Tetesi: Dunia inaenda kuungana dhidi ya Urusi

Urusi anajitetea dhiddi ya mpango ovu wa USA na kila mtu anajua alichokifanya Russia ni kwa mjibu wa sheria chini ya Article 51 of the United Nations Convention. Save, kwa viazi mbatata vichache.
Kwanini aivamie Ukraine na sio USA mwenye nia ovu?
 
Israel baada ya kuona vidrone vya iran vinavyojambisha ukraine naye amepanic analiunga soon patamu hapo.
 
Haitakiwi kuwa na double standard! Kama jambo fulani si sawa basi iwe si sawa kwa wote.

Wewe uliona si sawa Marekani kuvamia Iraq, kwa nini uone sawa Urusi kuvamia Ukraine?
Kama kisingizio ni kujenga military base basi hata Marekani ni sawa ikiweka kisingizio kuwa Saddam alikuwa anakusanya silaha za nyukilia ili kuidhuru Marekani!

Kama ukitaka haki simama kwenye haki, hakuna sababu yeyote inayohalalisha nchi moja kuvamia na kushambulia kijeshi nchi nyingine, na wala hakuna mwenye haki ya kuipangia nchi nyingine ijiunge na umoja gani.

Watu wengi wanaoshabikia Urusi hawasimami kwenye haki, bali wanasukumwa na chuki waliyonayo juu ya Marekani, wanaamini Urusi ikiishambulia Ukraine anayepata hasara ni Marekani...

Bahati Mbaya kabisa ni kwamba Putin kapiga hesabu vibaya, vita imemuelemea na anaweza kunyang'anywa hata eneo alilopora mwaka 2014 la Crimea. Kutishia kutumia nyukilia ni kama vile kutishia kujamba ilihali unaharisha...!

Carbon copy to my lovely sister, Dada Nyamizi
 
duh kuna watu ni vichaa , kupandikiza rais puppet Ukraine ni sahihi ? Au ndo Urusi alikuwaa anajilinda kwa kupandikiza rais kibendera ndan ya Urusi ? Je kupora Crimea napo pia ni kujilinda ? je kupandikiza waasi kwenye nchi ya jiran ni kujilinda pia ? tuambie viashiria vya kusema Ukraine ilikuwa inatumika kuiangusha Urusi , yaan USA aache kuwatumia washirika wa NATO aje aitumie nchi nje ya NATO , hv ukichaa huu mtaacha lin ? hv Urusi asingepora Crimea na kupandikiza waasi majimbo ya mashariki , Je Ukraine wangefukiria lin kutaka kujiunga na NATO ? ukute ww ni mtu mzima na una akil km kimah , ushabiki unakufanya mwendawazimu , Mpk sasa licha ya Ukraine kuharibiwq nchi yao ila wao hawaja rusha hata jiwe ndan ya Urusi
 
una ushaidi kututhibitmishia USA aliingilia siasa za UKRAINE mwaka 2014 , km huna bas jiite shogah mzee bila kumung'unya maneno , Uhuru wa kuongea unawafanya mnalopoka
 
They got money for wars, but can't feed the poor.
warusi sio ? maana ndo vinara wa vita , hatujawai wasikia kweny3 technology wakitunishiana na wakubwq wengine , wao utawasikia mara wapo syria na mikopo yao mara venezuela mara chen chen
 
Mbona Iddi Amin alianza kuipiga Tanzania bila sababu?
Mbona Saddam Hussein alianza kuipiga Kuwait bila sababu?
Mbona Stalin alianza kuipiga Finland bila sababu?
Huyu G tax hajui kuwa waimla wakilewa madaraka wanaweza kukupiga tu ili kuonyesha umwamba, hukumsikia mtoto wa Museveni alisema kuichukua Nairobia ndani ya wiki 2? Putin alisema Ukraine itakuwa jivu ndani ya siku 3. Huu ni ulevi wa madaraka...

Kumbuka Putin ana miaka mingi sana madarakani, ameshalewa madaraka, ila ulevi wake uko karibu kumtokea puani.. umeelewa G'taxi ? Na ndugu yako Bwana Utam
 
At least unaanza kuelewa, historia kifupi hawa USA waliiogopa iliyokuwa USSR Sana kwa umoja wao na nguvu zao za kiuchumi na kijeshi na siasa zao za kivomunisti na TATHIMINI baada ya vita pili ya dunia Urusi ilidhihilika ina nguvu kubwa kijeshi na USA kuona hivyo akaamua kushawishi washirka ndani ya ulaya na kuwaambia huyo jirani enu ni hatari hamko salama hivyo tuungane tuwe na umoja wa kusaidiana kiuchumi na kujilinda kijeshi pia siasa za baadhi ya nchi za ulaya na malekani ni za kibepari hivyo wakaanza umoja ukiwa na nchi 15, na moja ya makubaliano yao nchi yeyote akiingia memba, nato na marekani Wana haki ya kuweka base ya kijeshi, mrusi akaona hatari watu ambao maadui kiuchumi kijeshi kuendelea kumkaribia kimipaka nae akachukua hatua ya kmshawishi Rafiki yake Fidel kastro wa Cuba ambaye jirani Sana wa marekani naye akajenga military base cuba. USA AKAPINGA NA KULIA KWA NGUVU ZOTE KWAMBA HAIKUBALIKI AKASEMA NI HERI AINGIE VITA YA TATU YA DUNIA KULIKO URUSI KUWA NA KAMBI YA KIJESHI CUBA, Hawa ni wakibwa wakakaa na kuingia makubaliano ambayo yaiitaka Urusi kuvunja hiyo kambi 1962 na MAREKANI NA NATO YAKE WASIENDELEE KUSAJILI NCHI ZA ULAYA KUELEKEA UPANDE WA URUSI KUJIUNGA NA UMOJA WA KIVITA WAO HUO WA NATO lakini hata baada ya hiyo mikataba NATO na marekani waliendelea kuvunja mikataba na kumkaribia Russia na chokochoko tele, Russia ilifikia mahali akaweka ulmantum kwamba jamani Sasa imekuwa too much walipoanza mipango mikubwa na Ukraine kwa kupandikiza na kuanzisha shughuli zao za muda mrefu against Russia ndani ya Ukraine, RUSSIA HALIKUWA HANA NAMNA ZAIDI YA HATUA ANAZOCHUKUA, JIRANI YAKE HANA ADABU ANASHIRIKIANA NA MAADUI ZAKE,ANAKARIBISHA MAJAMBAZI ILI SIKU MOJA WAMVAMIE JIRANI YAKE,SASA UTAFANYAJE, NI KUANZA NA JIRANI MSHENZI HUYUHUYU, ILI WANAOKARIBISHWA WAONE
 
Mkuu uko nondo sana, wengi wanaamini porojo za America na western media. Hawajui chimbuko la mzozo. Marekani ni mnafiki sana
 
Mkuu uko nondo sana, wengi wanaamini porojo za America na western media. Hawajui chimbuko la mzozo. Marekani ni mnafiki sana
western media hawapendi watu wajue ukweli, urusi hukosoa mabaya ya marekani sana lakini bila propaganda ni wenye hekima sana, hata marekani anapotokea kuvamia nchi zingine huwa wanakosoa straight bila uoga. marekani hataki urusi awe na nguvu za kiuchumi na kijeshi, hivyo hivyo kwa china ameenda kufanya ushirika na ndugu wa kihistoria wa china ambaye ni Taiwani , kenda kuwafarakanisha na yeye kaweka mifumo yake kijeshi pale kwa maslahi yake, mtu na ndugu yake ugomvi hauishi, china kataka kumwadhibu taiwani yeye kasema nitaingilia, same tu ukraine na russia
 
Ndugu yangu
Andiko lako umeliandika ukiangazia upande mmoja nanhaujaweza kubalansi ukweli.

Hii vita imechochewa na NATO chini ya Marekani.

Ni vyema dunia ikagomea kusimama na Urusi ama NATO kwenye hii vita. We need to stand and speak for HUMANITY
 
Unaamini kua anachofanya Putin na Russia ni ujinga? Hujui kwamba unaweza kua mjinga wewe? Hivi sasa tunaweza sisi kama Tanzania ghafla tu tukaanza kuipiga Burundi bila sababu?
Mkuu

Hujui Burundi na Rwanda ni sehemu ya Tanganyika na utawala wa nchi hizi unategemea Baraka kutoka kwetu!!?

Kama wakienda kinyume sisi lazima tuwanyooshe maana Hao ni Watoto wetu!!
 
Kweli mkuu

Wanalipua jengo maksudi kama world trade center Halafu wanasingizia watu fulani wanawakamata na kuwatesa sana!halafu huwaachia KWA kusema walikosea hawana hatia !Baada ya hapo huwafuata kisiri na kuwashawishi wqjiunge na magaidi FULANI ya mchongo Ili kulipa kisasi chao!KWA sababu ya maumivu makali ya mwili, Roho na hisia basi hujiunga na KUWA magaidi!!

Halafu wanaendelea kuwatumikisha kuwapiga wapinzani wao au ku destabilize uchumi wa nchi FULANI ambao WANAENDA ki nyume na Sera zao!!
 
Sasa huku ni kukashifu dini za watu ni jambo baya usilete udini kwenye mada hii,kama umeshindwa hoja bora ukae kimya kuliko kuleta ujinga wa kushifu udini za watu kama huwezi kuwa great thinker basi usiwe great sinker
No, sijakashifu dini mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…