Dunia yashangazwa na kubadilika ghafla kwa Rais Samia kutoka kuwa mtenda haki na kuanza uonevu

Dunia yashangazwa na kubadilika ghafla kwa Rais Samia kutoka kuwa mtenda haki na kuanza uonevu

Tatizo umetengeneza picha kichwani kwako dunia inajali sana viongozi wastaarabu kitu ambacho si kweli. Museveni, Kagame na Magufuli wote wana tabia zinazofanana lakini ni wapi uliwahi kusikia wameadhibiwa kwa tabia zao za hovyo. Tigray (TPLF) wa Ethiopia ni kundi la kigaidi lakini ni mshirika wa Marekani wapi umewahi kusikia wanaandikwa vibaya kwenye vyombo ya kimataifa.

Je Marekani inaonekana kituko kwa kuendelea kumshikilia Julian Assange Uingereza kwa kesi za kubumba. Hakuna anaeguswa na kinachoendelea Tanzania labda Mama akosee hesabu kwa wakubwa wa dunia hii ndio ataundiwa zengwe.

Dunia iliyostaarabika haiwataki viongozi wastaarabu wasio na maslahi kwa wakubwa (Evo Morales wa Bolivia).
Hawa Chadema hawana upeo huo.

Reality hawaziangalii. Wanaishi kwenye dunia ya kusadikika
 
Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Wakati Sabaya anakamatwa Mbowe na genge lake walishangilia sana na kumuona mama kuwa ni mtoa haki pekee ambae hajawahi kupatikana toka dunia iumbwe, leo imekuwa zamu ya Mbowe watu waliomsifu mama wanaanza tena kumeza matapishi yao kwa kugeuza sifa zake kuwa matusi. Lkn hili wenye akili hatushangai maana ni kawaida upinzani kubadilika badilika, leo lowasa fisadi, kesho lowasa sio fisadi, leo kikwete dhaifu kesho kikwete ni raisi bora na magufuli ni dikteta, leo mama anaupiga mwingi, kesho mama ni katili zaidi ya ukatili wa magufuli nk.
endelea kuwa mshabiki
 
🤣🤣Basi POST ni kituko....

Compatriot wako MISSILE OF THE NATION ameanza na "DUNIA YASHANGAZWA..."

Kumbe Museveni na Kagame si wakazi wa DUNIA anyway mh.Rais SSH ni AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA....ameapa kulinda amani na utulivu wa nchi KWA TAARIFA ZOZOTE APATAZO....

Tusubiri mahakama iseme kuwa WATUHUMIWA WA UGAIDI hawana KESI YA KUJIBU.......

#KaziIendelee
Tena ni AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA TANZANIA YOTE
 
Alibugi kusema katiba isubiri uchumi, sasa atatumia urais wake kupambana na wapinzani.
Na atakumbukwa kama dikteta wa kwanza mwanamke.
Hahahahaa.

Hana muda mchafu, ni mbowe na genge lake ndio watatumia muda wao kupambana na polisi. Huku kazi zinasonga
 
Nimegundua hawa jamaa wanaelewa kila kitu kinachoendelea nchi hii.

Ukiacha hili la Mbowe,huyo Prof. anajua mpaka habari ya hizi tozo za laini za simu na wanasema kabisa ni za kututia watanzania umasikini.

Tuko uchi!
It didn't need rocket science to know hizo tozo hazimsaidii masikini
 
Hivi nyie watu akili zenu ziko sawasawa??

Mtangulizi wake ndio nini?? Mheshimiwa rais alikuwa ni msaidizi nambari moja wa hayati Magufuli.

Halafu kwenu nyinyi kuheshimu katiba ni kuruhusu mikutano ya kisiasa tu???? Si mngeshinda nyinyi uchaguzi ili muje na hoja zenu mzifanyie kazi???
Mwanafunzi ujifunza kwa Mwalimu
 
Hivi hamjaelewa tu where is the diverting point started? Mama alianza vizuri na infact hakutaka kabisa kuishi kwenye siasa za mivurugano na mitifuano. Anaamini kwenye kuliendea jambo kwa njia ya utaratibu na mazungumzo. Bado sijajua why intelligensia ya Chadema ni mbovu kiasi cha kushindwa kwenda naye na kupenyeza agenda zao na kuziweka sawa.

Sadly wakachagua njia ya vurugu. Ukizingatia tabia za wanawake kutopenda kuonekana wanyonge na nguvu kubwa iliyokuwa imezoea siasa za mipasho, umekuwa rahisi kwao kumshawishi mama kwamba "Hawa watu hawabebeki".

In short kinachoendelea ni kile kiitwacho LISILO BUDI HUTENDWA.

Katika hili sioni pa kumlaumu Samia zaidi ya bad approach ya Mbowe na Chama chake. Honestly speaking, Chadema imekuwa na utaratibu kutuchanganya tunaoiamini.
Poleni sana mnaoiamini
 
Kelele za CHURA hazimzuii TEMBO kunywa maji.....

Hiyo CNN na hiyo DUNIA imeshaongea sana kuhusu RWANDA....Mh.Kagame bado yupo.....M7 yupo....

CNN hawajapewa kibali cha KUWAAMULIA WENGINE WAISHI VIPI.....

TANZANIA IS A SOVEREIGN COUNTRY ,WE AS THE PEOPLE KNOW MUCH ABOUT OURSELVES THAN FOREIGNERS

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#AmaniKwanza
Hata kama haitamzuia tembo kunywa maji tayari mmesimama jalalani,CNN inasikika duniani sio hapo geita ulipo peke yake.
 
CNN ni fake news Rais Samia ana haki ya kulinda umoja wa Tanzania kutoka kwa hao maamluki wa kisiasa akina Mbowe and his company. Leo watanzania wameamini Hayati Magufuli alikuwa sahihi kabisa jinsi alivyoshughulikia hawa wanasiasa wa upinzani. Mbowe, Tundu Lissu na Maria Sarungi wasitegemee kuyumbisha nchi hii chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. CCM ni ile ile
Na tutasimama madhubuti.

Hatutokubali kuingia kwenye machafuko kamwe.

Amani ndio suala la msingi zaidi kwetu
 
Samia hajabadilika,Kaacha utawala wa sheria ufanye kaZi yake... Kaacha mahakama na polisi na usalama kufanya kaZi

Kesi ikiisha ataheshimu maamuzi, Ndicho tulichokua tunataka... Sasa akiingilia Leo kesho la polisi tutakua tunamsaidia?

Inakua vipi Leo chadema mnataka Samia aingilie mahakama? Tulieni, kama ya mdude alishinda kesi bila, akina mbowe wakarudishiwa pesa zao, simply because mama alitaka haki itendeke, iweje Leo mnataka aingilie watu walewale waliowapa haki just a few weeks ago? Mimi nadhani tusubiri Tu kesi hii kama zilivyo nyingine na maamuzi yatatoka... Hata wale uamsho wanashukuru mama kuheshimu mahakama...

Pia mbowe asome alama za nyakati - sio kila publicity inamjenga, this one imemchonganishaa zaidi na wananchi wa kawaida... The drama he created was unnecessary
I agree with you
Mbowe alijisahau akaanza kumtisha mama labda alisahau kuwa she is President
Bahati mbaya naona sympathy ya Wa TZ kwake imepungua sana
 
Hivi kwa namna gani angeweza kutimiza demand za upinzani ndani ya miezi minne? Tuwe rational kidogo.

Mama ameingia amekuta Hali ya uchumi mbaya kabisa kwa uharibifu wa magufuli. Private sector almost dead, graduates hawana ajira. Kuna janga la Corona ambalo solution yake bado ni kitendawili. Amekuta miradi mingi kuliko uwezo wa serikali ku finance miradi hiyo. Bado katika Hali hizo tunamtaka aanze kuwaita wabunge wale posho au kuitisha referendum ya katiba mpya? Are we serious? Hizo pesa zinatoka wapi na Hali ya uchumi ingekuwaje? Na Chama chake kingemuelewa vipi? Ametumia lugha ya kiungwana kwamba aanze na kuweka sawa uchumi then atageukia katiba. Definitely hayo ni maneno ya kutafuta namna ya kuongea na Chama chake ili agenda ya katiba airudishe. What's wrong with this approach? Sad, mnamtisha na mnaruhusu wavuta bange akina mdude watumie maneno ya kifedhuli huku tukitoa mashinikizo yasiyo na maana.

Sote tunajua kwa tuliyoyashuhudia kwa JPM, katiba mpya ni MUHIMU ili kuaddress changamoto zilizopo lakini kea namna gani katiba mpya tunaidai na kufanya katiba mpya kama ni agenda ya Chadema na si wananchi, hapo ndipo shida ilipo. Kwa maoni yangu yanayoendelea ni fundamental mistakes za Chadema wenyewe.
You nailed it mkuu.

Nobody could say it better
 
Tena wala asiwasikilize hao mabeberu waharibifu wa dunia
Mama nae alivyo anaweza akakusikiliza ushauri wako,kumbe unamwingiza chaka kwa masilahi yako ya kufisadi nchi hii.

Ccm mnajua katiba Mpya itawaondolea ulaji,itampa RAIA madaraka.
 
Haki inadaiwa na wala haiombwi.
Haya endeleeni kuidai, na katika kuidai huko tusiskie kelele za CNN wala ALJAZEERA wala wapumbavu wowote wale.

Nyinyi endeleeni kudai haki Sisi tunaendelea kujenga nchi yetu
 
I agree with you
Mbowe alijisahau akaanza kumtisha mama labda alisahau kuwa she is President
Bahati mbaya naona sympathy ya Wa TZ kwake imepungua sana
Huwezi ukawa na sympathy Kwa MTU ambaye hata Hana shukran
Mbowe was abused, people felt sorry for him, mama akamrudishia tumaini, jamaa akatoka Dubai alipokua analipwa na mabeberu, akarudi, akarudishiwa pesa zake, hata kabla hayajaisha, tayari kaanza kumtingisha yuleyule aliyemfanya awe na confidence ya kurudi

Nadhani angekua amesoma kidogo, angefanya mambo kisomi zaidi
 
Back
Top Bottom