Hivi nyie mnaifahamu familia ya Nyerere au mpo hapa kuchangamsha genge? Familia ya Nyerere haina shida na kamwe haitakuja kuwa na shida. Hao watoto wanapiga kelele kwa shida moja tu ya kutaka kusikilizwa na sio shida ya njaa ya hela. Mwanao unaweza kumpa kila kitu lakini akikuita 'baba! Baba!" alafu ukampotezea utakuwa umemuumiza sana na kumnyanyasa kisaikolojia. Watoto wa Nyerere wanataka kila wakikohoa watetemekewe kitu ambacho hakiwezekani. Kuhusu kufanikiwa, Nyerere amefanikiwa sana na ataendelea kufanikiwa na kuenziwa vizazi hadi vizazi pindi nchi idumupo! Legacy yake inaishi katika nyanja zote kisiasa, kielimu, kiuchumi, kiungozi, kiuzalendo, nk. Hakutatokea mtu nchi hii akashika dola hasipotembelea nyota ya Nyerere!