Dunia ina Umri gani? Mabillioni, Mamillioni, Malaki au Maelfu?

Dunia ina Umri gani? Mabillioni, Mamillioni, Malaki au Maelfu?

Biblia iko sahihi kabisa kuhusu maelezo yake. Watu ndio wapo kimakosa katika tafsiri zao. Biblia haijawahi sema kuwa dunia ina miaka kama elfu sita kuja saba kwa sasa ila miaka hiyo ni ya kuanzia Adamu.
Lakini kabla ya Adamu kuumbwa kulikuwa na miaka mingi huko nyuma ya kuumbwa kwa ulimwengu ikiwepo na dunia ndani. Yawezekana ni mamilioni au mabilioni ya miaka, maana maandiko yanasema kwamba "hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi" ,nukta; sasa baada ya kuziumba mbingu na nchi haijulikani alikaa mdagani kabla ya Roho wa Mungu kutulia sasa katika uso wa maji aliyoyaumba hapo kwanza na kuanza kuikarabati kwa ajili ya kuuweka uhai juu yake. Hapo ndipo sasa anatenga maji na nchi kavu na kisha kuweka viumbe hai.
Pia ijulikane kuwa mtu wa mwili wa nyama, yaani Adamu ndie kiumbe wa mwisho kuumbwa. Kwa wale wa nadharia ya uumbaji wa Mungu kuwa katika siku saba kwa mfano uliopo wa siku saba za juma za kawaida ya binadamu ndio kabsaa hawawezi kamwe kuupata uumbaji jinsi ulivyokuwa kwa kina.
Wewe umesema neno achana na hawa wababaishaji na maswali yao yaleyale kila siku Mungu ni Amin na Hakika. Na ukisikia Mungu kaumba siku 7 haimanishi Alianza j,mos na kumaliza Ijumaa ila ni jumla ya siku saba alimaliza Uumbaji
 
Huu ni mtihani mwingine. Ila cha msingi ni lazima tujue kuwa;
1. Shetani yupo
2. Shetani anapingana na Mungu
3. Shetani ana nguvu na akili nyingi sana.

Kutokana na hayo, ni rahisi kwa shetani kulazimisha wanasayansi waongee wanachoongea, au kubadilisha ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Maswali yapo mengi mnoooo tena mno, lakini hayana majibu. Kukosa majibu hakumaanishi kuwa Mungu hayupo au uumbaji siyo sahihi.

Mimi ninaamini uumbaji kwa kuwa ni neno la Mungu lilioandika.
kama wanasayansi ni wabaya hivo ukiumwa unaenda wapi, kanisani au hospitali
 
Kitabu cha Mwanzo, nadhani ndicho kitabu kibovu kabisa kwenye Bible.

Hakina logic, ni contradiction mwanzo mwisho.

Kitabu cha mwanzo kinasema kwamba watu waliumbwa baada ya kuumbwa kwa mimea na wanyama,wanyama waliumbwa[Mwa.1:11-24], kisha watu mke na mume wakaumbwa kwa pamoja [Mwa.1:26-31]
Yaani kwenye hizoo nukuu, Mungu aliumba wanyama na mimea halafu watu wakawa wa mwisho kuumbwa.Kwenye hizo nukuu, Bibilia inasema mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa wakati mmoja.

Sehemu nyingine ya kitabu cha Mwanzo inaeleza kwamba mtu aliumbwa kabla ya kuumbwa kwa wanyama.
Kitabu kinasema Mungu almuumba Adam kwanza[Mwa.2:7], halafu mimea ikaoteshwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:8-9].....Halafu wanyama wakaumbwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:18-19]

Halafu Eva akaumbwa mwishoni baada ya kuumbwa kwa Adam, mimea na wanyama[Mwa.2:21-23]

Hivi kweli kitabu chenye mikanganyiko kama hii unaweza kukitumia kama njia ya kujifunza chanzo cha uhai?
Tatizo lako unasoma biblia kaa novo
 
Hapa waliotuangusha ni wale wanafunzi wa Yesu,kwa sababu miongoni mwao kwa mujibu wa kitabu cha kikristu Biblia,walikuwa wasomi na mmoja wao ni Marko. Hawa walipaswa kumuuliza haya maswali na majibu ya Yesu yangesaidia sana leo.

Kwa hali ilivyo hivi sasa,Biblia na vitabu vingine vya Dini,haviaminiki tena. Na ni vigumu sana kuamini uwepo wa Mungu. Nadhani hii dhana ya uwepo wa Mungu ilikuwa mbinu tu ya watu kupiga hela!!
 
Hapa waliotuangusha ni wale wanafunzi wa Yesu,kwa sababu miongoni mwao kwa mujibu wa kitabu cha kikristu Biblia,walikuwa wasomi na mmoja wao ni Marko. Hawa walipaswa kumuuliza haya maswali na majibu ya Yesu yangesaidia sana leo.

Kwa hali ilivyo hivi sasa,Biblia na vitabu vingine vya Dini,haviaminiki tena. Na ni vigumu sana kuamini uwepo wa Mungu. Nadhani hii dhana ya uwepo wa Mungu ilikuwa mbinu tu ya watu kupiga hela!!
Sema wewe ndo huamini na si kosa lako maana hukuumbwa kuamini ila walioumbwa kuamini ni wengi na wanaongezeka katika jamii ya waaminio kila uchwao.
"Kondoo zangu huisikia sauti yangu" nae kila aisikiae sauti ya mchungaji (Yesu) huitika . Na ni kwa wakati uliokusudiwa kwake yeye aitwae.
Back to topic ni kwamba biblia iko clear na imeweka kila kitu wazi katika uumbaji hasa kitabu cha mwanzo. Kuna uumbaji wa roho katika mwanzo moja ukidhihirishwa katika mwili mwanzo mbili. Na kuna tofauti ya mamilioni kama sii mabilioni ya miaka katika umbaji hizi.
Kibaya zaidi katika ulimwengu wa kisayansi hawajui chochote kuuhusu huu ulimwengu wa roho. Wameishia tu kwa umbali mno kuwa na picha ya jicho la kisayansi katika sehemu ndogo sana kwenye hili eneo la allies na hata hivyo hawana maelezo ya kina juu ya hivi viumbe zaidi ya kuvibatiza jina la phenomena lisilo na maelezo zaidi.
 
Kuhusu hili kila upande una limited knowledge. Creationism hawaendi mbali kabisa, Wanasayansi wanaenda mbali lakini hawafiki mwisho. Ila ipo siku ukweli utajulikana.
 
1. Hata kama dunia ni older for 1000 years haitabatilisha theory ya evolution kwa sababu Evolution haina uhusiano sana na mabilioni bali inahusiana na mabadiliko ya kiumbe kutoka hatua moja kwenda nyingine.

2. Dunia inaweza kuwa old to 3billions na kuendelea lakini bado haimaanishi creation ni wrong. Who knows kama neno siku ni 24 hours? What if its a long period of time? Who knows!

Dating sio part ya evolution bali ni part inayojaribu kupima validity ya evolution.

I want you to tell you what I see here. You are resisting an idea rather than facing it. Usipoteze wakati kutaka kukataa idea bali isome na ichunguze zaidi na sio kukimbilia kuipinga au kuilinganisha na unachotaka kuelewa.

Sky is not the limit, The Mind is the limit.
 
Evolution pia inaweza kuwepo ndani ya Creation myth. Kama uhalisia kuwa creationist mnaamini kuwa Mungu alimuumba mwanadamu na akabadilika kuwa Africans, Indians, White n.k kutokana na mazingira na adaptation hapo tayari theory ya mageuzi imeshirikishwa katika maelekezo.



Tuache kukariri wrongly kuona evolution ni nyani kuwa mwanadamu tu, au mabillion ya miaka au inapinga creation au theory ya kishetani. Hizo ni limited delusions za jamii inayotaka kuelewa itakavyo.

Evolution kwa kifupi ina maana ya MAGEUZI. Kuwa viumbe havina appearance ya moja kwa moja bali hubadilika.

Tukiiweka hii theory simply na short ndipo mtaelewa kuwa its a logical argument na sio kelele.
 
Mimi moja kwa moja napingana na CREATIONISM kwa maana haina mantiki.Nasema haina mantiki kwa sababu inatuachia maswali yasiyo na majibu na kutulazimisha tuiamini badala ya kuielewa.Mimi nina maswali yafuatayo kuhusu CREATIONISM.

1.Kama watu wote walitokea sehemu moja(mf.Mashariki ya kati), ni technologia ipi iliyotumika kusambaza watu kutoka mashariki ya kati kwenda maeneo mbalimbalina ya Dunia kama Chile, Madagascar n.k?
walivukaje bahari? Kama walisafiri, kwa nini wasingekuwa wanawasiliana kwa safari za mara kwa mara? Kwa nini kina V.Da Gama, C.Columbus wawe wagunduzi wa maeneo mengine? ina maana waliamini Dunia ni maeneo walimoishi pekee?

2.Kama tumetokana na Baba na Mama mmoja, kwa nini watu tunatofautiana sana? nini sababu na mechanism iliyosababisha wawepo watu weupe na weusi? Miaka 6000 inatosha kuruhusu mabadiliko makubwa tunanoyashuhudia ya tofauti miongoni mwa jamii za watu wa hii Dunia?

3.Kwa nini kuna mabaki ya kale yenye umri zaidi ya miaka milioni? kwa nini hayo mabaki hayapatikani nje ya Africa? Kwa nini fossils zinaonesha 'Life complexity' inaongezeka kutoka matabaka ya chini kuja matabaka ya juu ya miamba?

4.Kwa kuwa Watu waliumbwa kutokana na udongo, ni material yepi yaliyotumika kuumba viumbe wengine kama wanyama na mimea? Mbona watu wanafanana sana na hawa viumbe wengine?

5.Ukowapi ushahidi/mabaki ya bustani ya Eden, masalia/makaburi ya Adam na Eva?
Yako wapi masalia ya safina ya Nuhu? Mbona Palaeontology haioneshi kama mafuriko ya Dunia nzima yamewahi kutokea na kuua watu?

6.Kwa nini vitabu vya dini havizungumzii uwepo wa sayari nyingine?, Kama hizo Sayari ziliumbwa na Mungu, ni za kazi gani?

7.Kama Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu, kwa nini aumbe viumbe hatarishi kwa watu wake kama vile; Virus, bacteria na Fungus wenye kusababisha magonjwa na vifo kwa watu? Mungu mwenye upendo wote anaweza kuumba vyanzo vya matatizo kwa watu wake?

8.Kwa nini miili ya viumbe vya Mungu iwe na vestigial organs?

9.Kwa nini Mungu aumbe Dunia yenye majanga asilia kama matetemeko ya nchi, mafuriko, vimbunga na milipuko ya volcano? Intelligent designer anaweza kuumba dunia yenye majanga kama hii ya kwetu?

10.Kwa nini Mungu alisikitika na kuhuzunika baada ya kumuumba Binadamu(Mwa.6:5-8)? Mungu gani mjuzi wa yote afanye jambo la kumsikitisha na kumhuzunisha siku za mbeleni?
Hivi umeelewa mada kweli wewe?

Mada haizungumzii kupinga chochote bali wewe sema unakubaliana na kitu gani....
 
Napingana na Bible, maana utafiti wake hauna mantiki na umejikita zaidi kwenye kuamini(imani)

Imani iko 50/50, inaweza ikawa kweli au isiwe hivyo basi bible inaongopa.

Big Bang imetokea kati ya miaka billion 12 mpaka 14
Iliyopita. To put this in perspective, the Solar System is thought to be 4.5 billion years old and humans
have existed as a genus for only a few million years. Astronomers estimate the age of the universe
in two ways:
1) by looking for the oldest stars; and
2) by measuring the rate of expansion of the
universe and extrapolating back to the Big Bang; just as crime detectives can trace the origin of a
bullet from the holes in a wall.
Unapingana na Biblia halafu mada inakutaka useme wewe unakubaliana na kitu kipi au dhana ipi juu ya umri wa dunia,hujioni wewe wa ajabu?
 
Kitabu cha Mwanzo, nadhani ndicho kitabu kibovu kabisa kwenye Bible.

Hakina logic, ni contradiction mwanzo mwisho.

Kitabu cha mwanzo kinasema kwamba watu waliumbwa baada ya kuumbwa kwa mimea na wanyama,wanyama waliumbwa[Mwa.1:11-24], kisha watu mke na mume wakaumbwa kwa pamoja [Mwa.1:26-31]
Yaani kwenye hizoo nukuu, Mungu aliumba wanyama na mimea halafu watu wakawa wa mwisho kuumbwa.Kwenye hizo nukuu, Bibilia inasema mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa wakati mmoja.

Sehemu nyingine ya kitabu cha Mwanzo inaeleza kwamba mtu aliumbwa kabla ya kuumbwa kwa wanyama.
Kitabu kinasema Mungu almuumba Adam kwanza[Mwa.2:7], halafu mimea ikaoteshwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:8-9].....Halafu wanyama wakaumbwa baada ya kuumbwa kwa Adamu[Mwa.2:18-19]

Halafu Eva akaumbwa mwishoni baada ya kuumbwa kwa Adam, mimea na wanyama[Mwa.2:21-23]

Hivi kweli kitabu chenye mikanganyiko kama hii unaweza kukitumia kama njia ya kujifunza chanzo cha uhai?
Una hasira sana na Biblia siyo?

Anzisha thread yako utapata majibu huko....
 
Mada hii nakumbuka niliianzisha ktk group la shule lakn waliipotezea.

Mimi naamini Evolutionists kwa sababu. Natamani sana nitoe sababu ya kuamini
 
Unapingana na Biblia halafu mada inakutaka useme wewe unakubaliana na kitu kipi au dhana ipi juu ya umri wa dunia,hujioni wewe wa ajabu?
hivi unajielewa kweli wewe?
kupitia hayo maelezo yangu hapo juu nadhani umeshatambua nko upande gani.

ficha uppumbavu wako, kabla hujaanza kuharisha
 
Unapingana na Biblia halafu mada inakutaka useme wewe unakubaliana na kitu kipi au dhana ipi juu ya umri wa dunia,hujioni wewe wa ajabu?
hivi unajielewa kweli wewe?
kupitia hayo maelezo yangu hapo juu nadhani umeshatambua nko upande gani.

ficha uppumbavu wako, kabla hujaanza kuharisha
 
hoe-oud-de-aarde.jpg

???????

Swali hili ni Muhimu sana hasa dunia ya leo maana limeigawa katika vipande viwili ambavyo havina ukaribu wala ufanano hata chembe.

1:Wanaoamini Dunia iliumbwa(Creationists) - Dunia ina umri wa miaka takribani 6000 (maelfu).Pia kunadhana ndogondogo zinazoendana na hii.

2:Wanaoamini Dunia iliibuka (Evolutionists) - Dunia iliibuka Takribani miaka Bilioni 4.6 na maisha kuanza miaka Billioni 3.5 iliyopita.Pia kuna dhana takribani saba za uibukaji.

Haya ndio Matokeo ya Hii mitazamo miwili.
1: Kama dunia ni changa (Miaka kama 6000) Basi Dhana ya uibukaji EVOLUTION inakufa hapohapo. Somo kwamba tulitokana na Sokwe linafia hapo hapo.​

2: Kama Dunia imezeeka na inaumri wa miaka Billioni 4.6 basi, Dunia haikuumbwa na chochote kuhusu uumbaji ni stori zisizo sawa. Na ikumbukwe bila tukio hili ktuokea kwa mabillioni ya miaka tena kidogo kidogo hii dhana inakufa rasmi.
Vipimo Vya miaka.
1: EVOLUTION; Hapa wanatumia Carbon dating au Radiometric Dating (Ni njia ambazo ili zifanye kazi inabidi ujumuishe na MAKISIO/ASSUMPTIONS), Yawezekana kuna mengi zaidi pia.

2:CREATION; Hapa inatumika Umri wa watu hasa waliozaliwa baada ya adam,Historia,Utafiti na nyaraka za kale na kwenda hadi kufika leo tulipo.Yawezekana kuna mengi zaidi pia

Karibuni kwa changamoto fikirishi,
always am a Winner Kiranga gasgas Nyani Ngabu CHARMILTON tejateja Apollo Iceman 3D UHURU JR Kikwajuni One Behaviourist Stefano Mtangoo Hb wa Ilala Kahtan Ahmed Vivax Warrior faiz MALCOM LUMUMBA na wengine wengi...

Dondosha hapa chochote unachoamini au kujua kuhusu haya mawili. Ninaamini hakuna ambaye yuko pande zote mbili kwani hazichangamani.

Ukitoa na reference, illustrations, Quotes, links, chochote kile Kumtetea Adam au Homosapiens na makazi yake tutashukuru
Nakurekebisha hapo hapo...! Binadamu hajatokana na sokwe..! Rekebisha kwanza hapo
 
Nakurekebisha hapo hapo...! Binadamu hajatokana na sokwe..! Rekebisha kwanza hapo
Chagua
Cell, bakteria, samaki, homo habils etc ni suala la muda gani tu. Mimi mtazamo wangu ni uumbaji nitaeleza kwa nini sio evolution. Na kwa nini naamini evolution ni suala la kidini au imani na sio sayansi kama Dunia inavyoaminishwa
 

Attachments

  • ourfacefish2man.jpg
    ourfacefish2man.jpg
    18.7 KB · Views: 58
Back
Top Bottom