Dunia yenye kila aina ya maumivu inathibitisha kuwa Mungu mwenye upendo na huruma hayupo

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
649
Reaction score
975
Dunia yenye vita, Dunia yenye kila aina ya majanga ya asili(tsunami, tetemeko n.k),Dunia yenye vichaa, Dunia yenye ukatili wa kila namna, Dunia yenye vipofu, Dunia yenye ajali, Dunia inayobagua walemavu na wazima, Dunia inayobagua makapuku na wenye navyo.

Hayo yote yote yanathibitisha Mungu mwenye upendo, huruma na anayejali hayupo.
 
Mungu wapo tofauti tofauti zaidi ya 1000 kulingana na dini ila shetani ni mmoja tu.
 
Naunga mkono hoja hata ili tunda lijaonewa huruma
IMG_0742.jpeg
 
Ingekuwa ameahidi kuwa Duniani ni bata na kujichana hapo kweli , lakini yeye kaahidi hapa Duniani ni kama uwanja wa majaribio wa dhiki , matatizo ,shida na raha mbalimbali na akatoa bishara njema kwa Wenye kusubiri na kutengamaa sawasawa kama jinsi alivyoelekeza.

Maisha ya peponi ndio ameahidi Kutokuwa na Tabu Wala dhiki sasa ikitokea mtu kaenda peponi Kisha kakuta hali kinyume hapo haitakuwa haki .

Kulalamika uwepo wa dhiki hizo Duniani ni sawa na mtu kushangaa rafu katika mechi ya mpira wa miguu au kulalamika kwa Nini magoli yawepo uwanjani wakati hiyo ndio asili yake jinsi ilivyoumbiwa na kila kitu kina hekima zake kuwepo.
 
Preach
 
Mungu angekuwepo watoto wasio kuwa na hatia wasingebakwa, Mungu angekuwepo angesaidia watoto yatima waliogeuka machokoraa mitaani.

Mungu mwenye upendo wote hayupo.
 
Dunia yenye vita, Dunia yenye kila aina ya majanga ya asili(tsunami, tetemeko n.k),Dunia yenye vichaa, Dunia yenye ukatili wa kila namna, Dunia yenye vipofu, Dunia yenye ajali, Dunia inayobagua walemavu na wazima, Dunia inayobagua makapuku na wenye navyo.

Hayo yote yote yanathibitisha Mungu mwenye upendo, huruma na anayejali hayupo.
Maumivu yanasababisha watu waamini Mungu hayupo na hayo hayo yanafanya wengine waamini Mungu yupo...Wengine wanatukana kwa sababu ya challenge na wengine wanashukuru challenge wakizivuka wanakuwa bora kuliko jana na wanagundua mazuri ambayo Mungu ameyaficha kwenye ngazi ya mwisho ya maumivu
 
Mathayo 24
33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
 
Dunia yenye vita, Dunia yenye kila aina ya majanga ya asili(tsunami, tetemeko n.k),Dunia yenye vichaa, Dunia yenye ukatili wa kila namna, Dunia yenye vipofu, Dunia yenye ajali, Dunia inayobagua walemavu na wazima, Dunia inayobagua makapuku na wenye navyo.

Hayo yote yote yanathibitisha Mungu mwenye upendo, huruma na anayejali hayupo.
Mungu ni muweza wa yote, ila japokua ni muweza wa yote, mambo mengine Duniani yanatokea kama uchaguzi mbaya wa mwanadam ,na hatakiwi kulaumiwa.
 
Mambo ya mbinguni ni hadithi za kusadikika kama hadithi za sungura na fisi. Hakuna kitu kinachoitwa Mbinguni wala kuzimu.

Mbingu ingekuwepo na nzuri na utamu unaoelezewa kwenye biblia usingeona Papa mwenye miaka 88 anapambania uhai wake hospitalini asife, anachohofia kufa ni nini kama akifa anaenda mbinguni kukaa na baba na kula raha milele na milele?

Mambo ya Mungu, mbinguni na ujinga mwingine unaofanana na huo ni hadithi tu za kutunga, hazina ukweli wowote.
 
Back
Top Bottom