Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Wakuu Kama Kuna mtu ana uzoefu na Duka la Dawa za Binadamu( Duka baridi) aje atusaidie uzoefu, kwenye mtaji na mambo mengine ya kuzingatia! Asanteni.
 
Wateja wa condom wanahitaji usiri akikuta watu wawili dukani hanunui
 
Wakuu Kama Kuna mtu ana uzoefu na Duka la Dawa za Binadamu( Duka baridi) aje atusaidie uzoefu, kwenye mtaji na mambo mengine ya kuzingatia! Asanteni.
Hakuna duka la dawa baridi siku hizi,kuna pharmacy na duka la dawa muhimu(ADDO)
 
Hakikisha unaonana na Mfamasia wa wilaya yako, atakupa utaratibu namna ya kufungua duka la dawa muhimu au Pharmacy, kwa nama yeyote ile ukishapata jengo unalotarajia kufungua duka hilo,lazima mfamasia aje kufanya ukaguzi kuona kama limefwata vigezo vyote kutokana na sheria ya famasia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani mkuu, vipi kuhusu biashara yenyewe Sasa huna uzoefu wowote angalau ukashare nasi!
 
ninapenda kuuliza ni mtaji kiasi gani approximatelly unaweza kufungua pharmacy kwa maeneo ya dar es salaam
je milioni kumi yaweza tosha
NB .
nazungumzia pharmacy not duka la dawa muhimu
naomba kuwasilisha
 
Pesa ndogo hiyo

Kwa mujibu wa sheria ya Famasi au PHARMACY ACT, Pharmacy ni sehemu ambayo chini ya usimamizi wa mfamasia ambaye amepewa dhamana ya uangalizi wa shughuli zake (Pharmaceutical services) itauza au kununua dawa zilizo kwenye makundi ya moto au Baridi nikiwa na maana dawa zinazohitaji uangalizi au prescription na dawa za kawaida au Over the counter medicines (OTC Medicines).

Watu wengi huchanganya kati ya Duka la dawa Muhimu (DLDM) na Pharmacy. Hivi ni vitu viwili tofauti na utofauti wake unakuja kuwa DUKA LA DAWA MUHIMU au kama yanavyojulikana kitaalamu (Accredited Drug Dispensing Outlets au ADDO) hayaruhusiwi kuuza baadhi ya dawa za moto kisheria, na ukikuta wanauza basi ujue ni kinyume na Sheria na Taratibu za Pharmacy Act na ni vyema ukatoa taarifa kwa vyombo husika au Baraza la Wafamasia.

Mtu yoyote anaweza kumiliki Famasi hata kama hana Taaluma ya Ufamasia ila atalazimika kumuajiri mfamasia kwa Part time au Full time na malipo mara nyingi hutegemea na makubaliano kati ya mmiliki na Mfamasia mwenyewe. Wengine huamua kuingia partnerships na wengine huamua kuwa huru kwa kuajiriwa kwa muda.

*Hatua Ya Kwanza*

Kama zilivyo biashara zingine ni vyema kwanza ukafanya utafiti binafsi kwa kuangalia *Location, economic status* ya watu wanaozunguka eneo hilo na *ushindani* wa kibiashara au kama kuna Famasi maeneo hayo ambayo yanaweza kukuletea ushindani mkubwa na kushindwa kufanikiwa kibiashara.

Baada ya kufanya hayo na kujiridhisha na eneo husika unalotaka kutoa huduma hiyo, mfuate mfamasia wa wilaya wa eneno hilo ili uweze kumweleza dhumuni lako na kukupa maelezo kama kuna maombi mengine yoyote ya uanzishwaji wa Famasi yaliyokwisha pelekwa kwenye eneo ulilochagua kufanya huduma hiyo.

Wengi huwa wanakurupuka kwa kulipia chumba cha biashara na baadae huingia hasara kwani wanakuta kuna mtu teyari kwenye eneo hilo ameshapeleka maombi ya kuanzisha Famasi kama yeye. Kisheria kuna umbali ambao lazima uwepo kati ya Famasi na Famasi na ili usiingie hasara hiyo ni vyema kabla hujalipia chumba cha biashara basi onana na mfamasia wa wilaya kwanza.

Ukubwa wa chumba cha Biashara pia ni kitu muhimu sana kuzingatia kwenye Biashara hii. Kama utataka kufungua Famasi ya rejareja, basi utatakiwa kuwa na chuma kisichopungua 25 meter square ili uweze kukigawa na kupata chumba cha mbele yaani counter, chumba cha kutolea dawa au Dispensing room na stoo ya dawa.

*Hatua Ya Pili*

Baada ya kuhakikisha eneo lako la biashara ni salama na chumba chako kina ukubwa unaotakiwa kadiri mfamasia wa wilaya alivyokushauri, basi lipia chumba chako na anza marekebisho kama utakavyoelekezwa na mfamasia wa wilaya ili pawe na muonekano wa kisasa na kuvutia kwa kuweka hizo partitioning kwa ajili ya chumba cha mbele, kutolea dawa na stoo! Wengi hupendelea kuweka partitioning za Aluminium lakini hata ceiling board na gypsum hukubalika na huokoa gharama.

Hakikisha hicho chumba kina mzunguko mzuri wa hewa kwa kuweka feni na Air conditioner! Sheria pia inataka kuwe na vigae chini ili kurahisisha usafi na kuzua maambukizi ya magonjwa au vumbi ambayo hupunguza nguvu za dawa au kuharibika. Pia unaweza kuweka mbwembwe zingine za kibiashara ili kuvutia wateja wako kama rolling adverts na vioo ukutani.

*Hatua Ya Tatu*

Ukishamaliza kufanya marekebisho yako na kama ulivyoshauriwa na Mfamasia wa Wilaya, unatakiwa kumwita ili aje kukukagua Jengo (Premise Inspection) na kukuandikia kibali ambacho utalazimika kulipia hizo form za ukaguzi na maombi ya kibali ambayo yakishajazwa hutumwa baraza la Famasi uweze kupewa leseni na ruhusa ya kuanzisha biashara yako (Licence and Permitt). Kwa kawaida hapa huwa kuna gharama za kulipia na gharama huongezeka kama mmiliki sio mfamasia, hulazimika kulipia professional fee ya Mwaka. Hii hatua huweza kucuhukua hata miezi mitatu au sita kukamilika au kupata kibali chako kwani Baraza la Wafamasia lazima likae vikao kupitia maombi yako.

Tukumbuke pia hii biashara ni tofauti na biashara zingine kwani ni huduma pia kwa jamii na ni ya kitaalamu. Mikataba ya ajira ya wataalamu kama Dispensing Nurse,Pharmaceutical Technician au Mfamasia wako lazima iwepo wakati wa ukaguzi na ujazaji wa form za leseni za Baraza la Wafamasia. Hii ina maana kwamba kama huna Medical background kwenye dawa utalazimika kuajiri hao watu muhimu ambao ni kati ya mfamasia au technician ili aweze kukusaidia kutekeleza majukumu ya utoaji huduma za dawa.

*Hatua Ya Nne*

Wengi wakishakaguliwa hukurupuka kwa kwenda kununua mzigo (Dawa) na kuziweka au kuzipanga stoo)!Cha msingi hutakiwi kuwa na papara, subiri vibali vyote vya baraza la Famasi umepata na leseni ya biashara kutoka kwa Afisa Biashara wa wilaya ndio ujihakikishie kuanza kununua dawa kutoka kwa whole salers au distributors.

*Hatua Ya Tano*

Hatua hii ni ya kufungua Famasi yako na teyari kwa kuanza huduma, kumbuka siku zote biashara ni ubunifu hivyo basi hakikisha wahudumu wako ni competent na wana ueledi wa kutosha kwenye kutoa maelezo sahihi ya dawa na matumizi yake!Hakikisha pia wahudumu muda wote ni wenye lugha nzuri kwa wateja wa rika zote na tabasamu muda wote!
Kama unajiweza kifedha ni vyema wahudumu wakawa na uniforms au makoti ya kitabibu(Medical coat) ili kuonekana professional zaidi na kuwavutia wateja.

Inashauriwa pia uwe na Water dispenser ili wateja wenye uhitaji wa lazima kuanza kunywa dawa papo hapo waweze kupata huduma hiyo bila kusahahu kipimo cha uzito kiwepo kuwawezesha wahudumu kutoa dozi za dawa sahihi kwa wateja hasa watoto chini ya miaka mitano.

*Cha Kuzingatia*
Kama zilivyo biashara zingine ni muhimu kujiandaa kwa fedha japo si lazima kiasi kikubwa (At least 20M), na biashara hii utalazimika kumuajiri mfamasia ili akusimamie Famasi yako na kwa sasa wafamasia hutoza si chini ya Tsh. 1,000,000/ kwa mwezi na huyo ni wa part time tu, hivyo basi ni vyema ukawa na kiasi cha kuanzia cha kutosha kwa ajili ya kumlipa advance hata ya miezi sita kabla biashara yako haija stabilize au kuzoeleka na kufanya vizuri.

Kwa sasa pia kuna makampuni au Distributors wanaokopesha dawa kwa wateja wake, hivyo unaweza pia kujihusiha na haya makampuni ili waweze kukukopesha dawa na kulipia baadae.

____________________
Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.

Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.

Sasa utaratibu ni huu:
1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.
2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.
3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.
4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) *imesema ni ruksa Mtanzania yeyote mwenye umri unaozidi miaka 18, kufungua duka la dawa muhimu za Binadamu na Mifugo (DLDM)*, hasa katika maeneo *ya Vijiji na Miji midogo* ambapo upatikanaji wa dawa muhimu ni wa matatizo.

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba *watakaofungua maduka Vijijini watapewa kipaumbele kwani watu wengi yamejikita kufungua maduka hayo maeneo ya mijini.*

Alisema mwombaji *anapaswa kuwa tayari kupitia mafunzo ya mwezi mmoja ili kujua sheria na kanuni za uendeshaji wa maduka hayo*, ili kuonyesha utofauti wa uedeshaji duka la dawa baridi na moto ambapo wamiliki wake walikuwa hawana uelewa.

Simwanza alisema kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa DLDM, *mmiliki na mtoa dawa wanalazimika kuingia mkataba wa kazi kwa lengo la kusimamia utendaji,* kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Alisema DLDM ni maduka ya kutunza na kuuza dawa zisizohitaji cheti cha daktari na baadhi ya dawa hizo kuhitaji cheti cha daktari.

*Mtoa dawa katika maduka hayo ni lazima awe na sifa za awali kama fundi sanifu, ofisa muuguzi, tabibu na mhudumu wa afya au wawe wasaidizi katika ngazi hizo.*
 
Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) *imesema ni ruksa Mtanzania yeyote mwenye umri unaozidi miaka 18, kufungua duka la dawa muhimu za Binadamu na Mifugo (DLDM)*, hasa katika maeneo *ya Vijiji na Miji midogo* ambapo upatikanaji wa dawa muhimu ni wa matatizo.

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba *watakaofungua maduka Vijijini watapewa kipaumbele kwani watu wengi yamejikita kufungua maduka hayo maeneo ya mijini.*

Alisema mwombaji *anapaswa kuwa tayari kupitia mafunzo ya mwezi mmoja ili kujua sheria na kanuni za uendeshaji wa maduka hayo*, ili kuonyesha utofauti wa uedeshaji duka la dawa baridi na moto ambapo wamiliki wake walikuwa hawana uelewa.

Simwanza alisema kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa DLDM, *mmiliki na mtoa dawa wanalazimika kuingia mkataba wa kazi kwa lengo la kusimamia utendaji,* kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Alisema DLDM ni maduka ya kutunza na kuuza dawa zisizohitaji cheti cha daktari na baadhi ya dawa hizo kuhitaji cheti cha daktari.

*Mtoa dawa katika maduka hayo ni lazima awe na sifa za awali kama fundi sanifu, ofisa muuguzi, tabibu na mhudumu wa afya au wawe wasaidizi katika ngazi hizo.*
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]..
 
safi sana @mwifa nikuulize kitu,je kama mm ni mfamasia unajua ajira hz za leo magumashi mengi je naweza kutumia kama shilingi ngapi kuanzisha premise kwa million 10 si unajua tena familia zetu hz
 
Hiyo premises uliyoilenga hapo ni ya namna gani? Retaile Pharmacy? Shop? Whole sale pharmacy? Processing unit?
 
ninapenda kuuliza ni mtaji kiasi gani approximatelly unaweza kufungua pharmacy kwa maeneo ya dar es salaam
je milioni kumi yaweza tosha
NB .
nazungumzia pharmacy not duka la dawa muhimu
naomba kuwasilisha
[QUO
Ukifanikisha kufungua karibu dukani tukuuzie jumla jumla
Whatsap 0758788801
 
Asante kwa maelekezo mazuri,
Swali: Nikihitaji kupata hayo mafunzo ya mwez mmoja napata wapi? Kuna gharama yoyote?
 
Back
Top Bottom