Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Dulla maneno mengi Sana alafu uwezo mdogo.
Leo sikuwa upande wowote ili niangalie kaa Uhuru Pambano hili. Kwa kweli Dulla kapigwa pasipo kuacha Shaka yoyote
Alafu alitaka amuotee raundi ya Kwanza na Ngumi yake ya kichawi.
Ile Ngumi Kwa Sisi wenye jicho la tatu ilikuwa Ngumi ya USHINDI Kwa Dulla, kitendo cha Twaha kuendelea kulimchanganya na kumaliza nguvu Dulla
Ha ha haDula ana mikwara mingi ila Hana uwezo [emoji4][emoji4][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ha ha haDullar hawezi mkono..hata mimi nikisimama nae namkalisha vizuri tu.
Hawajawahi kupigana ,huyo kijana wa Tanga anamkwepa sana kijana wa Morogoro.Huyu kijana wa Morogoro aliyeshinda hivj wamewahi pigana na yule kijana wa Tanga?
Wamepigana mara tatu ,na zote Dulla amepigwa.Bahati mbaya sana umechambua Kimahaba na siyo Kiutaalam / Kiufundi zaidi.
Kuna Bondia hapa umemtaja kuwa ni Mjivuni mbona nawe pia unaonekana ni Mjivuni na Mbinafsi?
Je, ikitokea wakarudiana na Dulla akaibuka Mshindi utakuja kusemaje labda hapa Kwetu Great Thinkers?
Ile ilikuwa ndumba live bila chenga.Mimi sio bondia Mkuu.
Na nimeshaeleza kuwa Mimi napenda sifa, ndivyo nilivyo,
Hata warudiane mara ngapi Dulla Hana uwezo wa kumpiga Twaha, labda Kwa ndumba Kama alivyotaka kufanya katika raundi ya Kwanza.
Hii ni mara ya tatu Wanapigana. Na Dulla zote kakaa.
Kama ulikuwa unaangalia mechi ya Jana utaungana na Mimi kuwa Dulla hamuwezi Twaha.
Ni ubishi wake wa kizaramo na mdomo mwingi ambao wanaume WA Dar wamejaliwa
Ha ha haWanaume wa daslam ukipigana nao kwa maneno huwawez kuwashinda hapo wanachukua had kombe la dunia ila mvute kati kwenye ulingo mpige jab 1, left-hook 1, Right-hook 1, overhand Right 1 alaf mmalizie na uppercut 1 anaanguka chali miguu juu haamki tena.
Zile kelele za sijui "niling'atwa na mbuzi" zinaishia hapo
Ha ha haDulla Mbabe kelele nyiingi kumbe uwanjani sifuri.
Aibu sana yaani anapigwa ngumi tatu yeye anarudisha moja tena isiyo na macho mpaka mwisho anaamua kukimbia kimbia tu ili walau ashindwe kwa points. Lol.
Kwa kweli Dulla angefanikiwa kumaliza pambano ile raundi ya kwanza ,angeongea shombo sana.Jana nimesfurahi sana yaaani
Ha ha haRaund ya kwanza nkajua kiduku kapoteza asee, ila niyule kiwete nahis ndo mganga wa dulla kafanya mambo mpaka raund ya kwanza ikawa vile
Selemani Kidunda ,mziki mwingine huo mkuu.Kidunda hatamaliza Raundi Saba atapigwa.
Kidunda ni mbishi lakini akipata mchezaji mzuri anayeshambulia wakati wote hatoboi
HaswaaaaSema Dulla kikomazi, mvumilivu na mbishi. Kwa Ngumi zile Kama ni bondia mwingine asingetoboa raundi ya 7.
Kidunda hachomoi nakuambia
Niliumia mno.Daa ile ngumi aliyopigwa Twaha na kuanguka, niliumia mnooo nikasema leo bondia wangu Twaha kazi ipo, lakini shukrani kwa kocha na Twaha mwenyewe kwa kurudi kwenye mchezo na kumtwanga Dullah mwanzo mwisho.
Hii ndio maana halisi ya Makodinda Makostamina, bendela chuma mlingoti chuma, ngumi zimesimama haina konakona, haina kamwambie nani, show show. Easy Power. Twaha Kiduku Mnyama.
Imagine bila ushirikina ingekwaje Kama na ushirikano bado kadundwaDulla licha ya kutumia ushirikina bado akaambulia kichapo cha mbwa koko.
Sana kaka, ilikua ni bomba moja ya hatari sanaNiliumia mno.
Mkuu nimemfahamu Kidunda kwa muda mrefu sana tangu miaka hiyo mburahati kwa shebe, ameanza kupigana hajulikan kwenye media, kadondosha sana mabondia wengi, mpaka mabondia wa Jeshi, mpaka Jeshi likamchukua na kumpa ajira kupitia ngumi. Mpaka sasa anatumikia JWTZ na huku akifanikiwa sana katika career yake ya ngumi. Ni bondia mzuri sana, mwenye nidhamu ndani na nje ya ulingo.Selemani Kidunda ,mziki mwingine huo mkuu.
Mkuu nimemfahamu Kidunda kwa muda mrefu sana tangu miaka hiyo mburahati kwa shebe, ameanza kupigana hajulikan kwenye media, kadondosha sana mabondia wengi, mpaka mabondia wa Jeshi, mpaka Jeshi likamchukua na kumpa ajira kupitia ngumi. Mpaka sasa anatumikia JWTZ na huku akifanikiwa sana katika career yake ya ngumi. Ni bondia mzuri sana, mwenye nidhamu ndani na nje ya ulingo.
Selemani Kidunda ni bondia mwenye ngumi nzito, mbishi ulingoni, anavumilia ngumi, ni mtaalam wa K'O.
Selemani Kidunda na Twaha Kiduku wanafanana kwa asilimia kubwa sana. Wote wana uwezo mkubwa sana Technically wapo vizuri ndani ya uwanja. Japo Twaha Kiduku anamzidi Sele Kidunda katika speed ya kuattach na guarding (kujilinda). Binafsi sitamani kabisa pambano hili likitokea kwanza. Ila natamani kwanza Selemani kidunda apigane na Dullah Mbabe akimalizana nae Dullah, ndio aje kwa Twaha Kiduku.
Pambano kati ya Twaha Kiduku vs Selemani Kidunda kama likifanikiwa kutokea, basi naamini wapenzi wa ngumi watashuhudia pambano zuri na bora pengine kuwahi kutokea Tanzania. Hii ni kutokana na ubora wa Mabondia hawa wawili.