uduzungwa
JF-Expert Member
- Oct 12, 2016
- 552
- 543
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uza jumla na rejareja inalipa.
Mkuu chapa kazi achana na maneno ya wanafunzi wa chuo humu... Nina rafiki yangu alianza duka la Dawa kea mtaji milion 3... Mambo mengine alijua mbele kwa mbele...
Nchi hii ukitaka uanze Kitu kwa kukamikisha taratibu zote hutakuja kuanzisha Kitu , hata kujenga Nyumba tunaambiwa mpaka upitie ofisi za mipango miji mkoa na wilaya ila watu tunajenga Kama kawaida.
Cha msingi tafuta wenye hayo maduka wakupe siasa za huko then Zama mazima utaji-adjust humo humo ndani.
Sent using Jamii Forums mobile app
ForexWanajukwaa kwema.
Naomba nianze moja kwamoja kwenye hoja yangu ili nipate ushauri. Nimepata kasenti kadogo hivi kama 17m. Sasa nikawaza nifanye biashara gani na wazo likanijia nifanye biashara ya phamacy.
Nimetafuta eneo nimepata sehemu ambayo kodi yake ni laki 5. Sasa najiuliza nianze hiyo biashara kwa hayo mazingira na mtaji utarudi?Ishu ni hiyo kodi ndio inaniumiza kichwa sana. Ila eneo ni nzuri tu.
Naomba ushauri na mawazo zaidi. Ni mimi mpambanaji wa maisha.
Man Army
Sent using Jamii Forums mobile app
Bado hela ya kumlipa mpharmasia ambayo ni Mill 5+ ...... Pia mtu aliyesoma Dispensing Certificate na yeye anatakiwa kuwepoNashukuru sana kwa ushauri.
Ila mzigo sio lazima ninunue mwingi sana.
Naweza nunua mzigo wa 6m kwa kuanzia
6m nikalipa kodi
3m mambo ya ukarabati
Afu inabaki 5m.
Hapo vipi mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Bado hela ya kumlipa mpharmasia ambayo ni Mill 5+ ...... Pia mtu aliyesoma Dispensing Certificate na yeye anatakiwa kuwepo
Bado TRA unatakiwa uwe na EFD Mashine,
Sio dispensary ni dispensing ( mtoa dawa).Huyo mphamasia anatakiwa alipwe mwisho wa mwezi. Tuseme 1m
Efd mashine laki4
Cheti cha dispensary???
Ngoja nione itakuaje huko mbele
Nashukuru
Sent using Jamii Forums mobile app
Hela hii bro kufungua pharmacy ni mtihan bora duka la dawa....pharmacy ina mashart na vigezo vikubwa zaidi mfano..lazima uwe na cheti cha mpharmacia ambae ana degree na mshahara wake si chini ya 1m...Wanajukwaa kwema.
Naomba nianze moja kwamoja kwenye hoja yangu ili nipate ushauri. Nimepata kasenti kadogo hivi kama 17m. Sasa nikawaza nifanye biashara gani na wazo likanijia nifanye biashara ya phamacy.
Nimetafuta eneo nimepata sehemu ambayo kodi yake ni laki 5. Sasa najiuliza nianze hiyo biashara kwa hayo mazingira na mtaji utarudi?Ishu ni hiyo kodi ndio inaniumiza kichwa sana. Ila eneo ni nzuri tu.
Naomba ushauri na mawazo zaidi. Ni mimi mpambanaji wa maisha.
Man Army
Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri muruwa kabisa. Hatajuta.Hela ndogo sana hiyo mkuu .... Dukani lazima kiwepo cheti cha mpharmasia ambaye utamlipa Million 1 mpaka million 1.5 kwa mkataba wa miezi 6....
Bado hujalipa kodi ya chumba ambayo umesema ni laki 5 kwa mwezi....
Bado ukarabati wa chumba vinatakiwa viwepo vyumba viwili vikubwa na ufunge Air condition ... Bado Manunuzi ya mzigo dawa,
Ongeza ifike hata Mill 25
Au nakushauri uanze na duka la Dawa Muhimu ambalo gharama yake haizidi Mill 5
Mkuu,biashara sio rahisi kama ulivoandika hapa.kuna maswali mengi uanpaswa kuwa umeshauliza au kujiuliza mapaka wakati huu.Kama hujajiliza hayo maswali basi usifikiri kwamba biashara ni hivo tu.Je wewe ni Daktaria au Mfamasia?Hilo eneo ulilochagua ni nini kimekuvutia kulichagua?Kuna hospitali karibu au nini?Kumbuka kwamba kila biashara ina fursa na changamoto zake na pia lazima utambue uwezo wako na worst case scenarios.Nashukuru sana kwa ushauri.
Ila mzigo sio lazima ninunue mwingi sana.
Naweza nunua mzigo wa 6m kwa kuanzia
6m nikalipa kodi
3m mambo ya ukarabati
Afu inabaki 5m.
Hapo vipi mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa ndogo hiyo
Kwa mujibu wa sheria ya Famasi au PHARMACY ACT, Pharmacy ni sehemu ambayo chini ya usimamizi wa mfamasia ambaye amepewa dhamana ya uangalizi wa shughuli zake (Pharmaceutical services) itauza au kununua dawa zilizo kwenye makundi ya moto au Baridi nikiwa na maana dawa zinazohitaji uangalizi au prescription na dawa za kawaida au Over the counter medicines (OTC Medicines).
Watu wengi huchanganya kati ya Duka la dawa Muhimu (DLDM) na Pharmacy. Hivi ni vitu viwili tofauti na utofauti wake unakuja kuwa DUKA LA DAWA MUHIMU au kama yanavyojulikana kitaalamu (Accredited Drug Dispensing Outlets au ADDO) hayaruhusiwi kuuza baadhi ya dawa za moto kisheria, na ukikuta wanauza basi ujue ni kinyume na Sheria na Taratibu za Pharmacy Act na ni vyema ukatoa taarifa kwa vyombo husika au Baraza la Wafamasia.
Mtu yoyote anaweza kumiliki Famasi hata kama hana Taaluma ya Ufamasia ila atalazimika kumuajiri mfamasia kwa Part time au Full time na malipo mara nyingi hutegemea na makubaliano kati ya mmiliki na Mfamasia mwenyewe. Wengine huamua kuingia partnerships na wengine huamua kuwa huru kwa kuajiriwa kwa muda.
*Hatua Ya Kwanza*
Kama zilivyo biashara zingine ni vyema kwanza ukafanya utafiti binafsi kwa kuangalia *Location, economic status* ya watu wanaozunguka eneo hilo na *ushindani* wa kibiashara au kama kuna Famasi maeneo hayo ambayo yanaweza kukuletea ushindani mkubwa na kushindwa kufanikiwa kibiashara.
Baada ya kufanya hayo na kujiridhisha na eneo husika unalotaka kutoa huduma hiyo, mfuate mfamasia wa wilaya wa eneno hilo ili uweze kumweleza dhumuni lako na kukupa maelezo kama kuna maombi mengine yoyote ya uanzishwaji wa Famasi yaliyokwisha pelekwa kwenye eneo ulilochagua kufanya huduma hiyo.
Wengi huwa wanakurupuka kwa kulipia chumba cha biashara na baadae huingia hasara kwani wanakuta kuna mtu teyari kwenye eneo hilo ameshapeleka maombi ya kuanzisha Famasi kama yeye. Kisheria kuna umbali ambao lazima uwepo kati ya Famasi na Famasi na ili usiingie hasara hiyo ni vyema kabla hujalipia chumba cha biashara basi onana na mfamasia wa wilaya kwanza.
Ukubwa wa chumba cha Biashara pia ni kitu muhimu sana kuzingatia kwenye Biashara hii. Kama utataka kufungua Famasi ya rejareja, basi utatakiwa kuwa na chuma kisichopungua 25 meter square ili uweze kukigawa na kupata chumba cha mbele yaani counter, chumba cha kutolea dawa au Dispensing room na stoo ya dawa.
*Hatua Ya Pili*
Baada ya kuhakikisha eneo lako la biashara ni salama na chumba chako kina ukubwa unaotakiwa kadiri mfamasia wa wilaya alivyokushauri, basi lipia chumba chako na anza marekebisho kama utakavyoelekezwa na mfamasia wa wilaya ili pawe na muonekano wa kisasa na kuvutia kwa kuweka hizo partitioning kwa ajili ya chumba cha mbele, kutolea dawa na stoo! Wengi hupendelea kuweka partitioning za Aluminium lakini hata ceiling board na gypsum hukubalika na huokoa gharama.
Hakikisha hicho chumba kina mzunguko mzuri wa hewa kwa kuweka feni na Air conditioner! Sheria pia inataka kuwe na vigae chini ili kurahisisha usafi na kuzua maambukizi ya magonjwa au vumbi ambayo hupunguza nguvu za dawa au kuharibika. Pia unaweza kuweka mbwembwe zingine za kibiashara ili kuvutia wateja wako kama rolling adverts na vioo ukutani.
*Hatua Ya Tatu*
Ukishamaliza kufanya marekebisho yako na kama ulivyoshauriwa na Mfamasia wa Wilaya, unatakiwa kumwita ili aje kukukagua Jengo (Premise Inspection) na kukuandikia kibali ambacho utalazimika kulipia hizo form za ukaguzi na maombi ya kibali ambayo yakishajazwa hutumwa baraza la Famasi uweze kupewa leseni na ruhusa ya kuanzisha biashara yako (Licence and Permitt). Kwa kawaida hapa huwa kuna gharama za kulipia na gharama huongezeka kama mmiliki sio mfamasia, hulazimika kulipia professional fee ya Mwaka. Hii hatua huweza kucuhukua hata miezi mitatu au sita kukamilika au kupata kibali chako kwani Baraza la Wafamasia lazima likae vikao kupitia maombi yako.
Tukumbuke pia hii biashara ni tofauti na biashara zingine kwani ni huduma pia kwa jamii na ni ya kitaalamu. Mikataba ya ajira ya wataalamu kama Dispensing Nurse,Pharmaceutical Technician au Mfamasia wako lazima iwepo wakati wa ukaguzi na ujazaji wa form za leseni za Baraza la Wafamasia. Hii ina maana kwamba kama huna Medical background kwenye dawa utalazimika kuajiri hao watu muhimu ambao ni kati ya mfamasia au technician ili aweze kukusaidia kutekeleza majukumu ya utoaji huduma za dawa.
*Hatua Ya Nne*
Wengi wakishakaguliwa hukurupuka kwa kwenda kununua mzigo (Dawa) na kuziweka au kuzipanga stoo)!Cha msingi hutakiwi kuwa na papara, subiri vibali vyote vya baraza la Famasi umepata na leseni ya biashara kutoka kwa Afisa Biashara wa wilaya ndio ujihakikishie kuanza kununua dawa kutoka kwa whole salers au distributors.
*Hatua Ya Tano*
Hatua hii ni ya kufungua Famasi yako na teyari kwa kuanza huduma, kumbuka siku zote biashara ni ubunifu hivyo basi hakikisha wahudumu wako ni competent na wana ueledi wa kutosha kwenye kutoa maelezo sahihi ya dawa na matumizi yake!Hakikisha pia wahudumu muda wote ni wenye lugha nzuri kwa wateja wa rika zote na tabasamu muda wote!
Kama unajiweza kifedha ni vyema wahudumu wakawa na uniforms au makoti ya kitabibu(Medical coat) ili kuonekana professional zaidi na kuwavutia wateja.
Inashauriwa pia uwe na Water dispenser ili wateja wenye uhitaji wa lazima kuanza kunywa dawa papo hapo waweze kupata huduma hiyo bila kusahahu kipimo cha uzito kiwepo kuwawezesha wahudumu kutoa dozi za dawa sahihi kwa wateja hasa watoto chini ya miaka mitano.
*Cha Kuzingatia*
Kama zilivyo biashara zingine ni muhimu kujiandaa kwa fedha japo si lazima kiasi kikubwa (At least 20M), na biashara hii utalazimika kumuajiri mfamasia ili akusimamie Famasi yako na kwa sasa wafamasia hutoza si chini ya Tsh. 1,000,000/ kwa mwezi na huyo ni wa part time tu, hivyo basi ni vyema ukawa na kiasi cha kuanzia cha kutosha kwa ajili ya kumlipa advance hata ya miezi sita kabla biashara yako haija stabilize au kuzoeleka na kufanya vizuri.
Kwa sasa pia kuna makampuni au Distributors wanaokopesha dawa kwa wateja wake, hivyo unaweza pia kujihusiha na haya makampuni ili waweze kukukopesha dawa na kulipia baadae.
____________________
Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.
Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.
Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.
Sasa utaratibu ni huu:
1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.
2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.
3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.
4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) *imesema ni ruksa Mtanzania yeyote mwenye umri unaozidi miaka 18, kufungua duka la dawa muhimu za Binadamu na Mifugo (DLDM)*, hasa katika maeneo *ya Vijiji na Miji midogo* ambapo upatikanaji wa dawa muhimu ni wa matatizo.
Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba *watakaofungua maduka Vijijini watapewa kipaumbele kwani watu wengi yamejikita kufungua maduka hayo maeneo ya mijini.*
Alisema mwombaji *anapaswa kuwa tayari kupitia mafunzo ya mwezi mmoja ili kujua sheria na kanuni za uendeshaji wa maduka hayo*, ili kuonyesha utofauti wa uedeshaji duka la dawa baridi na moto ambapo wamiliki wake walikuwa hawana uelewa.
Simwanza alisema kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa DLDM, *mmiliki na mtoa dawa wanalazimika kuingia mkataba wa kazi kwa lengo la kusimamia utendaji,* kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.
Alisema DLDM ni maduka ya kutunza na kuuza dawa zisizohitaji cheti cha daktari na baadhi ya dawa hizo kuhitaji cheti cha daktari.
*Mtoa dawa katika maduka hayo ni lazima awe na sifa za awali kama fundi sanifu, ofisa muuguzi, tabibu na mhudumu wa afya au wawe wasaidizi katika ngazi hizo.*
Safi maelezo yameshiba,hivi mfamasia anaesimamia pharmacy anakuwa na elimu gani na anasoma miaka mingapi?Pesa ndogo hiyo