Duni Haji: Wapinzani tusipoungana CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo. Alichoongea Zitto ndicho Lissu alichoongea na Rais Samia

Duni Haji: Wapinzani tusipoungana CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo. Alichoongea Zitto ndicho Lissu alichoongea na Rais Samia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo mzee Juma Duni Haji amesema endapo Wapinzani hawataamka kutoka usingizini na kuungana basi CCM itaendelea kutawala kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.

Mzee Duni amesema alichokiongea Zitto Kabwe pale Dodoma mbele ya Rais Samia ndio hicho hicho alichokiongea Tundu Lisu na Rais Samia kule Ubelgiji hivyo tofauti ni sehemu tu ya kuongelea.

Duni amesema kuwa chama kinara cha upinzani haisaidii chochote kwani NCCR ilishakuwa, CUF ilishakuwa na Chadema ilishakuwa lakini hakuna lolote la maana lililofanyika, so dawa ni kuungana tu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Alikuwepo CDM akapewa nafasi ya kuwa mgombea mwenza, lakini aliondoka kwa kusema kila mtu ni kambale. Sasa huo umoja anautaka wa nini? Wamegundua ACT haina ushawishi huku bara, sasa anataka muungano utakaowapandisha wao. Acha CCM itawale hiyo miaka 1,000 lakini sio kwa ridhaa ya umma.
 
Alikuwepo cdm akapewa nafasi ya kuwa mgombea mwenza, lakini aliondoka kwa kusema kila mtu ni kambale. Sasa huo umoja anautaka wa nini? Wamegundua ACT haina ushawishi huku bara, sasa anataka muungano utakaowapandisha wao. Acha ccm itawale hiyo miaka 1,000 lakini sio kwa ridhaa ya umma.
Upande wa Zanzibar napo hawana chao maana CUF imefufuka huku bara CHADEMA bado ni mwalimu wao
 
Kwani huyo zito alitokea wapi? Kwanini asingebaki hukohuko qlikokua. Unaleta chokochoko upewe taraka baade unasema bora turudiane?
 
Back
Top Bottom