Dunia bila ya Ukiranja wa Marekani itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana

Dunia bila ya Ukiranja wa Marekani itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana

Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.

Wote tutavalushwa surui fupi na kobasi.
 
Ukiwambia hivyo wairaq na walibya wanaweza kukugeuza kitoeo
 
Kwani Libya, Iraq, Syria, Vietnam na kwingineko USA na washirika wao walipozivamia na kujaribu kuwaondoa na kuwaua viongozi na raia wasio na hatia, walikuwa viranja wa dunia?

Kote USA na washirika wake walipopita wameacha maafa maakubwa, na hizo nchi hakuna amani wala utulivu tena.

Allen Kilewella huo ukiranja unaompamba nao USA ni huo wakumpa uhuru mke wako au kijana wako akaolewe na jinsi yake? Vipi siku mke wako akaomba talaka ili akaolewe na mwanamke mwenzake, utarudi hapo kumsifia?
Walio muua Gaddafi pale kwenye mtaro wabarabara ni walibya wenyewe tena wakawa wanambuluza kama kibaka sijaona mzungu pale inasikitisha sana japo USA katoa support ila wajinga niwalibya wenyewe wangempenda rais wao walingekubali kushawishiwa... Kwanzia tripol, benghaz, banwarid, silte kote huko walibya walitoa support jamaa auawe
 
Sasa nchi kama Iran ndo iwe superpower nazani kile wanachofanyiwa wandamanaji wakuvaa hijab ndo ingekua lifestyle.... Mashia wangetamba sunni wangeisoma
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
Unajua content ya marekani. Au u ajua marekani ni physical body. Ile ni spirit you have to bow to the owl mzee
 
Tangu Marekani iwe kiranja dunia imekuwa na amani, maendeleo, utangamano na mafanikio zaidi kuliko wakati wowote hii ni pamoja na madhaifu na matatizo yote ambayo Marekani inatuhumiwa nayo.
Kuanzia baada ya WWII hadi karne ya 21 ndicho kipindi dunia imezidi kuboreka zaidi kuliko karne nyingine zozote.
Mataifa ya kiarabu kama syria, Libya, Afghanistan, n.k wanaweza kuwa na mawazo tofauti.
Au wao sio eneo la dunia?
 
Majibu yako yapo shallow mno.
Unajibu bora liende tu.

Nimekuuliza kwanini unajibu eti kulingana na yanayoendelea!!!! This is a childish answer. Mtu msomi na GT hawezi akajibu kizembe hivi. Mada umeianzisha imekushinda uwezo.

Ukiulizwa kwanini lazima utoe sababu za:-
1. Kijamii
2. Kiuchumi
3. Kisiasa.

Ueleze kiundani kwanini unasema dunia itakuwa uwanja wa kuchinjana?
Toa mifano kwa kutumia statistical data.

Leta references ku support majibu yako.

Leta mlinganisho kuanzia baada ya vita vya pili vya dunia mpaka sasa nchi zipi zimeua watu wengi ndipo uweze fanya forecast ya future.

Ukianzisha topic nzito usilete majibu mepesi kama mtoto wa chekechea.

Hilo ni swali moja nahitaji elaboration kabla hatujaendelea na maswali mengine.

Karibu ujibu........
Ajabu sana.
Mtu anachukua statement nzito anakuja kuipost tu pasipo kutoa sababu yoyote kusuport hoja yake.

Mtoa mada ametupunja sana.
 
Waulize Wa-Japan kule Nagasaki na Hiroshima..., Vietnam na Bila kusahau Afghanistan n.k. Unadhani ni kipi kiliwapata watu kama Patrice Lumumba ? How is / was Libya before and after US interference; how was / is Iran before and after US interference ?

Na inferiority complex kudhani hauwezi mpaka uwepo wa fulani..., Na ndio maana United Nations imekuwepo lakini kazi zake zimekuwa hindered na VETO za nchi kama USA.....

Inasikitisha sana kuwa marginalized ila inasikitisha zaidi kukubaliana na hio hali kwa kuona kwamba ni sawa... Kweli tunahitaji Emancipation....
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
Usikonde hao hawataweza kwa sababu bila democracy huwezi tawala duniani. Wamebakia na udikteta wao na ujinga wa kufikiri watatawala fikra za watu kitu ambacho hakiwezekani
 
The world currently is becoming so volatile and dynamic.
The USA and it's allies which has for Long time exerted it's heagomy around the world is now been challanged by China and it's allies.
The question is can this two groups co exist harmoniously and peaceful?
As for me don't believe in multi pole world it's has never existed and I believe will never existed on group has to be at the top with one superpower on top of them, the. Which group will prevail and by which means,l? By conventional war? By economic war or by nuclear war?
What's the position of Africa and Tanzania in particular?
Do we stand to benefit or to loose from this global reset?
I would advise our leaders in Africa to stand affirm in their position and not play puppet to any group?
In this environment Africa should have one voice which can be archived by sincere unity among African leaders
All engagement with those powers.
 
Yeye si anasifiwa kiranja na mleta amani sasa ameshindwa vipi kuzuia ,kama kiranja haijalishi ameta au hajaleta kazi yake ni kuweka mambo sawa.

Huko Rwanda mfano CIA walikuwa na information kuhusu kila kitu kinachoendelea na kipi kitakuja kutokea lakini hawakufanya lolote la maana mpaka yakatokea yaliyotokea , USA ni kiranja wa mchong.
Kama watu wa Ruanda wanachukiana kiasi hicho na kuchinjana wenyewe kama kuku unataka Marekani aingilie ya nini kwanza waafrika wanahitaji kujielimisha na kujiheshimu sio kila kitu Marekani
 
Walikuwa wapi Rwanda mpaka wanachinjana ,DRC kukosa amani ,mauaji ya kutisha vita vya Bosnia mpaka kambi ya wakimbizi iliyokuwa chini ya UN kupigwa bomu na kuua innocent civilians ? tena baada ya tension ya Bosnia kuwa kubwa na mauaji ya kutisha Bill Clinton akajitokeza kupatanisha wakati damu nyingi zishamwagika.
Genocide ya rwanda ilitemdeka ndani ya siku 90 na inakadiriwa kuwa watu zaidi ya laki moja walipoteza maisha .yani ilikuwa ni wastani mauaji ya watu 1000 kwa siku!!
Bill clinton alikuwa busy na chechnya katika enzi zile ambazo taarifa zilikuwa zinachelewa sana kufika azingeweza kuwahi kupambana na mauaji yale.
 
Back
Top Bottom