Sun is Sun
JF-Expert Member
- Mar 13, 2024
- 649
- 975
PreachIngekuwa ameahidi kuwa Duniani ni bata na kujichana hapo kweli , lakini yeye kaahidi hapa Duniani ni kama uwanja wa majaribio wa dhiki , matatizo ,shida na raha mbalimbali na akatoa bishara njema kwa Wenye kusubiri na kutengamaa sawasawa kama jinsi alivyoelekeza.
Maisha ya peponi ndio ameahidi Kutokuwa na Tabu Wala dhiki sasa ikitokea mtu kaenda peponi Kisha kakuta hali kinyume hapo haitakuwa haki .
Kulalamika uwepo wa dhiki hizo Duniani ni sawa na mtu kushangaa rafu katika mechi ya mpira wa miguu au kulalamika kwa Nini magoli yawepo uwanjani wakati hiyo ndio asili yake jinsi ilivyoumbiwa na kila kitu kina hekima zake kuwepo.
Maumivu yanasababisha watu waamini Mungu hayupo na hayo hayo yanafanya wengine waamini Mungu yupo...Wengine wanatukana kwa sababu ya challenge na wengine wanashukuru challenge wakizivuka wanakuwa bora kuliko jana na wanagundua mazuri ambayo Mungu ameyaficha kwenye ngazi ya mwisho ya maumivuDunia yenye vita, Dunia yenye kila aina ya majanga ya asili(tsunami, tetemeko n.k),Dunia yenye vichaa, Dunia yenye ukatili wa kila namna, Dunia yenye vipofu, Dunia yenye ajali, Dunia inayobagua walemavu na wazima, Dunia inayobagua makapuku na wenye navyo.
Hayo yote yote yanathibitisha Mungu mwenye upendo, huruma na anayejali hayupo.
Mungu ni muweza wa yote, ila japokua ni muweza wa yote, mambo mengine Duniani yanatokea kama uchaguzi mbaya wa mwanadam ,na hatakiwi kulaumiwa.Dunia yenye vita, Dunia yenye kila aina ya majanga ya asili(tsunami, tetemeko n.k),Dunia yenye vichaa, Dunia yenye ukatili wa kila namna, Dunia yenye vipofu, Dunia yenye ajali, Dunia inayobagua walemavu na wazima, Dunia inayobagua makapuku na wenye navyo.
Hayo yote yote yanathibitisha Mungu mwenye upendo, huruma na anayejali hayupo.