Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Habari Wakuu

Baada ya kufanya research kidogo nimegundua maduka ya Pharmacy yameongezeka sana na yanazidi kufunguliwa, nahisi hii biashara ina faida nzuri japo sijapata mtu wa kunieleza kiundani sababu wanaoifanya wengi wanakuwa wasiri.

Je,
1. Ni kweli hii biashara inalipa?
2. Ni vigezo gani unatakiwa kutimiza ili uifanye?
3. Gharama zake zikoje ukiachana na kodi ya pango?
4. Kwa duka la Rejereja unatakiwa angalau uwe na mtaji wa kuanzia shilingi ngapi?, kwa jumla je?
5.Changamoto zake ni zipi?

Mwenye majibu angalau hata ya swali moja naomba anieleze.
Natakungliza Shukurani!
Mkuu ulifikia wapi? naomba mrejesho
 
Ndugu yangu, naomba na mimi nikupe mwanga zaidi kwa faida ya wengine.

Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.

Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.

Sasa utaratibu ni huu:

1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.

2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.

3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.

4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.

Thank you

Mwananchi mwenzenu.
Sorry mkuu nimeyapenda mawazo yako pia naomba unitumie nami hicho kitabu cha mwongozo wa DLDM ahsante Sana gmail yangu,. deushoja1993@gmail.com
 
Nauza duka la dawa kwa mwenye uhitaji anione nmeshindwa kuambatanisha picha... ni 3.3m, limelipiwa kodi mpka mwezi wa 12 na lesen ya biashara mpka mwakani na vibali vingne
Hiyo labda DLDM.

Pharmacy haiwezi kuwa na thamani hiyo, labda haina dawa na unauza tu vitendea kazi
 
Ngoja waje
 

Attachments

  • FB_IMG_16356227884522008.jpg
    FB_IMG_16356227884522008.jpg
    17.2 KB · Views: 99
Haiko hivyo ushauri anza hiyo biashara story za kumpa mphamasia 1.5m sijui laki 8 ni ngonjera unampa hata laki 2 kulingana na mauzopia mnaweza mkaingia mkataba ama partnership unamlipa % fulani ya faida

Phamacy zipo za jumla na rejareja so kwa visenti vyako utakuwa na pharmacy ya rejareja natumaini unatambua tofauti ya DLDM na pharmacy.

Unaweza kuanza na DLDM baadae uka upgrade kuwa pharmacy muhimu uwe forecast. Industry ya Dawa ni ngumu kama zilivyo biashara zingine na usipokuwa makini hii ni ngumu sana ina mambo mengi na ujanja kama biashara zingine.

Uzoefu ni 30% ya mtaji mtu ambaye tayari anamiliki Duka la Dawa muhimu kwa pesa yako anaweza kufanya kazi ya 24m hizo display cases nunua materials fundi akutengenezee. Anza na displays 4
Kubwa moja upana 6ft na urefu 6ft kila ngazi iwe na 33cm ni nzuri zaidi

Counter display 6ft by 3ft but ngazi ziwe pana 33cm
Na mbili ndogo za ukutani 3ft by 3ft .
Kununua Dawa nako ni Shida nyingine tegemea na distributors muhimu kuwa na taarifa sahihi na uwe na muda wa usimamizi by the way kupata pesa za kurun vizuri daily sales inabid iwe kuanzia 100k na ukianza vibaya miezi 6 ya mwanzo tayari unakuwa ushafilisika.

Pharmacy rejareja na DLDM huitaji EFD mashine unalipia tu mapato
Leseni ni 200k kwa 100k vingine utajifunzia mbele kwa mbele wauzaji malipo ni 150-200k including meals and transport wazoefu ni wazuri na ni wezi wabobezi wanacheza na logbook na sales book too.

Kugundua tofauti ni kazi kupata muuzaji mwaminifu na mchangamfu anaependa anachokifanya pia ni mtaji hasa kwa wanaoanza. Kwa sasa usipende kuzijua changamoto sana ukijua ya ndani zaidi hutofanya biashara yeyote
Mkuu umesomeka sana. Humu wa-pharmacy-a wanajipigia promo juu kwa juu. Eti malipo kwa mwezi kwa mphamasia analipwa 1m. Fix tuuu.

Mtu ana 15mil, unamwambia haitoshi awe na 30m. Sio Kila mtu anafungua pharmacy kariakoo bhana. Wafamasia acheni kuwatisha wajasiriamali, wakati hamna hata dldm za 1mil.
 
Back
Top Bottom