Dully alaumu wasanii ambao hawakuja kumzika baba yake

Duuuh,,!! Ajirekebishe mambo kama hayo ya msiba ya msingi sana kuhudhulia maana leo kwako kesho kwangu,, au yeye yakimfika zari na wema ndio watakao mpa company labda

Hivi huu msiba ulipangwa utatokea lini? Mligawa kadi? mlikuwa mnafanya sensa? wanao lalamika wamehudhuria misiba yote?
 
kuna watu wana mipasho Hadija Koppa mwenyewe hata subiri sana
 
Mswahili hakosi neno, na hivi diamond ana vihela ndo basi tena,
Hivi kati ya hao mastaa ni yupi alienda kumpa pole mama yake diamond akiwa india au akiwa hapa bongo?

Daaah....kweli mkuu hata huyo dully mwenyewe hajaenda hata kumpa pole baada ya kurudi kutoka india lkn hao ndo binadamu......one eyed claims
 
Mswahili hakosi neno, na hivi diamond ana vihela ndo basi tena,
Hivi kati ya hao mastaa ni yupi alienda kumpa pole mama yake diamond akiwa india au akiwa hapa bongo?

Hata huyo Dully na hao wanao toa lawama nacho jiuliza walisha hudhuria kila msiba?
 
hapo ndipo ninaposhangaa. yaani tumefika mahali tunamuhesabia mtu misiba mingapi kahudhuria? jamani hao waliohudhuria walitosha kabisa kumfariji mfiwa

Huyu mfiwa ana lake jambo si bure..ninacho jiuliza huu msiba aliupanga mpaka kila mtu ahudhurie?
 
Kwa Diamond mtasema mwisho mtachoka.atakae mchafua Diamond ni yeye mwenyewe,si magazeti,si blog wala si hapa.tafakari wewe na nafsi yako misiba mingapi hukwenda,kwasababu gani then njoo mwongelee mtoto wa bi sandra.
 
Kuja kwa watu inategemea na yeye anashiriki vipi kwenye matatizo ya wenzake, kama anashirikiana nao kula bata tu basi asilalamike.
 
Tatizo wanataka kusafiri nyota ya kijana wa watu.Kwani baba yake Dully ni nani mpaka wasanii wote wahudhurie msiba wake?

Kilicho nishangaza zaidi nikusikia Dully kalalamika.... ninacho jiuliza huu msiba aliupanga? yeye huwa ana hudhuria kila msiba?
 
Nadhani angetoa shukrani kwa watu wore walioshiriki kumsitiri mzazi wake badala yake anafanya sensa isio na bajeti huo si uungwana najua kina watu wengi wasio maarufu walikuwapo sasa kama wote hao hawana thamani I la kawaona wasanii wenzewe abadirike.
 
Baada yakuangalia ya msiba wanaanza kuongea na magazeti,akija D alokufa harejei kua hai wala asipokuja habadilishi chochote lakini hashuo zimewazidi...

Mtu ana anza kufanya sensa ya watu na kuanza kuwakashifi eti hawakuja kwakuwa walifikiri atataka pesa zaidi..nimeshangazwa haya maneno kusemwa na mtu kama Dully nilifikiri amekuwa kiakili.
 
Si Diamond pekee, ila wasanii wengi sana ambao walipaswa kwenda kumzika mzee sykes hawakujitokeza, tunajua huyu mzee aliishi vipi na baadhi ya wasanii na ushikaji wa Dully na wasanii. Lakini ndio hivyo labda watajifunza ila kama hawajajifunza basi wajifunze kwa Jakaya uungwana wa kitanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…