Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #281
Navyofahamu mimi muswada hupelekwa bungeni ukajadiliwa na ukipita hupelekwa kwa rais kusainiwa ili kuwa sheria!
Nina uhakika umekimbia maswali yangu kwa kujua ukweli ulipo.Ahaa, kamani hivyo, je ndivyo ilivyofanyika katika muungano wetu?
Huko nyuma umeninukuu nikisema uhalali wa muungano upo katika muda wa 50 tuliokaa pamoja, kisheria kuna walakini.
Ninasimama na maneno hayo kwasababu zile zile zilizokukimbiza usijibu hoja.
1. Muungano uliundwa na Nyerere na Karume. TANU au ASP hazikushirikishwa wala wananchi.
Hata mwanasheria mkuu wa znz marehemu Duarado akapewa likizo ya lazima.
Hakuna mahali kulifanyika kikao cha bunge iwe la Tangayika au baraza la mapinduzi kufikiria, kuridhia kujadili muungano kabla ya April 26 1964.
2. Kumbuka huu ni mkataba wa kuunganisha nchi na si wa madini unaoweza kusainiwa na Karamagi kwa mama ntilie, hivyo ilipaswa uwepo mfumo wa kuwashirikisha wananchi moja kwa moja au kupitia vyombo vingine.
Kilichotokea ni Muungano kufanyika kwanza hapo April 22-26 na kufuatiwa na 'decree' kabla ya bunge la muda na mpito kupitisha sheria za mkataba ule katika mambo kadha wa kadha ili kuuboresha.
Hii maana yake sheria 'ilisainiwa' kwanza halafu bunge likafuatilia 'kuboresha' sheria zinazohusiana na mkataba.
Kwa maneno yako, mswada hujadiliwa na kisha kuwa sheria baada ya kusainiwa.
Ukitazama mtiririko wa muungano utaona unakinzana na maneno yako.
Hivyo si mimi wa kufanya research kuthibitisha ukosefu wa uhalali, ni wewe ufanye research ya kuthibitisha uhalali wa muungano.