaomcha Mungu na kutenda yaliyo safi na ya haki.
 
My dear Demi , nani aende kwenye mipombe na harufu zake, mimi?
Hahaa. I was set free from the bondage of alcohol a long time ago!
Nipo kwenye biashara ya pombe kwa miaka 7 sasa.
Nataka kusema hivi BIASHARA YA POMBE INALIPA HASAAA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kelele ni kelele tu, zitoke bar au kanisani au msikitini au kwenye sherehe ni kelele.
 
Kelele ni kelele tu, zitoke bar au kanisani au msikitini au kwenye sherehe ni kelele.
Zaburi 98:4 (NENO)
Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda
 
Zaburi 98:4 (NENO)
Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda
Sasa mbona kelele zinaenda kwa majirani badala ya Mwenyezi MUNGU?
 
Kama huna hela tulia usiwapangie maisha watu kila mtu atakufa kivyake,, masikini mnasumbuwa sana
 
Kama huna hela tulia usiwapangie maisha watu kila mtu atakufa kivyake,, masikini mnasumbuwa sana
Kama hujaokoka, tulia, usiwapangie walokole cha kusema. Walokole wanafanya kazi kubwa ya kuwajulisha watu jinsi ya kuepuka kifo cha milele.
 
Sasa mbona kelele zinaenda kwa majirani badala ya Mwenyezi MUNGU?
Nakumbuka kuna Mkuu fulani alilalamikiwa na wananchi kwamba walokole katika Kanisa fulani wanawapigia kelele majirani. Mkuu huyo aliwajibu kwa hekima: "Wanaopiga kelele ni walevi kwenye baa. Walokole wakiwa kanisani, hawapigi kelele. Wanamuomba Mungu na kumsifu."

Sauti za kumsifu Mungu sio kelele.
 
Sawa ila mm nkiokoka naihis ntakosa amani sasa saizi nipo huru sana, swala lakufurahia ndoa halina uhusiano wowote na ulokole acha umbea wako hapa, vip mbasha kilikumkuta nn kama kuokoka ndiyo furaha ya ndoa??
 
Utafiti gani unataka wakati uthibitisho wa kwanza ni ww hapo hv unaona hata akili yako ipo sawa hv wewe asilimia kubwa kila kwny huu uzi wanakuona amnazo tena bila kificho acha unawashawishi watu ujinga wakitapeli.
 
Unajua maana ya kelele? Wakija wengine wanaoabudu mungu wanayemjua wao wakakuwekea spika hapo kwako hazitakuwa kelele?
 
Unajua maana ya kelele? Wakija wengine wanaoabudu mungu wanayemjua wao wakakuwekea spika hapo kwako hazitakuwa kelele?
Sauti zenye lengo la kuudhi hizo ndio kelele. Wanaomwabudu na kumsifu Mungu hawana lengo hilo. Ila kama wewe humpendi Mungu sishangai nyimbo za sifa kwa Mungu ukiziita kelele. Kuna viwanja vya mpira vimejengwa karibu na makazi ya watu. Wakati wa mpira, mashabiki wanashangilia kwa sauti kubwa sana lakini huwezi kusikia watu wanasema hizo ni kelele.
 
Sauti zenye lengo la kuudhi hizo ndio kelele. Wanaomwabudu na kumsifu Mungu hawana lengo hilo.
Atakaye abudu anachojua yeye kuwa ndiye mungu anakuwa na lengo la kuudhi? Ustaadh akija kuweka maspika hapo kwako kila ijumaa anaita majini kwa kiarabu zitakuwa si kelele sababu hana lengo la kuudhi?
Ila kama wewe humpendi Mungu sishangai nyimbo za sifa kwa Mungu ukiziita kelele.
Imani yako si imani ya kila mtu, ukiwa na ustaarabu wa kiwango cha kujua hili kunamtambulisha pia MUNGU unayemuabudu kuwa ni wa wastaarabu. Nukuulize, kwanini makanisa hayaweki maspika karibu na mahospitali makubwa?
Kuna viwanja vya mpira vimejengwa karibu na makazi ya watu. Wakati wa mpira, mashabiki wanashangilia kwa sauti kubwa sana lakini huwezi kusikia watu wanasema hizo ni kelele.
Ni kelele. Kelele ni kelele hata zisiposemwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…