Duni Haji: Wapinzani tusipoungana CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo. Alichoongea Zitto ndicho Lissu alichoongea na Rais Samia

Duni Haji: Wapinzani tusipoungana CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo. Alichoongea Zitto ndicho Lissu alichoongea na Rais Samia

kuiondoa tu CCM ni sawa ndio. Shida ni tunampa nani kwa sababu zipi. Hata wakiungana, lkn je, wanastahili kutuongoza? Kuungana ndio kutawapa sifa ya kufanya tuwachague?
 
Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo mzee Juma Duni Haji amesema endapo Wapinzani hawataamka kutoka usingizini na kuungana basi CCM itaendelea kutawala kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.

Mzee Duni amesema alichokiongea Zitto Kabwe pale Dodoma mbele ya Rais Samia ndio hicho hicho alichokiongea Tundu Lisu na Rais Samia kule Ubelgiji hivyo tofauti ni sehemu tu ya kuongelea.

Duni amesema kuwa chama kinara cha upinzani haisaidii chochote kwani NCCR ilishakuwa, CUF ilishakuwa na Chadema ilishakuwa lakini hakuna lolote la maana lililofanyika, so dawa ni kuungana tu.

Maendeleo hayana vyama!
Mbona wao kina duni na ACT yao ya michongo wameungana na CCM?
 
kuiondoa tu CCM ni sawa ndio. Shida ni tunampa nani kwa sababu zipi. Hata wakiungana, lkn je, wanastahili kutuongoza? Kuungana ndio kutawapa sifa ya kufanya tuwachague?
Sifa ya kufanya watu wachaguliwe ni ipi?
 
Back
Top Bottom