Mkuu nimemfahamu Kidunda kwa muda mrefu sana tangu miaka hiyo mburahati kwa shebe, ameanza kupigana hajulikan kwenye media, kadondosha sana mabondia wengi, mpaka mabondia wa Jeshi, mpaka Jeshi likamchukua na kumpa ajira kupitia ngumi. Mpaka sasa anatumikia JWTZ na huku akifanikiwa sana katika career yake ya ngumi. Ni bondia mzuri sana, mwenye nidhamu ndani na nje ya ulingo.
Selemani Kidunda ni bondia mwenye ngumi nzito, mbishi ulingoni, anavumilia ngumi, ni mtaalam wa K'O.
Selemani Kidunda na Twaha Kiduku wanafanana kwa asilimia kubwa sana. Wote wana uwezo mkubwa sana Technically wapo vizuri ndani ya uwanja. Japo Twaha Kiduku anamzidi Sele Kidunda katika speed ya kuattach na guarding (kujilinda). Binafsi sitamani kabisa pambano hili likitokea kwanza. Ila natamani kwanza Selemani kidunda apigane na Dullah Mbabe akimalizana nae Dullah, ndio aje kwa Twaha Kiduku.
Pambano kati ya Twaha Kiduku vs Selemani Kidunda kama likifanikiwa kutokea, basi naamini wapenzi wa ngumi watashuhudia pambano zuri na bora pengine kuwahi kutokea Tanzania. Hii ni kutokana na ubora wa Mabondia hawa wawili.