Haitakiwi kuwa na double standard! Kama jambo fulani si sawa basi iwe si sawa kwa wote.
Wewe uliona si sawa Marekani kuvamia Iraq, kwa nini uone sawa Urusi kuvamia Ukraine?
Kama kisingizio ni kujenga military base basi hata Marekani ni sawa ikiweka kisingizio kuwa Saddam alikuwa anakusanya silaha za nyukilia ili kuidhuru Marekani!
Kama ukitaka haki simama kwenye haki, hakuna sababu yeyote inayohalalisha nchi moja kuvamia na kushambulia kijeshi nchi nyingine, na wala hakuna mwenye haki ya kuipangia nchi nyingine ijiunge na umoja gani.
Watu wengi wanaoshabikia Urusi hawasimami kwenye haki, bali wanasukumwa na chuki waliyonayo juu ya Marekani, wanaamini Urusi ikiishambulia Ukraine anayepata hasara ni Marekani...
Bahati Mbaya kabisa ni kwamba Putin kapiga hesabu vibaya, vita imemuelemea na anaweza kunyang'anywa hata eneo alilopora mwaka 2014 la Crimea. Kutishia kutumia nyukilia ni kama vile kutishia kujamba ilihali unaharisha...!
Carbon copy to my lovely sister, Dada
Nyamizi