Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #301
PROFESA SHIVJI ALICHANGIA SANA UPOTOSHAJI
Tutakumbuka wakati wa bunge la katiba mwanzoni kabisa, prof Shivji alialikwa katika kongamano.
Katika mada yake profesa alizua tafrani inayoacha maswali mengi kuliko majibu.
Profesa alitumia muda mwingi kuisumanga Tanganyika kana kwamba ndilo tatizo la muungano. Hilo halikuanza siku za karibuni, tunakumbuka ziara zake za mabaraza kule Zanzibar akieleza dhulma na kukoksekana kwa uhalali wa muungano.
Shivji alijenga hoja za Zanzibar kuporwa madaraka na maamuzi yake.
Kinachostua ni ukweli kuwa Profesa alikaa kimya sana wakati wa mchakato hasa huku bara.
Kabla ya bunge la katiba akajitokeza na kudai muundo muafaka ni serikali 2 akiwaunga mkono CCM.Katika hoja zake, Shivji alidai Tanganyika haijawahi kuwa na utaifa ukilinganisha na Zanzibar yenye karne zaidi ya mbili.
Alisema Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na mwaka 1964 tukaungana wakati Nyerere akiwa bado anajenga utaifa.
Profesa anataka tuamini kuwa sisi ni Taifa kwasababu ya muungano, na kwamba muungano usingekuwepo sijui tungekuwa taifa gani.
Lakini hoja kubwa aliyoikwepa ni kuhusu katiba ya ZNZ ya 2010.
Kwa utetezi wa juu juu Profesa alisema kifungu cha katiba hiyo kinacholazimu mambo ya muungano lazima kikubaliwa na BWL, si tatizo bali ni kukamilisha tu taratibu.
Tunachotaka kumuonyesha profesa ni jinsi ambavyo pengine kwa hisia tu au sababu zingine ameficha ukweli unaohusiana na kifungu hicho.
1. Katika bunge la JMT wapo wabunge 81 kutoka Zanzibar wanaowakilisha Zanzibar
Wabunge hao wanalipwa na Tanganyika kwa kuwakilisha nchi yao.
Pamoja na hayo maamuzi yanayohusu masuala ya muungano hupitishwa na bunge, wao wakiwa ni sehemu yake. Tena wamepewa uwezo wa kuamua kwa kukataa au kukubali kama wazanzibar.
2. Kwavile kuna wabunge 81 wanaokuja kwa masilahi ya znz, hakuna sababu za jambo lolote lile kupelekwa baraza la wawakilishi kwa ajili ya kuidhinishwa.
Kufanya hivyo ni kuliweka bunge la JMT chini ya baraza la wawakilishi lisilo na Mtanganyika hata mmoja achilia mbali kwa bahati mbaya.
3. Kama anavyosema Profesa ni kukamilisha utaratibu, hakuna sababu za kuwa ni kifungu hicho.
Wazungu wanasema 'If it is not broken don't fix it' kwamba kama hakuna tatizo au uharibifu huna haja ya matengenezo. Na BLW kama linakamisha tu utaratibu(formality) hakuna sababu ya kuweka kifungu hicho.
4. Kifungu hicho kimeonekana kuwa na nguvu kwani tume ya Warioba haikuweza kufanya kazi hadi pale BLW liliporidhia.
Hivyo basi kuna kila sababu ya kuamini kuwa kifungu hicho kimewekwa makusudi ili kuifanya Zanzibar iwe na mamlaka juu ya mambo ya Tanganyika.
Hili ni jambo ambalo Profesa Shivji amelipotosha sana kwa kuaminisha watu kuwa katiba ya 2010 haina tatizo katka muundo wa muungano wa sasa.
Ni kwa kuamini hivyo, CCM na akina Nape Nnauye hupita wakiuzngumzia UKAWA zaidi ya matatizo makubwa yaliyopo.
Tatizo la katiba ya 2010 haliwezi kufumbiwa macho. Ni tatizo linaloleta mgongano wa kikatiba.
Ipo siku taifa la Tanganyika litashindwa kufanya maamuzi ya wananchi wake wakisubiri maamuzi hayo yaidhinishwe na BLW.
Wakati hayo yanatokea Zanzibar yenye wawakilishi katika serikali na bunge la JMT wanajitambua kama TAIFA kwa mujibu wa katiba yao ya 2010.
Akina Nape kama Profesa Shivji hawalioni tatizo la muungano siku zijazo.
Mathalan, siku watiifu wa kusikiliza bila kuhoji akina Nape watakapofikia mahali wamechoka, vijana wa zama hizo wataamka siku moja na kusema muungano wa nchi mbili moja ikiwa uvunguni haukubaliki.
Na tatizo kubwa ni siku Watanganyika watakapochoka kupeleka miswada ya mambo yao ya maendeleo ndani ya BLW. Ukifika muda huo itakuwa ni 'basi yaishe' hakuna muungano wa jambo hata moja.
Tusemezane

Last edited by a moderator: