Dunia yashangazwa na kubadilika ghafla kwa Rais Samia kutoka kuwa mtenda haki na kuanza uonevu

Dunia yashangazwa na kubadilika ghafla kwa Rais Samia kutoka kuwa mtenda haki na kuanza uonevu

Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Wakati Sabaya anakamatwa Mbowe na genge lake walishangilia sana na kumuona mama kuwa ni mtoa haki pekee ambae hajawahi kupatikana toka dunia iumbwe, leo imekuwa zamu ya Mbowe watu waliomsifu mama wanaanza tena kumeza matapishi yao kwa kugeuza sifa zake kuwa matusi. Lkn hili wenye akili hatushangai maana ni kawaida upinzani kubadilika badilika, leo lowasa fisadi, kesho lowasa sio fisadi, leo kikwete dhaifu kesho kikwete ni raisi bora na magufuli ni dikteta, leo mama anaupiga mwingi, kesho mama ni katili zaidi ya ukatili wa magufuli nk.
Tatzo nyumbu wana akili ndogo sanaaaaaaa, ko wanataka mahakama iwe huru kumkamata sabaya tuu ila mungu wao mbowe asiguswe? Hii kitu ndo tunataka , wote tuwe sawa na syo wanasiasa wawe na kinga ya sheria kisa n wanasiasa,. Tusubiri kesi iende mahakaman tuone ushahid wa upande wa mashtaka na kama akionekana na hatia apelekwe KISONGO AKUTANE NA SABAYA😂😂😂
 
Wahuni wanamshauri Bi mkubwa awe katili, muonevu kama Jiwe, wakimdanganya kuwa eti akiwaruhusu wapinzani kuenjoy haki zao za kisiasa basi watainuka kisiasa. Na yeye anauchukua huu ushauri wa kipuuzi Matokeo yake anageuka "Dictatress".

Alikuwa anakwenda vizuri ktk siku zake za awali za utawala wake, Sasa hivi ndo anakunjua makucha yake kutuonysha kutoheshimu kwake katiba aliyoapa kuilinda!

Asipogutuka na kuwa sober nchi itamshinda!
Mkuu,

Huna hoja ya kusema Mama haheshimu katiba aliyoapa kuilinda. Jambo kubwa kwa taifa hili ambalo ndio tunu nambari moja ni amani. Na mama is doing extremely well in preserving it.

Hatushughulishwi na mbwa wa kizungu wanaobweka huko CNN na ALJAZEERA
 
Samia alidhani kupaka wanja ndio urembo, kumbe ni hadaa tupu ambayo watu wanaitambua haraka!

Samia kwa sasa hana lolote analoweza kusifiwa kwamba kalisimamia vyema, uongozi wake ni wa mashaka sana.
Kwenu nyinyi yes.

Maana tunajua kwamba nyinyi hamna jema mnaloweza kufanyiwa mkaridhika.

Tutasimama na rais wetu iwe jua iwe mvua.
 
Aisee ndugu yangu...., kumbuka hata Mugabe-Zimbabwe alikuwa anazungumza propaganda na maneno kama haya unayosema......haya ndugu yangu, sie watazamaji tu......
hahaha !! I am just being sarcastic!!
Aisee ndugu yangu...., kumbuka hata Mugabe-Zimbabwe alikuwa anazungumza propaganda na maneno kama haya unayosema......haya ndugu yangu, sie watazamaji tu
 
Kelele za CHURA hazimzuii TEMBO kunywa maji.....

Hiyo CNN na hiyo DUNIA imeshaongea sana kuhusu RWANDA....Mh.Kagame bado yupo.....M7 yupo....

CNN hawajapewa kibali cha KUWAAMULIA WENGINE WAISHI VIPI.....

TANZANIA IS A SOVEREIGN COUNTRY ,WE AS THE PEOPLE KNOW MUCH ABOUT OURSELVES THAN FOREIGNERS

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#AmaniKwanza
Well said. Mkuu huu uzi mbona hukuniita mapema???
 
Mtaa gani unaousemea? huku mtaani mbona mambo shwari tu?

Shida yenu CDM ni kutaka kuwin sympathy za watu wa nje,badala ya kupambana mpate sympathy ya wananchi wa Tanzania ambao kimsingi ndo waamuzi wa hatima yenu.Kwa kufanya hivyo mnaonekana kama chama cha vibaraka.
Dah! Uko vizuri. Asante sana[emoji106]
 
Wakuu wa Majeshi ya ulinzi ndo wanaongoza nchi hii hasa kwa Kumtishia maisha Mama Samia Suluhu Hassan
1.Inspector General of police(IGP)
- Simon Sirro
2.Commander of defence force(CDF)
- Venance Mabeyo
Hii ni legacy ya Magufuli
 
Wewe unadhani watu lazima wafanye mivuruguvurugu ndo ujue wamekasirishwa na jambo
Watanzania siyo watu wa mivurugu lakini wakikasirshwa wanazungumza, wanasema wanatoa rai
Sasa kama wewe ni kiongozi mbabe unaweza kuamua kupuuza, lakini hii haimaanishi kuwa raia hawasemi
Raia gani wanasema? Raia wenyewe si ndiyo sisi? Kwanini wakimbilie nje? Kwani wao ndiyo wanawachagua au kuwapigia kura?
 
Nimegundua hawa jamaa wanaelewa kila kitu kinachoendelea nchi hii.

Ukiacha hili la Mbowe,huyo Prof. anajua mpaka habari ya hizi tozo za laini za simu na wanasema kabisa ni za kututia watanzania umasikini.

Tuko uchi!
Kama serikali inavyoelewa kila uchafu wenu- mko uchi kabisa maana mpaka mje mfike huko al jazeera mkiwa uchi mtakuwa mmeshaaibika sana.
 
Mifumo yote tunayotumia inatokana na wao

Camera, security systems nk. Lazima wajue kila kitu
Ni kweli yatokana na wao lakini si kweli kuwa lazima wafahamu kila kitu..

Unaweza kununua mitambo na kuiweka katika mazingira utakayo weye.

Cha msingi kuwa na watu ambao na uelewa katika kusimamia na kuindesha hiyo mitambo.
 
Alikuwa na nafasi moja nzuri sana ya kujijenga kisiasa na kupata heshima kubwa ya kukumbukwa kama kiongozi aliyeibadili Tanzania kutoka kwenye janga.

Miaka minne hii, angejikita katika kufanya mabadiliko ya kisiasa nchini, akasimamia haki, utawala wa sheria.
Angewanyima wapinzani ajenda ya kumsumbua, na 2025 asingepata upinzani wa kumtisha.

Haya yote kayatupilia mbali kwa muda mfupi sana. Lililobaki kwake sasa ni kuzidi kukandamiza zaidi ili yeye na chama chake waendelee kuwepo madarakani.
Hii ni kazi ngumu. Hakuna ajuae Tanzania itaendelea kuvumilia kuwa chini ya udikteta.
Hahahaahahahahha.

Kuwa wewe rais ufanye hivyo.
 
Aliambiwa apige chini sumu za jiwe,ngoja aendelee kubugia sumu.Tozo,kamatakamata cv ishabomolewa
 
Samia hajabadilika,Kaacha utawala wa sheria uganye kaZi yake... Kaacha mahakama na polisi na usalama kufanya kaZi

Kelsi ikiisha ataheshimu maamuzi, Ndicho tulichokua tunataka... Sasa akiingilia Leo kesho la polisi tutakua tunamsaidia?

Inakua vipi Leo chadema mnataka Samia aingilie mahakama? Tulieni, kama ya mdudr au kesi nyingine maamuzi yatatoka

Pia mbowe asome alama za nyakati - sio kila publicity inamjenga, this one imemchonganishaa zaidi na wananchi wa kawaida... The drama he created was unnecessary
hakika
 
Kinachonisikitisha, huyu mama alikuwa na nafasi ya kipekee ya kupendwa na kukong'a nyoyo za watanzania.
Alitakiwa afanye mambo. matatu tu

1. Kuachana na pia kurekebisha mambo ya kijingajinga ya mtangulizi wake

2. Kuyafanyia kazi mazuri ya mtangulizi wake ikiwemo miradi mikubwa

3. Kufanya reforms za msingi za kiuchumi na kisiasa ili yale yaliyojitokeza kwa mwendazake yasijitokeze tena

Sasa unfortunately kaanza kukumbatia hata yale ya kijinga ya mwendazake kama kuonea, kutoheshimu katiba na kiapo alichokula.

Asipobadilika, wananchi watamchukia vibaya sana!
Hivi nyie watu akili zenu ziko sawasawa??

Mtangulizi wake ndio nini?? Mheshimiwa rais alikuwa ni msaidizi nambari moja wa hayati Magufuli.

Halafu kwenu nyinyi kuheshimu katiba ni kuruhusu mikutano ya kisiasa tu???? Si mngeshinda nyinyi uchaguzi ili muje na hoja zenu mzifanyie kazi???
 
Mama alianza vizuri kina mbowe wenyewe wamembadilisha,kwa walichokifanya kina mbowe naombea sabaya aachiwe apewe ukuu wa wilaya wake kule kule hai,mdude akamatwe atuambie watanzania wembe aliemnyolea magu ni upi ambao anadai atamnyolea samia wembe huo huo,mtu alishaanza kuweka mambo sawa mnaanza kumletea ujinga!
Tunawaangalia sasa huku tukiwasubiri wamlazimishe mama.

Wao walisema watamlazimisha
 
🤣🤣
Mkuu uliyasema hayo kipindi kile baada ya UCHAGUZI WA 2020....Robert Amsterdam HAKUTOKEA na zile "issue" za THE HAGUE.....🤣

Nimekugusia mh.Kagame na mh.Museveni kukuonesha ni jinsi gani kuwa PAMOJA NA DUNIA NA WANAHARAKATI kuwaandama kwa maneno mengi na makali ila BADO WAPO....sembuse Tanzania ya CCM ?!! Sembuse Rais wetu mh.SSH?!!!

#HakunaNamnaKaziInaendeleaTu
#PundaAfeMzigoUfike
#MzigoNiAmaniYaNchi
#MzigoNiUtulivuWaNchi
#JMTMilele
Kwani Za hegi kesi haijafunguliwa bado??
 
Back
Top Bottom