Dunia ni mortgage: Nadharia hii kuhusu sababu ya binadamu kuletwa duniani inafikirisha sana

Dunia ni mortgage: Nadharia hii kuhusu sababu ya binadamu kuletwa duniani inafikirisha sana

Cosmology is the study of the universe; its birth, evolution, and ultimate fate. This includes further developing and refining the prevailing model, the Big Bang theory, investigating the universe's rate of expansion, and measuring radiation left over from the Big Bang, the so-called cosmic microwave background. yawezekan haipo sawa 100% lakin mungu siku moja anampongeza mtu apa for good try.

Nchi fulani mwanasayansi mmoja ametengeneza coiled drumg zinazo zunguka kwa spend kubwa sana kuna element ameziweka ndani zitengeneze mlipuko kama wa big bang theaory coz walitega vinasa sauti kutoka kwenye space ya mbali sana kipindi cha nyuma walisikia sauti flani ambayo inafanana na sauti inayo toka kwenye hii cioled drum ya sasa.
maana yake there is a place where is the heart of the universe and its active up to today explosion never end, expand more and more and more. nimeandika kwa uchache coz siikumbuki vizur nilisoma muda kidogo
 
theory yako ikideal na binadam tu tayari ni very wrong theory very wrong. good theory lazima iweze kuelezea kilakitu. the theory of evething
 
nadharia ya ovyoo sanaa hii.logically haiko sawa kabixaaa. unachanganya mambo sana. kwamba dunia intakuwa mbingu baada ya kupewa hatimiliki unasahau kwamba mbingu si physical upewe hati milik ya kuishi milele na iyo miili ya udongoo nop haikai hata kidogo.

Dimensions,portal, quantum cosmos,matrix, sacred geometry hivi ndo vitu vya kuingiza hapa sasa.
Mbingu Ni mfumo. It is not a physical place. Ni mfumo Mpya wa utawala..
 
theory yako ikideal na binadam tu tayari ni very wrong theory very wrong. good theory lazima iweze kuelezea kilakitu. the theory of evething
Nimesema Dunia Ni nyumba YENYE Kila kitu ( furnished) ambayo imekuwa mortgaged Kwa binadamu..Hivyo vitu vingine kama Wanyama, mimea etc Ni furniture's Na mapambo
 
Kila binadamu anae zaliwa anazaliwa akiwa Na FINGER PRINTS zake yeye mwenyewe. Hakuna binadamu anae zaliwa Na finger prints zinazo fanana Na finger prints ZA binadamu mwingine hata kama wamezaliwa mapacha.


Sio kweli, wapo mapacha wanafanana mpaka finger print fuatilia uthibitishe mwenyewe.

Kuna story amaizing juu ya pacha wanaaofanana ambapo moja aliiba vito, wakamdaba akasema sio yeye ikabidi aachiwe cuz ilishindikana kuwatofautisha
 
 
Mafundisho ya uislamu,ukristo Na uyahudi KUHUSU chanzo Na Sababu ya binadamu kuwepo katika sayari ya Dunia wote mnayajua so sipo hapa Kwa ajili ya kuyarudia..

Nipo hapa Kwa ajili ya kuelezea Nadharia KUHUSU chanzo Na Sababu ya Maisha ya binadamu ulimwenguni ambazo zilitolewa Na watu walio fikiri nje ya vitabu vya Dini hizo tatu.

Kwa ufupi Dini inapo mzungumzia Mungu Na chanzo cha Maisha katika sayari ya Dunia huwa inaanzia from the conclusion wakati philosophy Na science ina move toward the conclusion.

Relgion = from the conclusion

Philosophy and Science= Toward the conclusion.

Watu wa science wakifikia hatua ya kumjua Mungu basi watakuwa wamemjua Mungu kwelikweli Kwa Sababu watakuwa wamemtafuta mpaka wamempata. Nyakati hizo zikifika Dunia itageuka Na kuwa mbingu Kwa Sababu maswali yote magumu katika USO wa Dunia yatakuwa Na majibu yake.

Watu wa Dini wamefeli kuyafanya Maisha ya Duniani kuwa kama mbinguni Kwa Sababu wao tayari Wana assume kwamba wanamjua Mungu Kwa hiyo mtazamo WA mafundisho yao unaanzia kwenye conclusion ( kwamba wanamjua Mungu) Hatari ya Jambo hili Ni kwamba Kuna uwezekano mkubwa Sana watu wa Dini wakawa wanatoa maelekezo kutoka kwenye fikra zao wenyewe huku waki assume kwamba yanatoka Kwa Mungu.

Ndio maana Dini ndio zimekuwa chanzo cha matatizo mengi makubwa ulimwenguni..

BACK TO MY POINT

"DUNIA NI MORTGAGE" NI NADHARIA KUHUSU CHANZO NA SABABU YA BINADAMU KUWEPO DUNIANI AMBAYO INAFIKIRISHA SANA...

Nadharia HII inasema kwamba hili gimba linalo Elea angani ambalo linajulikana kama sayari ya Dunia Ni a mortgaged property ambayo Mwenyezi Mungu ametupangisha Sisi wanadamu Kwa consideration maalumu . Tukifanikiwa kukamilisha Deni tunalo Daiwa basi tutapewa rasmi kuimiliki sayari ya Dunia milele Na tutaishi DUNIANI milele kama mbinguni..

Ngoja nitumie mfano rahisi...

Ni hivi: Serikali imejenga nyumba kigamboni. Gharama ya nyumba Ni shilingi milioni Mia Moja Na ishirini. Nyumba imekamilika Ina Kila kitu ndani.

Serikali inakuuzia wewe nyumba hiyo Kwa mkopo.

Utaingia Na kuruhusiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo bure Kwa makubaliano kwamba utakuwa unalipa shilingi milioni Kumi Kila mwezi.

Baada ya miezi Kumi Na mbili ukisha kamilisha Deni lako basi rasmi utapewa hati ya nyumba Na wewe utakuwa ndio mmiliki halali WA hiyo nyumba.

Ukisha kuwa mmiliki halali WA hiyo nyumba utakuwa Sasa Na uhuru wa kufanya chochote juu ya hiyo nyumba Kwa kuwa Sasa utakuwa mmiliki halali mwenye mamlaka kamili juu ya hiyo nyumba.

Hivi ndivyo ilivyo Kwa sayari ya dunia, Mungu Na wanadamu Kwa Mujibu wa nadharia hiyo..

NI HIVI

Mungu ameitengeneza sayari yetu ya Dunia Na ndani yake akaweka Kila kitu ( fully furnished )

Kisha akaitoa mkopo sayari hiyo kwetu Sisi wanadamu ili tupate kuimiliki ..

Ili tuweze kuimiliki sayari HII tunatakiwa kulipa gharama alizo tumia Mwenyezi Mungu kuitengeneza sayari HII ya Dunia Na vitu vyote vilivyomo ndani yake ikiwa Ni pamoja Na MIILI yetu ambayo raw materials zake zilitoka hapa hapa duniani( kumbuka Sisi Ni roho ambao tunaishi kwenye miili)

Tukisha maliza kulipa Deni ( gharama) alizo tumia Mwenyezi Mungu kuitengeneza sayari yetu basi Mungu atatupa funguo ( hati miliki) ZA kuitawala Dunia.

Tukisha fikia levo ya kumiliki funguo ZA kuitawala Dunia basi Mungu atashusha mbingu ( mfumo) Mpya duniani. Hakutakuwa na vifo, MAGONJWA , vita nakadhalika.

Kwa ufupi Dunia itakuwa Firdaus/Pepo/mbingu


JE NI NINI GHARAMA ALIZO TUMIA MWENYEZI MUNGU KUITENGENEZA DUNIA?

NI UPENDO. God created the world out of pure love. Kwa hiyo currency pekee ambayo Mungu anaitambua Ni " UPENDO". Hii ndio currency ambayo unaweza kuitumia kununua kitu chochote kutoka Kwa Mungu.

UPENDO NI NINI? UPENDO NI KUMPENDA BINADAMU MWENZAKO KAMA UNAVYO IPENDA NAFSI YAKO.. kama alivyo SEMA Yesu Masiha.

Binadamu tukifikia levo HII ya kuwa na UPENDO wa kiwango hiki ambao Ni collectively Dunia nzima basi tutakuwa tumelipa Deni letu Kwa Mungu Na Mungu hatokuwa Na Sababu ya kutokutupa hatimiliki( funguo) ZA kuitawala Dunia.

( UPENDO Huu utatakiwa kuwa collectively Yani watu wote dunia nzima kila MTU ampende mwenzake kama anavyo jipenda yeye mwenyewe ndani ya NAFSI yake)

Ni levo ya UPENDO ambayo mkristo atapenda muislamu kama anavyo jipenda yeye and vice versa.

Mzungu atampenda mwafrika, mchina,mwarabu,muhindi,myahudi etc and vice versa kama anavyo jipenda yeye mwenyewe.

Myahudi atampenda mpalestina and vice versa kama anavyo jipenda yeye mwenyewe.

Kila binadamu atampenda binadamu mwenzake kama.anavyo jipenda yeye mwenyewe Na atamtendea wema kama anavyo taka.kutendewa yeye mwenyewe..

Tukifikia levo HII basi Mungu wa Mbinguni atatupa funguo ZA kuitawala Dunia Na hakutakuwa Na MAGONJWA, vifo , vita Wala chochote kibaya katika Dunia HII..

We will become " PRIMUS INTER PARES WITH THE LORD "

NA HII NDIO SABABU YA TRUE MISSION OF CHRIST JESUS KUJA DUNIANI

Yesu alikuja duniani Kwa ajili ya kutukomboa wanadamu Kwa kutuletea ujumbe Huu kwamba TUWE NA UPENDO..

NI UPENDO PEKEE NDIO UTAKAO MKOMBOA MWANADAMU HAKUNA KINGINE CHOCHOTE...

NIMEZALIWA NA KUKULIA KATIKA UISLAMU LAKINI DHIMA YA KRISTO KWA WANADAMU NINA IELEWA PENGINE KULIKO MA ASKOFU NA WACHUNGAJI WENGI DUNIANI

INAPOSEMWA KUWA NA KRISTO MAANA YAKE NI KUWA NA ROHO YA UPENDO AMBAO NIMEUZUNGUMZIA HAPO JUU. UPENDO AMBAO ULI HUBIRIWA NA YESU MWENYEWE... UNAWEZA KUWA MUISLAMU AU MHINDU AND STILL UKAWA NA KRISTO NDANI YAKO . KRISTO NI UPENDO USIO NI MIPAKA. KUWAPENDA BINADAMU WENZAKO KAMA UNAVYO JIPENDA WEWE.

NDIO MAANA HATA BIBLIA YENYEWE INASEMA KAMA HAUNA UPENDO ( KRISTO) WEWE HUFAI KITU KABISA...


Ndio maana Yesu anasema hatorudi duniani mpaka watu wote wawe wamehubiriwa habari zake . PENGINE alimaanisha mpaka watu wote wawe INCHRISTED"

Ni Kweli kabisa ukiwa Na KRISTO ndani yako hata Lucifer hawezi kukufanya kitu Kwa Sababu katika ulimwengu WA roho nguvu kubwa kuliko zote Ni nguvu ya KRISTO ( UPENDO)

Kwa nguvu ya KRISTO( UPENDO) unaweza ku conquer nguvu zote ZA kiroho hapa duniani...

Ndo maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake ufalme wa Mungu ( KRISTO) umo ndani yenu. Kwamba Mungu ( KRISTO) anaishi ndani yenu Na Zaidi akawaambia utafuteni Kwanza ufalme wake Mungu ( KRISTO/UPENDO) Na mambo mengine yote mtazidishiwa...

Maandiko yanavyo SEMA " HAPO MWANZO KULIKUWA NA NENO NA NENO ALIKUWA KWA MUNGU VITU VYOTE VISINGE FANYIKA PASIPO HUYO NENO..

Huyo NENO Ni KRISTO ( UPENDO) Na kwamba bila Upendo MUNGU ASINGE UMBA CHOCHOTE DUNIANI..

Mungu anaposema huyo Ni mwana wangu mpendwa nilie pendezwa nae anamaanisha KRISTO( UPENDO )

Na Yesu anaposema Mtu haji Kwa baba bila kupitia kwangu Kwanza anamaanisha njia pekee itakayo ku connect Na MUNGU ni UPENDO ( KRISTO)

Hata Yesu anaposema " BABA IKIWA NI KWA MAPENZI YAKO BASI NAOMBA KIKOMBE HIKI KINI EPUKE " lakini Mungu hakumuepusha YESU ( MTU ALIE BEBA ROHO YA KRISTO/ROHO YA UPENDO) Na kikombe hicho tafsiri yake Ni kwamba YESU ALIKUWA ANA MUULIZA MUNGU JE KUNA NJIA NYINGINE YOYOTE ILE AMBAYO WANADAMU WANAWEZA KUKOMBOLEWA KWAYO? MUNGU AKAJIBU KWA VITENDO KWAMBA HAPANA NJIA NYINGINE ISIPOKUWA NJIA YA KRISTO( UPENDO) ndio maana akaruhusu Yesu amwage damu yake pale msalabani.

Tunaposema Yesu Ni Mwana wa Mungu tunamaanisha kwamba Roho ya upendo/KRISTO ni roho kutoka Kwa Mungu ambayo Mungu Ali IPA Hadhi Na kuifanya kuwa mwana wake. Na Yesu anaposema " MIMI NA BABA TU KITU KIMOJA" anamaanisha " MUNGU NA UPENDO NI KITU KIMOJA.MUNGU NI UPENDO NA UPENDO NI MUNGU"

Kwa mtazamo wangu, Mtume Paulo ndio Mwanafunzi wa Kweli wa Yesu . Pamoja Na kwamba Mtume Paulo Hakuwa miongoni mwa wale wanafunzi Kumi Na wawili wa Yesu Wala hakuwahi kukutana Na Yesu physically Bali yeye alijifunza habari za Yesu kupitia wanafunzi wa Yesu lakini yeye ndio Alie muelewa Yesu Ni Nani PENGINE kuliko Mwanafunzi mwingine YOYOTE wa Yesu ISIPOKUWA Petro ambae alimtambua Yesu kuwa KRISTO. Mtume Paulo kwenye kitabu cha Tito 2:13 anamtaja KRISTO KUWA NDIE MUNGU MKUU Na Ni ukweli kabisa MUNGU NDIO UPENDO MKUU UPENDO MKUU KUPITA KITU CHOCHOTE..

Wanaposema YESU NI MUNGU wanamaanisha KRISTO/UPENDO NI MUNGU. NA WANAPOSEMA MUNGU ANA NAFSI TATU WANAMAANISHA MUNGU NI BABA MWENYE ROHO TAKATIFU YENYE UPENDO MKUU.


Mfano IPO Mingi Sana ila Kwa leo inatosha hiyo


JE MTU BINAFSI. HAWEZI KUFIKIA LEVEL YA UPENDO UTAKAO MUWEZESHA KUPEWA FUNGUO ZA KUMILIKI DUNIA?

Jibu Lake Ni NDIO... WaPo watu walio fikia level ZA juu Sana ZA Englightenment kiasi kwamba duniani waliishi Na kuheshimika kama miungu Na kifo hakikuwa Na Sauti YOYOTE kwao. Baadhi ya watu Hao Ni kama BUDHA au hata YESU MWENYEWE ambae mwili wake ulitumika.kubeba roho ya KRISTO.

Je mbona watu Hao walikufa?

Yesu alikufa akafufuka Na mpaka Leo HII bado anaishi ( Yesu Yu Hai) Na BUDHA mpaka leo HII bado anaishi katika mioyo Na NAFSI ZA wabudha achilia Mbali kwamba BUDHA amekuwa re incarnated from time to time..

UPENDO. UPENDO UPENDO
Umeupiga mwingi ntarudi ngoja nmalizie homework
 
Nimesema Dunia Ni nyumba YENYE Kila kitu ( furnished) ambayo imekuwa mortgaged Kwa binadamu..Hivyo vitu vingine kama Wanyama, mimea etc Ni furniture's Na mapambo
Binadamu huyu wa juzi. hiyo dunia yenyewe mwenyewe ni mgeni ni kama mtalii nae anashangaa . mfano pyraminds hatujui nani kajenga kuna mashimo ambayo hatujui mwisho na hatujui nani kachimba kuna majengo hatujui nan kajenga alafu unasema dunia iko mortgaged kwa ajili ya binadamu unacho andika unakijua kwel au unafanya kuburudisha
 
Sio kweli, wapo mapacha wanafanana mpaka finger print fuatilia uthibitishe mwenyewe.

Kuna story amaizing juu ya pacha wanaaofanana ambapo moja aliiba vito, wakamdaba akasema sio yeye ikabidi aachiwe cuz ilishindikana kuwatofautisha

same case imewahi kutoka seoul, south korea!
 
Binadamu huyu wa juzi. hiyo dunia yenyewe mwenyewe ni mgeni ni kama mtalii nae anashangaa . mfano pyraminds hatujui nani kajenga kuna mashimo ambayo hatujui mwisho na hatujui nani kachimba kuna majengo hatujui nan kajenga alafu unasema dunia iko mortgaged kwa ajili ya binadamu unacho andika unakijua kwel au unafanya kuburudisha
U think too much bro
 
Binadamu huyu wa juzi. hiyo dunia yenyewe mwenyewe ni mgeni ni kama mtalii nae anashangaa . mfano pyraminds hatujui nani kajenga kuna mashimo ambayo hatujui mwisho na hatujui nani kachimba kuna majengo hatujui nan kajenga alafu unasema dunia iko mortgaged kwa ajili ya binadamu unacho andika unakijua kwel au unafanya kuburudisha
Kwani ikulu ya DSM unajua Nani kaijenga?
 
Mmmmmh I smell something wrong here!
Ngoja nihifadhi nondo Kwa matumizi ya baadae
Usimwage Michele Kwenye kuku wengi ila hiyo theory Ina contradiction nyingi Sana!

Ila Kwa upande wa wafia dini hapo umegonga penyewe!
 
Mmmmmh I smell something wrong here!
Ngoja nihifadhi nondo Kwa matumizi ya baadae
Usimwage Michele Kwenye kuku wengi ila hiyo theory Ina contradiction nyingi Sana!

Ila Kwa upande wa wafia dini hapo umegonga penyewe!
Hakunaga theory isiyo kuwa Na contradiction
 
Mfumo upya wa utawala !! utawala upii? wa kutoka wapi na utakuja lin? ata uwanzisha nani na kwann?
Mkuu ukitaka straight answers jaribu na wewe kutoa majibu yaliyo straight..

Nchi fulani mwanasayansi mmoja ametengeneza coiled drumg zinazo zunguka kwa spend kubwa sana kuna element ameziweka ndani zitengeneze mlipuko kama wa big bang theaory coz walitega vinasa sauti kutoka kwenye space ya mbali sana kipindi cha nyuma walisikia sauti flani ambayo inafanana na sauti inayo toka kwenye hii cioled drum ya sasa.
Maana yake there is a place where is the heart of the universe and its active up to today explosion never end, expand more and more and more. nimeandika kwa uchache coz siikumbuki vizur nilisoma muda kidogo
Ebu tueleezee kidogo juu ya hayo uliyo yaandika hapo juu... Labda tutaanzia hapo.

Ni element zipi zilitumia/kuziweka kwenye hiyo coil?
Space ya mbali, ipi?
Space ipi hiyo ambayo inakuwa regarded kama heart of the universe?
 
It was a nice read, tho nilianza kuhisi nimerudi kanisani. I don't agree with some things, or rather some things are questionable/debatable/unresolved, mfano Yesu kufufuka, but you gave me something to think about.
 
Back
Top Bottom