Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

PROFESA SHIVJI ALICHANGIA SANA UPOTOSHAJI

Tutakumbuka wakati wa bunge la katiba mwanzoni kabisa, prof Shivji alialikwa katika kongamano.
Katika mada yake profesa alizua tafrani inayoacha maswali mengi kuliko majibu.

Profesa alitumia muda mwingi kuisumanga Tanganyika kana kwamba ndilo tatizo la muungano. Hilo halikuanza siku za karibuni, tunakumbuka ziara zake za mabaraza kule Zanzibar akieleza dhulma na kukoksekana kwa uhalali wa muungano.
Shivji alijenga hoja za Zanzibar kuporwa madaraka na maamuzi yake.

Kinachostua ni ukweli kuwa Profesa alikaa kimya sana wakati wa mchakato hasa huku bara.
Kabla ya bunge la katiba akajitokeza na kudai muundo muafaka ni serikali 2 akiwaunga mkono CCM.Katika hoja zake, Shivji alidai Tanganyika haijawahi kuwa na utaifa ukilinganisha na Zanzibar yenye karne zaidi ya mbili.

Alisema Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na mwaka 1964 tukaungana wakati Nyerere akiwa bado anajenga utaifa.

Profesa anataka tuamini kuwa sisi ni Taifa kwasababu ya muungano, na kwamba muungano usingekuwepo sijui tungekuwa taifa gani.

Lakini hoja kubwa aliyoikwepa ni kuhusu katiba ya ZNZ ya 2010.
Kwa utetezi wa juu juu Profesa alisema kifungu cha katiba hiyo kinacholazimu mambo ya muungano lazima kikubaliwa na BWL, si tatizo bali ni kukamilisha tu taratibu.

Tunachotaka kumuonyesha profesa ni jinsi ambavyo pengine kwa hisia tu au sababu zingine ameficha ukweli unaohusiana na kifungu hicho.

1. Katika bunge la JMT wapo wabunge 81 kutoka Zanzibar wanaowakilisha Zanzibar
Wabunge hao wanalipwa na Tanganyika kwa kuwakilisha nchi yao.

Pamoja na hayo maamuzi yanayohusu masuala ya muungano hupitishwa na bunge, wao wakiwa ni sehemu yake. Tena wamepewa uwezo wa kuamua kwa kukataa au kukubali kama wazanzibar.

2. Kwavile kuna wabunge 81 wanaokuja kwa masilahi ya znz, hakuna sababu za jambo lolote lile kupelekwa baraza la wawakilishi kwa ajili ya kuidhinishwa.

Kufanya hivyo ni kuliweka bunge la JMT chini ya baraza la wawakilishi lisilo na Mtanganyika hata mmoja achilia mbali kwa bahati mbaya.

3. Kama anavyosema Profesa ni kukamilisha utaratibu, hakuna sababu za kuwa ni kifungu hicho.
Wazungu wanasema 'If it is not broken don't fix it' kwamba kama hakuna tatizo au uharibifu huna haja ya matengenezo. Na BLW kama linakamisha tu utaratibu(formality) hakuna sababu ya kuweka kifungu hicho.

4. Kifungu hicho kimeonekana kuwa na nguvu kwani tume ya Warioba haikuweza kufanya kazi hadi pale BLW liliporidhia.

Hivyo basi kuna kila sababu ya kuamini kuwa kifungu hicho kimewekwa makusudi ili kuifanya Zanzibar iwe na mamlaka juu ya mambo ya Tanganyika.

Hili ni jambo ambalo Profesa Shivji amelipotosha sana kwa kuaminisha watu kuwa katiba ya 2010 haina tatizo katka muundo wa muungano wa sasa.

Ni kwa kuamini hivyo, CCM na akina Nape Nnauye hupita wakiuzngumzia UKAWA zaidi ya matatizo makubwa yaliyopo.

Tatizo la katiba ya 2010 haliwezi kufumbiwa macho. Ni tatizo linaloleta mgongano wa kikatiba.
Ipo siku taifa la Tanganyika litashindwa kufanya maamuzi ya wananchi wake wakisubiri maamuzi hayo yaidhinishwe na BLW.

Wakati hayo yanatokea Zanzibar yenye wawakilishi katika serikali na bunge la JMT wanajitambua kama TAIFA kwa mujibu wa katiba yao ya 2010.

Akina Nape kama Profesa Shivji hawalioni tatizo la muungano siku zijazo.
Mathalan, siku watiifu wa kusikiliza bila kuhoji akina Nape watakapofikia mahali wamechoka, vijana wa zama hizo wataamka siku moja na kusema muungano wa nchi mbili moja ikiwa uvunguni haukubaliki.

Na tatizo kubwa ni siku Watanganyika watakapochoka kupeleka miswada ya mambo yao ya maendeleo ndani ya BLW. Ukifika muda huo itakuwa ni 'basi yaishe' hakuna muungano wa jambo hata moja.

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
KIWEWE CHA KUZINDUKA TANGANYIKA
UNAFIKI WA WAZANZIBAR, KATIBA YA ZNZ 2010 INAELEZA YOTE

BMLK lililoahirishwa limeshuhudia matukio ya matusi, kejeli na kashfa.
Yapo matukio yaliyoshangaza na kuonyesha unafiki na uzandiki.
Matukio hayo yaliwfanywa kwa wingi zaidi na wznz.

Wznz waliondoka na msimamo wa serikali 3 au mkataba.
Ndivyo ilivyokuwa mitaani na mikutano ya CCM na CUF.
Kauli mbiu ikiwa znz kwanza, ikishereheshwa na maneno 'sisi sasa ni wamoja.
Na wala si maneno tu, mawaziri kama Nahodha Shamsa walisikika wakidai znz huru.

Kilichodhihirisha nia ya znz huru yenye mamlaka ni marekebisho ya katiba ya znz ya 2010.
Marekebisho yaliletwa na serikali ya CCM chini ya Amani Karume, yakasimimiwa (BLW) lenye nusu nusu CUF na CCM.

Katiba ikapitishwa na kupigiwa kura na wznz kwa kishindo. Vipengele vinavyokinzana na katiba ya JMT na vinavyoiweka katiba hiyo chini ya udhalili wa katiba ya znz 2010 vilisomeka bila shaka. Wabunge wa znz (JMT) na BLW walivisoma, wanasheria wakavipitia na wasomi kama Shivji wakaviangalia kwa kina vina.

Hakuna mzanzibar, awe mbunge, msomi au mvuvi aliyesimama kuonyesha tatizo la katiba ya 2010.
Hakuna aliyefanya hivyo kwasababu katiba ilitengenezwa dhidi ya 'adui yao Mtanganyika'.
Wznz wakaungana kuhakikisha adui Tanganyika hafurukuti.

Hatukusikia mbunge wowote kutoka znz ndani ya bunge la JMT akieleza utata uliojiojitokeza.
Hatukusikia mwakilishi yoyote kutoka znz akizungumzia matatizo ya katiba ya znz ya 2010.
Wote wameungana kwa ajili ya kukabiliana na adui Tanganyika.

Kabla hatujaendelea, niwakumbushe, mbunge wa znz aliyeuliza swali kuhusu wizara ya sheria na kijibiwa na Werema akaulize kwao. Ni kweli aliyoyasema Werema kwasababu ndani ya bunge la JMT mchango wa wznz haoenekani zaidi ya kuzua tafrani. Mtakumbuka suala la Pinda n.k.

Katika mazingira ya kwaida, wabunge wa znz ndani ya bunge la JMT wangeweza kusimama na kueleza utata wa kikatiba ya 2010,hawakufanya hivyo, ni wamoja dhidi ya adui Tanganyika.

Ni unafiki kwa wazanzibar waliosimama na kutetea serikali 2.
Unafiki unatokana na ukweli kuwa huko nyuma hawakuzungumzia tatizo la katiba yao 2010, leo wanapata ushuja wa kuzungumzia serikali 2 zinaimarisha muungano?
Huu ndio unafiki wa wznz wakiwa Dar es Salaam na wakiwa mizani znz.

Ni unafiki wa wawakilishi (BLW) kutoka znz kuzungumzia S2 kwasababu walishiriki vema kuivunja katiba ya muungano kwa kupitisha katiba ya znz ya 2010.

CUF nao kama wznz wa CCM ni wanafiki. Unafiki wao ni kutokana na kauli zao kuwa wanataka muungano ila muundo ubadilike. Kama walijua hivyo, wangesimama bungeni Dodoma au ndani ya BLW na kuonya kuhusu katiba ya 2010 iliyovunja muugano kwa kuanzia.

Makundi haya mawili ya CCM na CUF yanaongozwa na unafiki.
Kila kundi lina unafiki wake, lakini wana common interest ambayo ni kumtumia Mtanganyika kwa kujifanya wanataka muungano.

Haja yao si muungano wanaousema, ni kutaka kujibanza mgongoni mwa Tanganyika wakipunga upepo kwa gharama ya Mtanganyika.

Huko nyuma tumewahi kuuliza kama wznz wanajua wanachotaka.
Unafiki wa kutupiana matusi na kashfa wakiwa wamekuja na msimamo mmoja ni wa hali ya juu.

Pandu aliongoza kikao cha BLW kujadili S3.
Alipofika Dodoma yeye kama Shasa Vuai hawakubali tena waliyojadiliana znz.
Wanataka S2 kuimarisha muungano ambao wakati znz inauvunja walikuwa kimya.

Ndani ya bunge la katiba, CCM znz wanataka S2 tu ili kuimarisha muungano waliouvunja kwa katiba ya 2010.

CUF wanataka serikali 3 ili kuimarisha muungano waliokubali katiba yake ivunjwe na ile ya 2010
Hakuna mznz hata mmoja aliyesema katiba ya 2010 ni tatizo kubwa. Walichokiona ni nafasi sawa.

Na unafiki wa wznz unafikia kileleni pale waliPOsimama kidete wakitaka tume ya Warioba iwe na wajumbe sawa.

Leo wznz wale wale walioandama kutaka tume iwe na wajumbe sawa, wanakana uwakilishia wa wajumbe wao waliosema S3 ni jibu. Wamedharau tume ya Warioba wakishikilia msimamo wa S2.

Duru tunajiuliza, endapo wzn wangekuwa wachache katika tume sijui leo ingekuwaje.
Kwa mantiki hiyo wznz wa CCM waelewe kuwa katiba yao ya 2010 imeshavunja muungano.
Wana CUF waelewe katiba yao ya 2010 imevunja muungano.

Watanganyika, waelewe muungano ulishavunjwa na wazanzibar.
Hakuna muafaka au jibu la S2 kama katiba ya 2010 ipo wima.

Akina Nape Nanuye hawaliongelei hili kama tatizo. Leo watafanikiwa kulinda muungano kwa mabomu na risasi. Jambo moja hawatafanikiwa, ni kuona Watanganyika wanadhalilika kwa kuandaa taratibu zao eti hadi zipate baraka za BLW.

Hawatafaikiwa kwasababu Watanganyika wameshaona znz inawafanya shamba la bbi.
Mambo yatahamia mitaani, huko hakuna sheria za vitabuni ni sheria za mwituni.
Muungano utabaki ofisini, mitaani watu watakimbizana.

Je,ile methali ya heri nusu ya shari kuliko shari kamili haina maana wakati utakapofika?

Tusemezane
 
PROFESA SHIVJI ALICHANGIA SANA UPOTOSHAJI

Tutakumbuka wakati wa bunge la katiba mwanzoni kabisa, prof Shivji alialikwa katika kongamano.
Katika mada yake profesa alizua tafrani inayoacha maswali mengi kuliko majibu.

Profesa alitumia muda mwingi kuisumanga Tanganyika kana kwamba ndilo tatizo la muungano. Hilo halikuanza siku za karibuni, tunakumbuka ziara zake za mabaraza kule Zanzibar akieleza dhulma na kukoksekana kwa uhalali wa muungano.
Shivji alijenga hoja za Zanzibar kuporwa madaraka na maamuzi yake.

Kinachostua ni ukweli kuwa Profesa alikaa kimya sana wakati wa mchakato hasa huku bara.
Kabla ya bunge la katiba akajitokeza na kudai muundo muafaka ni serikali 2 akiwaunga mkono CCM.Katika hoja zake, Shivji alidai Tanganyika haijawahi kuwa na utaifa ukilinganisha na Zanzibar yenye karne zaidi ya mbili.

Alisema Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na mwaka 1964 tukaungana wakati Nyerere akiwa bado anajenga utaifa.

Profesa anataka tuamini kuwa sisi ni Taifa kwasababu ya muungano, na kwamba muungano usingekuwepo sijui tungekuwa taifa gani.

Lakini hoja kubwa aliyoikwepa ni kuhusu katiba ya ZNZ ya 2010.
Kwa utetezi wa juu juu Profesa alisema kifungu cha katiba hiyo kinacholazimu mambo ya muungano lazima kikubaliwa na BWL, si tatizo bali ni kukamilisha tu taratibu.

Tunachotaka kumuonyesha profesa ni jinsi ambavyo pengine kwa hisia tu au sababu zingine ameficha ukweli unaohusiana na kifungu hicho.

1. Katika bunge la JMT wapo wabunge 81 kutoka Zanzibar wanaowakilisha Zanzibar
Wabunge hao wanalipwa na Tanganyika kwa kuwakilisha nchi yao.

Pamoja na hayo maamuzi yanayohusu masuala ya muungano hupitishwa na bunge, wao wakiwa ni sehemu yake. Tena wamepewa uwezo wa kuamua kwa kukataa au kukubali kama wazanzibar.

2. Kwavile kuna wabunge 81 wanaokuja kwa masilahi ya znz, hakuna sababu za jambo lolote lile kupelekwa baraza la wawakilishi kwa ajili ya kuidhinishwa.

Kufanya hivyo ni kuliweka bunge la JMT chini ya baraza la wawakilishi lisilo na Mtanganyika hata mmoja achilia mbali kwa bahati mbaya.

3. Kama anavyosema Profesa ni kukamilisha utaratibu, hakuna sababu za kuwa ni kifungu hicho.
Wazungu wanasema 'If it is not broken don't fix it' kwamba kama hakuna tatizo au uharibifu huna haja ya matengenezo. Na BLW kama linakamisha tu utaratibu(formality) hakuna sababu ya kuweka kifungu hicho.

4. Kifungu hicho kimeonekana kuwa na nguvu kwani tume ya Warioba haikuweza kufanya kazi hadi pale BLW liliporidhia.

Hivyo basi kuna kila sababu ya kuamini kuwa kifungu hicho kimewekwa makusudi ili kuifanya Zanzibar iwe na mamlaka juu ya mambo ya Tanganyika.

Hili ni jambo ambalo Profesa Shivji amelipotosha sana kwa kuaminisha watu kuwa katiba ya 2010 haina tatizo katka muundo wa muungano wa sasa.

Ni kwa kuamini hivyo, CCM na akina Nape Nnauye hupita wakiuzngumzia UKAWA zaidi ya matatizo makubwa yaliyopo.

Tatizo la katiba ya 2010 haliwezi kufumbiwa macho. Ni tatizo linaloleta mgongano wa kikatiba.
Ipo siku taifa la Tanganyika litashindwa kufanya maamuzi ya wananchi wake wakisubiri maamuzi hayo yaidhinishwe na BLW.

Wakati hayo yanatokea Zanzibar yenye wawakilishi katika serikali na bunge la JMT wanajitambua kama TAIFA kwa mujibu wa katiba yao ya 2010.

Akina Nape kama Profesa Shivji hawalioni tatizo la muungano siku zijazo.
Mathalan, siku watiifu wa kusikiliza bila kuhoji akina Nape watakapofikia mahali wamechoka, vijana wa zama hizo wataamka siku moja na kusema muungano wa nchi mbili moja ikiwa uvunguni haukubaliki.

Na tatizo kubwa ni siku Watanganyika watakapochoka kupeleka miswada ya mambo yao ya maendeleo ndani ya BLW. Ukifika muda huo itakuwa ni 'basi yaishe' hakuna muungano wa jambo hata moja.

Tusemezane
Tatizo lako unasoma pasipo kuelewa maana na hapo ndipo unapokosea sana. Kwa mfano Profesa Shivji anapozungumzia UTAIFA alikuwa na maana rahisi kabisa ya kwamba Muungano wetu umekuja wakati Nyerere alikuwa ktk hatua za kujenga UTAIFA hii haina maana nyingine zaidi ya kwamba sisi wenyewe tulikuwa bado katika mgawanyiko wa makabila 120 ambayo hayakuwa na Umoja wa aina yoyote licha ya kwamba kila kabila lilizungumza lugha yake.

Hakunamahala popote Profesa alkuwa na maana unayozungumza wewe maana umetafsiri maneno ya mtu kwa jinsi unavyodhani wewe kwa sababu tu hukubalini na mawazo ya Profesa juu ya swala la Tanganyika. Hii haikusaidii wewe lolote isipokuwa unajipiotosha wewemwenyewe zaidi kama bainaianik anayeamini Ngo'mbe ni Mungu basi sema utakavyosema hutaweza kuibadilisha imani yake juu ya Uuungu. Haitakiwi hivinmkuu wangu Jukwaa hili linatakiwa umakini zaidi ya kuelat hizi habari za Utanganyika na YUzanzibar bali nini suluihisho la Utaifa tulonao leo.
 
Hakunamahala popote Profesa alkuwa na maana unayozungumza wewe maana umetafsiri maneno ya mtu kwa jinsi unavyodhani wewe kwa sababu tu hukubalini na mawazo ya Profesa juu ya swala la Tanganyika.

Hii haikusaidii wewe lolote isipokuwa unajipiotosha wewemwenyewe zaidi kama bainaianik anayeamini Ngo'mbe ni Mungu basi sema utakavyosema hutaweza kuibadilisha imani yake juu ya Uuungu. Haitakiwi hivinmkuu wangu Jukwaa hili linatakiwa umakini zaidi ya kuelat hizi habari za Utanganyika na YUzanzibar bali nini suluihisho la Utaifa tulonao leo.
Mkuu, kwanza, nilichokisema kuhusu katiba ya znz 2010 hukukieleza kama kina tatizo. Tatizo ulilooona ni kuhusu Prof Shivji

Shivji alisema Nyerere alikuwa katika hatua za kujenga utaifa.
Hatukuwa na utaifa kabla ya hapo.Akasema nje ya muungano Watanganyika watagawanyika.

Hii maana yake ni kuwa kazi ya kujenga utaifa aliyoanza Nyerere ima haijamalizika au inaendelea kwa nguvu ya muungano. Hapa nasema si kweli!
Znz ingekataa muungano bado tungekuwa taifa tu.

Utaifa uliojengwa kutupatia uhuru ndio kilikuwa chanzo cha utaifa wenyewe.
Shivji anaposema znz ilikuwa na utaifa kwa miaka 200 na zaidi, anajaribu kututisha kuwa ni kutokana na uwepo wa znz sisi tunakuwa kama taifa.
Kwamba utaifa wa znz ndio unaambukiza utaifa wa Tanganyika.

Hata hivyo znz imejiondoa katika utaifa wa Tanzania taratibu na kuhitimisha mwaka 2010 ambapo katiba yake inasema znz ni nchi na taifa ikiwa na serikali n.k
Hivyo Tanganyika inabaki kuwa na utaifa wake bila znz, kwasababu utaifa uliopo ni symbolic.

Kuhusu kuongelea Utanganyika na Uzanzibar, unatulaumu wengine bila sababu za msingi.
Miaka 50 tumejaribu kuwa pamoja na wznz.

Hivi karibuni wameonyesha wazi kutukataa, kutukana na wala hawajitambulishi kama Watanzania bali wazanzibar. Katiba ya 2010 inanitetea na wala si maneno yangu.

Kwa mwendo huo, hatuna budi kutafuta utaifa wa Tanganyika.
Zanzibar wana utaifa wao tayari.

Nikukosa fikra kama tutaendelea kujidanganya kuwa muungano huu uliovunjwa na znz bado upo na una maana.

Ndio maana tunasema, kuna maeneo 7 tunaweza kuwa pamoja, mengine kila mtu awe na lake. Hiyo itawezekana kupitia S3.

Kwa S2 ni dhahiri tumeshindwa na hakuna namna matatizo ya miaka 50 na awamu 4 za uongozi zimeshindwa, tukabaki tukiamini kuwa kuna suluhu kama Mkandara anavyotaka tujadili.

Hata kama suluhu itatafutwa, tunapouliza kuhusu wznz kusema jambo moja wakiwa znz na kukana wakiwa Dodoma ni unafiki, na hilo Mkandara halizungumzii.

Hali ilivyo, ni miujiza kuamini kuwa muungano upo kukiwa na katiba ya znz ya 2010.
Tumemuonyesha Mkandara wapi katiba hiyo inapoleta mkanganyiko.

Mkandara anasema ni halali kwa znz kufanya uhuni huo na ni sawa kwa Watanganyika kukaa kimya. Sisi wengine tunasema, nope! time is up, sasa tunataka twende mbele.
Muda wa kubembeleza wznz wasio na shukrani umekiwsha.

Kama hakuna suluhu mezani, basi tutaitafuta kwa njia nyingine.
Huko njia nyingine kutakuwa na lawama na fedheha.
Muhimu ni kuwa na amani ya kudumu kama majirani kuliko muungano wa manung'uniko yasiyoisha.Ndio maana tunasema heri nusu ya shari kuliko shari kamili.

Ule uvumilivu wa Watanganyika sasa unafikia mwisho.
Na mwisho wa uvumilivu huwa ni tatizo.

Ni bora suluhu itafutwe kwa ridhaa ya wananchi na si kuwalazimisha.
Mbele ya safari kutakuwa na kulaumiana, lakini nani wa kulaumiwa?
Yule aliyejitoa miaka 50 au yule anayevunja muungano.

Tanganyika itazuinduka mkuu wangu, si maneno yangu ni kauli ya 'nature'
 
Tatizo lako unasoma pasipo kuelewa maana na hapo ndipo unapokosea sana. Kwa mfano Profesa Shivji anapozungumzia UTAIFA alikuwa na maana rahisi kabisa ya kwamba Muungano wetu umekuja wakati Nyerere alikuwa ktk hatua za kujenga UTAIFA hii haina maana nyingine zaidi ya kwamba sisi wenyewe tulikuwa bado katika mgawanyiko wa makabila 120 ambayo hayakuwa na Umoja wa aina yoyote licha ya kwamba kila kabila lilizungumza lugha yake.

Hakunamahala popote Profesa alkuwa na maana unayozungumza wewe maana umetafsiri maneno ya mtu kwa jinsi unavyodhani wewe kwa sababu tu hukubalini na mawazo ya Profesa juu ya swala la Tanganyika. Hii haikusaidii wewe lolote isipokuwa unajipiotosha wewemwenyewe zaidi kama bainaianik anayeamini Ngo'mbe ni Mungu basi sema utakavyosema hutaweza kuibadilisha imani yake juu ya Uuungu. Haitakiwi hivinmkuu wangu Jukwaa hili linatakiwa umakini zaidi ya kuelat hizi habari za Utanganyika na YUzanzibar bali nini suluihisho la Utaifa tulonao leo.
Mkandara,

Tunapozungumzia utaifa na ujenzi wake chini ya mwalimu nyerere, maana yake ni nini hasa, je ni "utanzania"? Je, nguzo kuu ya utaifa huu wa "utanzania" ni muungano baina ya Tanganyika na zanzibar? Je, utaifa huu wa utanzania unavuniwa na pande zote za muungano au unawahusu zaidi waliokuwa wakiitwa watanganyika?

Kwanini hadi leo (na hata kabla ya mabadiliko ya katiba znz 2010), watu kutoka upande mmoja wa muungano (zanzibar) wameendelea kujitambulisha kama wazanzibari kuliko watanzania, huku wanaojitambulisha zaidi kama watanzania wakiwa ni wale waliojulikana awali kama watanganyika?

Kwa miaka 50, nini imekuwa msingi wa ujenzi wa utaifa wa "uzanzibari? Je ni muungano kama ulivyokuwa nguzo ya utaifa wa utanzania kwa upande wa waliokuwa watanganyika?

Je, kati ya muungano na azimio la arusha, kipi kimejenga utaifa zaidi kwa watanganyika (ukipenda waite watanzania)?

Kuna haja gani ya kuendelea kupigia debe utaifa wa "Tanzania" iwapo miaka 50 baadae, wanaoitwa watanzania ni wale waliokuwa watanganyika kabla ya muungano huku wale walioungana nao (znz) wakijivunia utaifa wa zanzibar kuliko Tanzania?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi;9627033]Mkandara,

Mkandara anaamini utaifa wetu unajengwa na muungano na wazanzibar. Masikini hatambui kuwa miaka 50 wznz ni taifa tofauti na Tanzania na wala hawataki kuwa sehemu ya utaifa wa Tanzania au Tanganyika. Miaka 50 baadaye Mkandara anaamini muungano wa 1964 bado upo hai.

Mkandara anajifariji hata kama ukweli anauona. Hataki kukubali kuwa wznz wamevunja utaifa, nasi tunabaki 'tukishangaa' hee wenzetu wametuacha! tutabaki salama-Nyerere.

Mkandara anaamini kuwa kwa hali ilivyo bado tunaweza kuishi kama watu wa taifa moja. Yupo katika state of denial kuwa muungano umevunjwa na wznz siku nyingi na katiba ya 2010 ni kupigilia msumari katika jeneza.
He is in the state of denial na siku zote huwezi kupata suluhu kama upo katika denial.

Utapataje suluhu kama hakuna utambuzi wa tatizo? Denial ni tatizo kubwa sana
 
Mchambuzi na Nguruvi3,
Nawaomba mrudie tena kusoma alichoandika Nguruvi3 ya kwamba Profesa Shivji alisema - Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na mwaka 1964 tukaungana wakati Nyerere akiwa bado anajenga utaifa.

Hili neno AKIWA BADO (while) anajenga Utaifa ina maana gani kwenu kama sii kazi ilotangulia muungano wenyewe! Nachoelewa mimi ni kwamba Nyerere akiwa bado na kazi ya kujenga Utaifa wetu (Tanganyika) hivyo ikafuatiwa na Muungano. Hakuna mahusiano ya maandishi hayo na utaifa wa Tanzania....
 
Kwa maoni yako yaweza kuonekana hivyo. Kwa maoni ya Shivji, alisema hatuna Utaifa kwasababu mwalim alikuwa bado ana ujenga hivyo kuvunja muungano kutaleta tatizo la makabila kujitenga. Akasema znz ilikuwa na utaifa miaka 200 na zaidi. Hapa prof alikuwa ana maanisha kuwa Utaifa wetu upo ndani ya muungano na ndio maana ni wamoja, nje ya muungano ile kazi aliyoanza mwalimu 1961 ambayo haikukamilika hadi muungano itakuwa na madhara.

Maana ya Shivji ilikuwa kuonyesha muungano ulivyojenga utaifa na nje ya hapo tutaparaganyika kwa maneno yake na si yangu. Sisi tunasema si kweli, alikuwa antisha kama wanavyotisha CCM sasa hivi.
Nyerere alianza jitihada za muungano wa mtaifa yetu way mwaka 1963 bila kujali kazi yake ya kujenga utaifa ilikuwa imekamilika au la.Kenya walipokataa EAF, Tanganyika haikuparahanyika. Tena Kenya walitukataa mwaka 1977 na baso tupo kama taifa, seuse Zanzibar.\

Mwalimu Alifanya hivyo akiamini kuwa tayari tulikuwa na utaifa, kazi iliyokuwepo ni kuusimika usimame imara na kuondoa tofauti.

Prof Shivji anapokuja na dhana ya utaifa wetu unajengwa na muungano, si kweli.
Zanzibar leo wakiamua kuondoka katika muungano haina maana taifa letu litakufa, in fact hawapo katika muungano hadi sasa.
Ukisoma katiba yao ya 2010 hakuna muungano Mkandara , kilichopo ni Zanzibar kuvizia fursa za jina Tanzania katika kupata mafao ya Watanganyika, nje ya hapo znz hawatutambui.

Ndio maana tunasema, tunataka utaifa wetu ili mbele ya safari tuwe na mahali pa kushika. Tunataka fiscal autonomy ya Tanganyika.
 
Nadhani utakubaliana nami kwamba in order to study or understand nation hood in Tanzania na mchakato wake kwa ujumla, ni lazima kuhusisha suala hili na ujamaa, na sio muungano.
Na ni kwa mantiki hii utaifa wa mtanzania maana yake ni utaifa wa mtanganyika. Mzanzibari anaingia kwenye utanzania kwa tiketi ya uraia, sio utaifa, na ni kwa lengo la kutafuta fursa tu. Vinginevyo utaifa wake ni uzanzibari.

Mkuu sikuelewi kabisa manaa kila unalozungumzia hapa ni Tanzania, hizo jitihada za mwaka 1963 ni jitihada zipi? kama sio Kuijenga Tanzania hata kabla ya Uhuru wa Zanzibar ama Mapinduzi - Rejea mkutano wa Kampala, Uganda.
Na hata napozungumzia ya Kenya na EAC sisi tayari tulishakuwa Tanzania hivyo Nyerere alisema ama alifanya kama rais wa Tanzania na sii Tanganyika. Na unaposema Utaifa wetu sii wa Muungano ila wa Tanganyika sasa inakuwaje mnaitaka Tanganyika leo ambayo wewe mwenyewe unaamini ipo? Na pengne nipe darasa nini haswa maana ya TAIFA maanake mimi sii Mtanganyika hata kidogo bali Mtanzania.

Na dhana ya kwamba tuna Utaifa wetu ilihali hatuna tena naaweza kusema kizazi hiki cha leo ni watu wachache sana waloweza kubeba passport ama karatasi yoyote inayowaita wao kama Watanganyika. Utaifa ni Utanganyika na hata ktk uchaguzi mkuu wa miaka kabla ya Uhuru kina Marealle walipigania uhuru wa Kilimanjaro na kina Mtenvu, Fundikira wakitazama zaidi ukanda wa ziwa na Tabora.

Profesa Shivji habahatishi wala hasemi lisilokuwepo, maana wewe na mimi tunaitwa WATANZANIA kama Utaifa wetu, hakuna kitu Watanganyika wala haikufikiia historia ya Watanganyika, zaidi ya swala la muungano wa NCHI 2 kuunda Utaifa wetu hasa kutokana na kwamba hadi tunapata Uhuru sisi wote tulijuliana kama jumuiya ya AEC zaidi ya Utaifa wa nchi hizo.

Kabla ya Uhuru sisi wote tulitawaliwa na Muingereza, tulitumia fedha ya Mkoloni na jumuiya nzima iliendeshwa kwa ngfuvu ya Umoja huo zaidi ya Utaifa wa nchi hizi. Hivyo hata tulipopata Uhuru bado tulikuwa ktk mfumo huo. Kenya walipata Uhru wao 1963, Zanzibar 1963 baada ya makubaliano kati ya Kenyatta na Shamte kuuziana mpaka ya ukanda wa pwani ya Mombasa na Malindi.

Hivyo japo sisi tulipata Uhuru wetu mapema lakini bado Nyerere alikuwa na kazi kubwa sana ya kujenga Utaifa wetu na na kama sijakosea mwaka 1967, Nyerere alilazimika kuchagua kiswahili kuwa lugha ya Taifana lugha ya kufundishia. Ni katika mfumo huo wa Kijamaa Nyerere aliweza kuwatawanya Watanzania wa makabila kufanya kazi mikoani, vijiji vya Ujamaa na kadhalika hivyo haikuwa tu swala la kiuchumi bali pia kujenga UTAIFA ambao leo hii kizazi hiki kinajivunia.

Ni rahisi kwenu vijana kupigania Utanganyika maana huu Utanzania wenyewe mmepewa katika sahani la dhahabu. Ni sawa na mtoto alolelewa na Mama kwa miaka mingi baada ya baba yake kumkataa lakini baada ya kugundua kwamba Baba ana kipato kikubwa ama mheshimiwa nbasi mtoto unaanza kutafuta Identity ya Baba!

Hii habari ya Utanganyika ni kwa sababu tu mnajua Tanganyika ina utajiri mkubwa lakini laukama tungekuwa maskini kama Sudan tusingeinua kidole, tena tungelazimisha kama Sudan ya Kaskazini. Hii akili hii ya kutazanma mali ili ku define asili yetu ya Utanganyika ndio sintokubali.

Mimi sii Mtanganyika na waa sintokuwa Mtanganyiika ila kwa kulazimika kwa sababu naipenda Tanzania yangu ambayo ndio imenilea na kunikuza.. Huu ndiio Utaifa wangu na kusema kweli sikumbuki kabisa Utaifa wa Kitanganyika maana kati ya mwaka 1961 hadi 1963 nilikuwa bado sina akili ya kuchanganua tofauti baina ya Utanganyika na Ukerewe wangu!.
 
Mkandara,

Nadhani utakubaliana nami kwamba in order to study or understand nation hood in Tanzania na mchakato wake kwa ujumla, ni lazima kuhusisha suala hili na ujamaa, na sio muungano.
Na ni kwa mantiki hii utaifa wa mtanzania maana yake ni utaifa wa mtanganyika. Mzanzibari anaingia kwenye utanzania kwa tiketi ya uraia, sio utaifa, na ni kwa lengo la kutafuta fursa tu. Vinginevyo utaifa wake ni uzanzibari.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu wangu neno UTAIFA linawahusu WATU na Uraia wao. haina maana ya ARDHI ama NCHI isipokuwa kwa kutumia neno TAIFA. Hivyo mkuu jaribu sana kutambua kwamba Utaifa unaozungumziwa ni wa watu na hatukuwahi kuwa wamoja kati ya mwaka 1961 hadi 1964 zaidi ya kupokea mageuzi ya Kiutawala. Ni toka mwaka 1964 hadi leo ndio identity yetu imekuwa wazi zaidi na kujulikana kwa watu waitwao Watanzania, nyumka ya hapo tuliitwa tu British East Africa na tanganyika ilikuwa kama jimbo tu ndani ya jumuiya hiyo....
 
Kwahiyo unataka kusema usingekuwepo muungano tungekuwaje. Hili ndilo swali usilotaka kujibu. Hebu tueleze bila muungano tungekuwa na kitu gani.

Pili, si kweli kuwa tulijulikana kama Watanzania mwaka 1964. Jina Tanzania halikupatikana mwaka huo.
Rejea historia vema, na hapa namwalika Mag3 atueleze chanzo cha jina Tanzania ni lini na proposal zake zilikuwaje.
Mkandara wewe hukuwa Mtanzania mwaka 1964, usipotoshe vijana makusudi.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara,

Nadhani utakubaliana nami kwamba in order to study or understand nation hood in Tanzania na mchakato wake kwa ujumla, ni lazima kuhusisha suala hili na ujamaa, na sio muungano.
Na ni kwa mantiki hii utaifa wa mtanzania maana yake ni utaifa wa mtanganyika. Mzanzibari anaingia kwenye utanzania kwa tiketi ya uraia, sio utaifa, na ni kwa lengo la kutafuta fursa tu. Vinginevyo utaifa wake ni uzanzibari.
Katiba ya Zanzibar ya 2010 imetamka wazi kuhusu TAIFA LA ZANZIBAR. Sielewi Mkandara kwanini anafanya mgomo wa kuelewa.

Mzanzibar anajiita Mtanzania anapotoka fursa tu, zaidi ya hapo ni mzanzibar.
Na ni kwa uhakika mzanzibar anatumia fursa ya Uraia si vinginevyo.

Ni kichekesho tunapoambiwa Muungano ndio ulizaa utaifa wa Tanganyika, kana kwamba Kenya au Uganda hawana utaifa.
Kwamba tuliambukizwa utaifa na zanzibar. Shivji kavuruga akili za watu hadi wanasahau kuwa mwaka 1965 hakukuwa na Tanzania. Mchambuzi tafadhali msaidie Mkandara kuhusu decree zilizozaa jina la Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo unataka kusema usingekuwepo muungano tungekuwaje. Hili ndilo swali usilotaka kujibu. Hebu tueleze bila muungano tungekuwa na kitu gani.

Pili, si kweli kuwa tulijulikana kama Watanzania mwaka 1964. Jina Tanzania halikupatikana mwaka huo.
Rejea historia vema, na hapa namwalika Mag3 atueleze chanzo cha jina Tanzania ni lini na proposal zake zilikuwaje.
Mkandara wewe hukuwa Mtanzania mwaka 1964, Usipotoshe vijana makusudi.
Usingekuwepo Muungano Nyerere angeendelea na kazi yake ya kujenga Utaifa wetu wa Watanganyika pengine hata hilo jina lingebadilishwa..who knows. Ni kutokana na muuungano Nyerere alilazimika kuacha kuujenga Utaifa huo na kuanza kujenga Utaifa wa Watanzania yaani hapa wigo limeongezeka.

Labda nikupe mfamo mwingine wa maneno ya profesa:-
Tuseme mimi ni waziri wa Habari,Utamaduni,vijana na michezo nikasema hivi:- Niliteuliwa kama waziri wa wizara ya Habari na UItamaduni mwaka 1996 na mwaka 2000 (Ni mfano tu hauna uhalisia wa miaka) Tukajiunga na Vijana na Michezo wakati bado naijenga wizara....Wewe utaelewa nini hapa?.

Swala La Utanzania,

Mkuu wangu unatafuta sana visababu kwa kukosoa neno kwa neno ilimradi tu kutafuta kosa la kubishana. Sasa iwe Tanzania haikuwepoo mwaka 1964 tunachobishana hapa ni mwaka gani au hoja ya Profesa Shivji kuhusu Utanganyika na Utanzania? Nani kati yetu anaweza sema kwa Uhakika Utanganyka wetu ulipatikana lini na nani alotupa jina hilo na kwa nini wewe unakubali kuitwa Mtanganyka kwa jina lilotolewa na wakoloni?. Hapa sii itakuwa natafuta ubishi mpya!

Mkuu wangu hatupo hapa kubishana ila kufahamishana tu ya kwamba Hapakuwa na kosa kwa Profesa kusema maneno yale ila uliyaelewa vibaya na kwa bahati mbaya unatumia kulaani maneno yale (taken out of context). Na hata majuzi tu Ukawa walidai ya kwamba Kikwete aliwatia hofu wananchi ati ya Jeshi linaweza kuchukua nchi, hamkutaka kumuelewa kwa sababu hamfahamu kwamba serikali kuuanayoongoza rais yenye wizara 7 tu (mambo 7 ya Muungano) inakuwa haina nguvu ya dola, rais ata play ceremonial role ambayo hata akiitwa amiri jeshi mkuu hatakuwa na nguvu ya kiutendaji hivyo.

Jeshi litakuwa na nguvu kubwa na wanaweza kuiondoa serikali madarakani kwa sababu serikali hiyo sio source ya mapato yake. It's a fact ambayo mifano yake ipo wazi kama Misri toka enzi za Abdel Nasser na tumeendelea kuona wanajeshi wakichukua madaraka ya nchi ambazo rais wa nchi hizo hakuwa na madaraka makubwa.

Kifupi nitasema hvi wakati wewe unaidai Tnanganyika kama NCHI, Kuna Wazanzibar wenye fikra kama zenu wanaodai TAIFA la Zanzibar lenye kiti chake UN na hawa mko pamoja UKAWA halafu mnataka kuudanganya Umma kwamba mnautakia mema muungano wa Tanzania.

Hao CCM hawana hoja pia wala hawajui kwa nini wanaxitetea serikali 2 zaidi ya maslahi binafsi kwa sababu wao pia wanataka kuwepo kwa mambo ya Muungano na Yasokuwa na Muungano badala ya kuwa Mambo yote ni ya Muungano isipokuwa shughuli zote za serkari sio za Muungano. Jambo pekee ambalo linakuwa la Muungano na lisokuwa ya Muungano ni SHERIA.
 
Katiba ya Zanzibar ya 2010 imetamka wazi kuhusu TAIFA LA ZANZIBAR. Sielewi Mkandara kwanini anafanya mgomo wa kuelewa.

Mzanzibar anajiita Mtanzania anapotoka fursa tu, zaidi ya hapo ni mzanzibar.
Na ni kwa uhakika mzanzibar anatumia fursa ya Uraia si vinginevyo.

Ni kichekesho tunapoambiwa Muungano ndio ulizaa utaifa wa Tanganyika, kana kwamba Kenya au Uganda hawana utaifa.
Kwamba tuliambukizwa utaifa na zanzibar. Shivji kavuruga akili za watu hadi wanasahau kuwa mwaka 1965 hakukuwa na Tanzania. Mchambuzi tafadhali msaidie Mkandara kuhusu decree zilizozaa jina la Tanzania.

Mkandara
anaelewa fika jinsi gani utambulisho wa Tanganyika ulivyobadilishwa kuwa Tanzania kwa amri tu (presidential decree) ambapo alama, tunu, na mengineyo yaliyoitambulisha Tanganyika kama taifa yalihamishiwa kwa Tanzania kwa vile tu kitu kimoja kimeongezeka katika mlinganyo - zanzibar. Mkandara anaelewa kwani kashiriki mjadala husika humu.

Nimemhoji mkandara huko juu je ni kwanini utaifa wa Tanzania unahusisha zaidi mtanganyika huku mzanzibari akipendelea kutambuliwa na utaifa wa mzanzibari? Mkandara hajaja na majibu ya kuridhisha zaidi ya kuegemea upande wetu wa hoja kwa kukiri (pengine bila kujijua) kwamba lipo tatizo.

Wananchi hawakuwahi ulizwa iwapo walikuwa tayari kuachana na utaifa uliowaunganisha dhidi ya mkoloni "utanganyika" na badala yake kuhamia kwenye utanzania. Hakuna ushahidi juu ya hili. Kwa maana hii, utaifa anaojadili mkandara hence shivji ilikuwa ni utaifa - top-bottom, not bottom-up au participatory. Baadae Watanganyika waliupokea utanzania kwa kumwamini tu Mwalimu na malengo yake hata kama walifichwa katika hatua za mwanzo. Na malengo ya mwalimu yamekwama, wazanzibari hawataki utanzania uwe ndio utaifa wao, sijui kama mkandara unalielewa hilo.

Mkandara, naomba nikuulize:

1. Ni chombo au taasisi gani ambayo au ambazo zilitumika kutekeleza au kufanikisha ujenzi wa huo utaifa wa "Tanzania"?

2. Lengo la ujenzi huu lilikuwa ni kufanikisha nini hasa? Tafadhali weka malengo unayoyajua wazi.

3. Ni vitu gani vilitumika au viliwekwa kama vipimo vya mafanikio?

4. Miaka 50 baadae malengo husika yamefanikiwa kwa kiasi gani na kwa ushahidi upi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi

Utaifa wa Tanzania una sehemu mbili, ya Tanganyika na Zanzibar.
Zanzibar wameshaondoa utaifa wao ndani ya Tanganyika. Hivyo utaifa wa Tanzania haupo tena.
Mkandara anaogopa kujibu swali hilo kwasababu anafahamu atatamka neno Tanganyika.
Hataki Tanganyika si kwasababu ni jina baya la mkoloni, bali kuitaja tu unawaweka wazanzibar pembeni.
Mkandara hata hilo, lakini pia hakanushi kuwa zanzibar ina utaifa wake. Hapa ndipo alipokwama.

Mkandara analeta hoja laini na za kuburudisha pale anaposema Tanganyika ni jina la mkoloni. Sijui Tabora, Singida, Dodoma na kwingine ana uhakika gani kuwa si majina ya ukoloni.

Je, Kenya, Uganda waliokuwa pamoja nasi katika British East Africa wamepungukiwa nini kwa kubaki na majina ya wakoloni. Na nimuulize Mknadara, hivi Kampala ni jina la Mkoloni au Waganda.

Na mwisho nimecheka sana Mkandara alipouambia ulimwengu kuwa mwaka 1963 nyerere alipohudhuria UN general assembly, alikwenda kama British East Africa leader na si Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara anaelewa fika jinsi gani utambulisho wa Tanganyika ulivyobadilishwa kuwa Tanzania kwa amri tu (presidential decree) ambapo alama, tunu, na mengineyo yaliyoitambulisha Tanganyika kama taifa yalihamishiwa kwa Tanzania kwa vile tu kitu kimoja kimeongezeka katika mlinganyo - zanzibar. Mkandara anaelewa kwani kashiriki mjadala husika humu.

Nimemhoji mkandara huko juu je ni kwanini utaifa wa Tanzania unahusisha zaidi mtanganyika huku mzanzibari akipendelea kutambuliwa na utaifa wa mzanzibari? Mkandara hajaja na majibu ya kuridhisha zaidi ya kuegemea upande wetu wa hoja kwa kukiri (pengine bila kujijua) kwamba lipo tatizo.

Wananchi hawakuwahi ulizwa iwapo walikuwa tayari kuachana na utaifa uliowaunganisha dhidi ya mkoloni "utanganyika" na badala yake kuhamia kwenye utanzania. Hakuna ushahidi juu ya hili. Kwa maana hii, utaifa anaojadili mkandara hence shivji ilikuwa ni utaifa - top-bottom, not bottom-up au participatory. Baadae Watanganyika waliupokea utanzania kwa kumwamini tu Mwalimu na malengo yake hata kama walifichwa katika hatua za mwanzo. Na malengo ya mwalimu yamekwama, wazanzibari hawataki utanzania uwe ndio utaifa wao, sijui kama mkandara unalielewa hilo.

Mkandara, naomba nikuulize:

1. Ni chombo au taasisi gani ambayo au ambazo zilitumika kutekeleza au kufanikisha ujenzi wa huo utaifa wa "Tanzania"?

2. Lengo la ujenzi huu lilikuwa ni kufanikisha nini hasa? Tafadhali weka malengo unayoyajua wazi.

3. Ni vitu gani vilitumika au viliwekwa kama vipimo vya mafanikio?

4. Miaka 50 baadae malengo husika yamefanikiwa kwa kiasi gani na kwa ushahidi upi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
swadakta mkuu wangu napenda sana maswali ya aina hii badala ya wewe kuwa na majibu yako tayari kichwani kama anavyofanya Nguruvi3. Labda nianze na yeye tu kwa kusema tena hivi Taifa la Tanganyika lilikuwepo toka enzi lakini WATU wake kama wa taifa moja hawakuwepo na wala hatukuwahi kuujenga ndani ya Mkoloni wala baada ya Uhuru kabla ya Muungano kwa sababu huko nyuma mkoloni aliwatumia Machief wetu kutugawa na kututawala kiasi kwamba hatukuweza kujenga nguvu ya pamoja kama Taifa. Ipo siri kubwa ya Ukoloni ktk kuyagawa mataifa kwa klengo la kuondoa UTAIFA wa watawaliwa. Na baada ya Uhuru Mwalimu ndio kwanza alianza kuujenga Utaifa wetu lakini muungano ukaongeza wigo la Utaifa huo.

Sasa nirudi kwako,
1. Umeuliza ni Chombo gani? nacho nitakisema kama ni CCM ya Mwalimu, hiki ndicho chombo kilichoandika mwogozo wa nchi, itikadi, sera na ilani zake ktk mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi toka kukoloniwa yakilenga kuwashirikisha wananchi wote wa Nchi hizi kuwa kitu kimoja. Navyotambua mimi swala la Muungano baina yetu na Zanzibar lilikuwa na utata sawa kabisa na ndoa ambapo mwanamme anachukuliwa kuwa na haki, nguvu na uweozo kuliko mwanamke, hivyo kumuwezesha mwanamke ama tuseme kuundwa kwa Umoja wa wananwake haikuwa na maana mbaya ya kwamba wanaume wamesahauliwa bali lengo ni kuwashirikisha wanawake pia ktk ujenzi wa Taifa, vivyo hivyo swala la Zanzibar kwa umakini zaidi lilifikiriwa ktk lengo la kujenga Utaifa bila wao kumezwa ama kuonekana wadhaifu tusohitaji mchango wao.

2. Umeuliza lengo, hapa mkuu nadhani hili sii swali kwa sababu tunachozungumzia ni UTAIFA kwa maana ya kuwaunganisha watu wote chini ya TAIFA moja ili wapate identity yao ya kujitambua wao, na kutambuliwa nje kama raia wa taifa husika. Kabla ya hapo British East Afrika ilikuwa ndio kama TAIFA na nchi zake (states) ndio hizo Tanganyika, Kenya Uganda na Zanzibarkwa hiyo hapakuwa na Utaifa zaidi ya kukoloniwa, Hivyo lengo kuu lilikuwa ni kujenga UTAIFA (umoja wa raia wake) ambao hata kama muungano huu usingekuwepo Nyerere na TANU wangeendelea kujenga UTAIFA wa Tanganyika ambao haukuwepo japo tulikuwa huru.

Makosa makubwa ya kutotanguliza kujenga UTAIFA yamefanywa na nchi kama Sudan yenyewe na kisha Sudan Kusini ambao baada tu ya kuupata ya wao kujitenga na Sudan Kaskazini hawakutazama umuhimu wa Ujenzi wa UTAIFA wao, Yalowakuta leo sii bahati mbaya maana vita baina ya wao kwa wao ilionekana wazi hata kabla kutengana, pia hata Ethiopia japo waliungana nchi hiyo na Eritrea, viongozi wao toka Haile Sellasie na Haile Marium hawakujenga UTAIFA wa nchi hizo zaidi ya kutumia mabavu. Mwisho wa siku utengano japo TAIFA ni moja. Tunayaona huko Nigeria ambako hadi leo hakuna Utaifa, kila siku ni vita baina ya Kusini na Kaskazini.

3. Ni vitu gani viliwekwa kama kipimo cha mafanikio.
UTAIFA hauhitaji kuwekewa kipimo maana unachokijenga ni WATU wenyewe kujitambua kama raia HURU wa Taifa hilo hivyo ushiriki na kujitambua kwao wao ndio kipimo pekee ambacho leo sisi wote hapa tunajiita WATANZANIA. Sasa hizi habari za Uzanzibar ndizo changamoto za zoezi zima la Utaifa ambapo watu kama kina Jussa hawatakosekana. Hivyo mtazamo wangu hili swala la kuitaka Tanganyika ni swala la kuuvunja huu UTAIFA tulokuwa nao, na hatua hii haituhakikishii UTANGAYIKA maana kesho msukuma na Wakurya wenye dhahabu na Almasi ama Wayao wa Mtwara wenye gas na mafuta wakaja dai Utaifa wao kwa sababu hizi hizi ya kwamba mikoa ya Singida,Dodoma, Rukwa na kadhalika ni mzigo kwao.

Hii habari ya kuwepo SISI na WAO ndio hatari kubwa ya UTAIFA na tukiweza kuiondoa hizo fikra basi UTAIFA wetu utakuwa umekamilika kama yalivyo ktk mataifa makubwa yaloendelea kujitambua kama Watanzania. Huwezi kumkuta Mmarekani akisema mimi ni Mu -Ohio, sana atasema ni mkazi wa jimbo la Ohio lakini Utaifa wake unabakia palepale.

4. Hili swali nadhani unaweza kupima wewe mwenyewe kutokana na yale malengo niloyataja. Tazama upana wa wananchi wake kujitambua kama wao ni wananchi raia wa nchi hii ya Tanzania. Wameweza vipi kushiriki ktk ujenzi wa Taifa lao, kulinda Uhuru wa nchi yao na maslahai ya Taifa lao. Uzalendo ndicho kipimo halisi cha Utaifa hivyo utakuta ya kwamba UTAIFA wetu umejengeka ktk kiwango cha juu sana tofauti na nchi nyinginezo hasa baada ya kuondoa Ukabila, Udini, Umajimbo na tumebakiwa na vikwazo vichache ambavyo vinasababishwa na haswa wanasiasa wachumia tumbo. Tukiweza kuwaelewa hawa watu vizuri, nini malengo yao na nia zao sidhani kama tunaweza kushindwa kuudumisha Utaifa huu kwa karne zijazo.

Kama tutashindwa leo tukafikia maamuzi ya utengano ili kuunda jumuiya mpya ambayo hatujui matatizo yake, basi haitakuwa kazi kubwa pia kwa mikoa yetu kutengana haswa tunapoendekeza hizi siasa za matumizi ya nchi na rasilimali zake kujenga hoja ya mamlaka kamili Kiutawala kama sababu za kukosa Utaifa ambao waasisi wetu walijaribu sana kuujenga pasipo kutumia nguvu wala mtutu wa bunduki. Ninavyoamini mimi ni kwamba demokrasia pekee sio suluhisho la matatizo yetu ya kisiasa ni lazima tufahamu kwamba chimbuko la mapungufu yote yalozua kero hizi za Utawala yametokana na sababu za KIUCHUMI ambapo katiba yetu haikidhi.

Hivyo swala zima ya Katiba mpya linatakiwa zaidi kuzingatia sukluhu ya KIUCHUMI na sii kisiasa kwani kwa madai ya Tanganyika ni kuturudisha ktk utengano wa Kisiasa ilihali swala kubwa na jukumu kubwa la Katiba mpya ni katiba inayoweza wananchi kukua kiuchumi haswa lkatika dunia hii ya Soko huria na Utandawazi. katiba iliyopo haikidhi mahitaji hayo na inawamyima wananchi wake furza za kikatiba ilihali wamekwisha jenga UTAIFA wao..
 
Sasa nirudi kwako,
1. Umeuliza ni Chombo gani? nacho nitakisema kama ni CCM ya Mwalimu, hiki ndicho chombo kilichoandika mwogozo wa nchi, itikadi, sera na ilani zake ktk mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi toka kukoloniwa yakilenga kuwashirikisha wananchi wote wa Nchi hizi kuwa kitu kimoja.

Nadhani unajua kuna tofauti kubwa Kati ya tanu na CCM.

CCM ilizaliwa miaka 13 baada ya muungano (1977), kabla ya hapo, kulikuwa na TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar. Hata katiba ya muda ya JMT kwa miaka 13 (kipindi cha 1965-77) ilitamka wazi kwamba - hadi pale tanu itakapoungana na asp, chama pekee cha kisiasa katika jamhuri ya muungano kitakuwa ni TANU.

Hivyo basi ujenzi wa huo utaifa wa Tanzania unaoujadili, ujenzi huu ulikuwa ukiendeshwa na chama cha Tanganyika (Tanu), sio CCM (chama cha muungano). Kwa maana nyingine, haupo sahihi kusema Kwamba ccm ndiyo taasisi iliyotumika kujenga utaifa wa Tanzania, unless hoja ibadilike kuwa kwamba ujenzi wa utaifa wa Tanzania ulianza mwaka 1977, na sio 1964.

Hili swali nadhani unaweza kupima wewe mwenyewe kutokana na yale malengo niloyataja. Tazama upana wa wananchi wake kujitambua kama wao ni wananchi raia wa nchi hii ya Tanzania. Wameweza vipi kushiriki ktk ujenzi wa Taifa lao, kulinda Uhuru wa nchi yao na maslahai ya Taifa lao. Uzalendo ndicho kipimo halisi cha Utaifa hivyo utakuta ya kwamba UTAIFA wetu umejengeka ktk kiwango cha juu sana tofauti na nchi nyinginezo hasa baada ya kuondoa Ukabila, Udini, Umajimbo na tumebakiwa na vikwazo vichache ambavyo vinasababishwa na haswa wanasiasa wachumia tumbo. Tukiweza kuwaelewa hawa watu vizuri, nini malengo yao na nia zao sidhani kama tunaweza kushindwa kuudumisha Utaifa huu kwa karne zijazo.

Tanu ilizaliwa miaka kumi kabla ya muungano, miaka saba kabla ya uhuru. Na kama umesoma vizuri historia ya nchi yetu, Tanu iliundwa kwa madhumuni ya kuwaunganisha waafrika ndani ya Tanganyika dhidi ya mkoloni, kwa hiyo hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya ujenzi wa utaifa wa Tanganyika. Tanu ilifanikiwa kujenga utaifa wa Tanganyika over and beyond udini na ukabila, na umoja na utaifa huo ndio uliofanikisha harakati za uhuru chini ya Tanu. MaSwali kwako kufuatia mafanikio ya tanu:

1. Je utaifa wa Tanganyika ulikuwa na mapungufu gani?

2. Utaifa wa tanzania ulilenga watanganyika au watu gani? Kwa maana nyingine, je, mradi wa utaifa wa tanzania ulilenga kuimarisha mapungufu ya utaifa wa tanganyika au kitu kingine?

3. Kwanini leo wale wanaohusishwa na utaifa wa tanzania ni wale wale waliohusishwa na utaifa wa tanganyika?

4. Kati ya mzanzibari na mtanganyika, ni yupi anayefupisha ndoto ya utaifa wa Tanzania ndani ya muungano?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkandara;9662452swadakta mkuu wangu napenda sana maswali ya aina hii badala ya wewe kuwa na majibu yako tayari kichwani kama anavyofanya Nguruvi3
Ninapokuuliza jambo nina ufahamu nalo, hilo si kosa.
Mtu asiyejua anauliza nini hawezi kuuliza kwasababu hajui anauliza nini.
Na wala siulizi ili kupta lecture ninapouliza ninalenga katika kujadiliana, kupata mitazamo tofauti na kutambua nilichokuwa sikifahamu pengine. Mkuu naheshimu mawazo yako, tuendelee na mjadala
Na baada ya huru Mwalimu ndio kwanza alianza kuujenga Utaifa wetu lakini muungano ukaongeza wigo la Utaifa huo
Tumefika mahali tunakubaliana baada ya uhuru, Nyerere alikuwa anajenga utaifa wa Tanganyika, halafu tukaungana na Zanzibar, hivyo kuongeza wigo. Na wala si utaifa kuanza 1964 kama ulivyosema, kwasababu ya muungano. Hili tumeshalimaliza nadhani
1. swala la Zanzibar kwa umakini zaidi lilifikiriwa ktk lengo la kujenga Utaifa bila wao kumezwa ama kuonekana wadhaifu tusohitaji mchango wao
Huwezi kujenga utaifa ukiwa na ka-utaifa kengine.
Taifa ni moja tu na wala hakuna kumezwa.
Hapo chini umesema hakuna taifa la Ohio au California, halafu unataka kutuambia'bila kumezwa'
Kumbuka ziliungana nchi mbili, wapi uhalali wa kumezwa Tanganyika ulipopatikana.

Udhaifu wa znz upo wazi ndio wanauendekeza.
Kila mara wanadai kupata upendeleo maalumu. Huwezi kuwa na Taifa ambalo kuna watu wana privilege zaidi ya wengine.
Kitendo cha kudai na kuomba omba bila kutoa mchango wowote wa mawazo ni udhaifu wanaouendekeza wao.
Tunawezaje kuwa na taifa la watu wanaofikiria nafasi 3 za ubalozi au IGP.
Hapa mchango wa znz ni upi, na je huo si udhaifu
2.Tunachozungumzia ni UTAIFA kwa maana ya kuwaunganisha watu wote chini ya TAIFA moja ili wapate identity yao ya kujitambua wao, na kutambuliwa nje kama raia wa taifa husika
Ndivyo ilivyo sasa hivi, laikini mzanzibar hakubali kuwa yeye ni Mtanzani. Katiba yao ya 2010 ina ushahidi wa wznz kutoukubali Utanzania. Katika mazingira hayo unawezaje kuwa na Taifa lenye kaaifa. Again, unaweza kuwa na Taifa la Texas katika Taifa la Marekani. Mkuu unaona jinsi unavyo ji contradict bila kutegemea
Hivyo lengo kuu lilikuwa ni kujenga UTAIFA (umoja wa raia wake) ambao hata kama muungano huu usingekuwepo Nyerere na TANU wangeendelea kujenga UTAIFA wa Tanganyika ambao haukuwepo japo tulikuwa huru
Excellent! baada ya utaifa wa Tanzania kukataliwa na wznz, tunataka kuendelea.Nashukuru umekubali uhalali wa utaifa wa Tanganyika, jambo ulilogoma kwa kusema utaifa ulianza 1964
Makosa ya kutotanguliza kujenga UTAIFA yamefanywa na nchi kama Sudan yenyewe na kisha Sudan Kusini ambao baada tu ya kuupata ya wao kujitenga na Sudan, Ethiopia. Mwisho wa siku utengano japo TAIFA ni moja. Tunayaona huko Nigeria ambako hadi leo hakuna Utaifa, kila siku ni vita baina ya Kusini na Kaskazini
Nyerere aliyekuwa anaujenga utaifa practically alisema 'Kama wznz hawautaki muungano sitawapiga mabomu'.Sasa hivi wznz hawataki muungano, kwanini tuwapige mabomu? Hawataki muungano

.
 
3. Ni vitu gani viliwekwa kama kipimo cha mafanikio.UTAIFA hauhitaji kuwekewa kipimo maana unachokijenga ni WATU wenyewe kujitambua kama raia HURU wa Taifa hilo hivyo ushiriki na kujitambua kwao wao ndio kipimo pekee ambacho leo sisi wote hapa tunajiita WATANZANIA
. Flat!
Wazazibar wanajitambua kama wznz kwa mneno na matendo.
Katiba yao ya 2010 inawatambulisha kwa kila kigezo cha utaifa na imeweka wazi.
Unaposema sisi na wao ni taifa moja, nadhani unajidanganya. Hawataki utaifa wa Tanzania.
Hakuna sababu za kuwabambikizia kitu wasichokitaka. Unless utuambie katiba 2010 imefanyiwa marekebisho jana.

Zunguka duniani na huko uliko. Wznz huwa na makundi yao ya kizanzibar na hata jumuiya zao za kizanzibar.
Hakuna nchi ya nje yenye jumuiya wa Wasukuma au Wahaya.

Hapo Ontario ulipo ukipitia website kuna ZANZCAN.
Huwezi kuwa member wa ZANCANA hadi uwe mzanzibar.
Ndivyo ilivyo Bristol, Reading na East London.Huwezi kutudanganya,Tanganyika wanaitwa Wapemba kwasababu hupenda kujitambulisha hivyo
Sasa hizi habari za Uzanzibar ndizo changamoto za zoezi zima la Utaifa ambapo watu kama kina Jussa hawatakosekana.

Hivyo mtazamo wangu hili swala la kuitaka Tanganyika ni swala la kuuvunja huu UTAIFA tulokuwa nao, na hatua hii haituhakikishii UTANGAYIKA maana kesho msukuma na Wakurya wenye dhahabu na Almasi ama Wayao wa Mtwara wenye gas na mafuta wakaja dai Utaifa wao kwa sababu hizi hizi ya kwamba mikoa ya Singida,Dodoma, Rukwa na kadhalika ni mzigo kwao.
Haya ndiyo mambo tusiyoyataka.
Mkuu Mkandara huwezi kuita upuuzi changamoto.
Spade si kijiko kikubwa. Huna sababu za kupaka mafuta Uzanzibar, ni tendo la makusudi na la kipuuzi. Si changamoto.

Mtazamo wako kuhusu Tanganyika ni bias na skewed.
Huwezi kumlaumu Mtanganyika aliyejitoa miaka 50.

Utaifa wa Mtanganyika hauji kwa maneno unakuja kwa matendo.
Ukiwa na Tanzania kisha ukaondoa Zanzibar kwa utaifa, hubaki na utaifa wa Tanzania, unabaki na Utanganyika. Kudhanikuwa unabaki na Utanzania is to fool yourself.
Chemistry haikubali, Physics haikubali, physics haikubali na mathematics hakuna, the least to say
Hii habari ya kuwepo SISI na WAO ndio hatari kubwa ya UTAIFA na tukiweza kuiondoa hizo fikra basi UTAIFA wetu utakuwa umekamilika kama yalivyo ktk mataifa makubwa yaloendelea kujitambua kama Watanzania
Miaka 50 'sisi' tulikuwa tayari kuiondoa.

Unaona soni kusema Uzanzibar uondolewe kama tunaka utaifa mmoja.
Kuendelea kuficha ukweli kwa aibu ya maneno kama changamoto, sisi na wao ndiye yale yale ya CCM' tunaliangalia, mchakato, mtazamo, nyeti n.k. ili mradi tu kukwepa ukweli. Walioanzisha u-sisi na wao ni wznz, period
Huwezi kumkuta Mmarekani akisema mimi ni Mu -Ohio, sana atasema ni mkazi wa jimbo la Ohio lakini Utaifa wake unabakia palepale.
Ni halali kwa wazanzibar kujiita wazanzibar ndani ya Tanzania.
Mkuu mbona unajichanganya changanya mwenyewe! simple logic defies your own argument
4.Tazama upana wa wananchi wake kujitambua kama wao ni wananchi raia wa nchi hii ya Tanzania. Uzalendo ndicho kipimo halisi cha Utaifa hivyo utakuta ya kwamba UTAIFA wetu umejengeka ktk kiwango cha juu sana tofauti na nchi nyinginezo hasa baada ya kuondoa Ukabila, Udini, Umajimbo na tumebakiwa na vikwazo vichache ambavyo vinasababishwa na haswa wanasiasa wachumia tumbo. Tukiweza kuwaelewa hawa watu vizuri, nini malengo yao na nia zao sidhani kama tunaweza kushindwa kuudumisha Utaifa huu kwa karne zijazo
Here we go! Utaifa wetu upi?
Wazanzibar wana wao, huo wetu ni upi? Wameshaondoka katika Tanzania, huo utaifa wa pamoja ni upi mkuu!
Kama tutashindwa leo tukafikia maamuzi ya utengano ili kuunda jumuiya mpya ambayo hatujui matatizo yake, basi haitakuwa kazi kubwa pia kwa mikoa yetu kutengana haswa tunapoendekeza hizi siasa za matumizi ya nchi na rasilimali zake kujenga hoja ya mamlaka kamili Kiutawala kama sababu za kukosa Utaifa ambao waasisi wetu walijaribu Ninavyoamini mimi ni kwamba demokrasia pekee sio suluhisho la matatizo yetu ya kisiasa ni lazima tufahamu kwamba chimbuko la mapungufu yote yalozua kero hizi za Utawala yametokana na sababu za KIUCHUMI ambapo katiba yetu haikidhi
Katiba imeshindwaje kukidhi haja.
Muungano una mambo mengi, uchumi, political will na commitment.

Wznz hawana hata moja katika hayo na hivyo kufanya hoja yako kutokuwa na uzito stahili.
Demokrasia ni utaratibu unaohakikisha mambo ya economy, political will and commitment yanafikiwa in fair way.

Unachotaka kusema hapa ni kuwa Katiba imewanyima waznz fursa za kicuhumi.
Sisi wengine tunaona wznz ni zigo na mchango wao mkubwa ni nafasi za ubalozi, IGP na mkuu wa majeshi.

Katika mitazamo ya namna hiyo hatuwezi kufika popote.
Tuwaache wafaidike na fursa zao, nasi tupewe nafasi ya fiscal autonomy ya kuhudumia Watanganyika.

Talaa hawataki hayo 7 tunayodhani tutawasaidia, then njia nyeupee. Let them go.
Usitishe watu kuwa Tanganyika itawgawanyika. Umeangalia upande mwingine?
Muungano haujengwi kwa hofu, na hakuna ushahidi kuwa tungekuwa Tanganyika bila ya muungano mikoa ingejitenga.
Uganda haikutokea wala Kenya, kutufanya tuamini kuwa znz ndio wanatuweka pamoja na si kinyume chake ni kudanganya
Hivyo swala zima ya Katiba mpya linatakiwa zaidi kuzingatia sukluhu ya KIUCHUMI na sii kisiasa kwani kwa madai ya Tanganyika ni kuturudisha ktk utengano wa Kisiasa ilihali swala kubwa na jukumu kubwa la Katiba mpya ni katiba inayoweza wananchi kukua kiuchumi haswa lkatika dunia hii ya Soko huria na Utandawazi. katiba iliyopo haikidhi mahitaji hayo na inawamyima wananchi wake furza za kikatiba ilihali wamekwisha jenga UTAIFA wao..
Hapa unajificha ficha, tatizo la muungano ni znz na wala si uchumi.
Unachotaka kusema hapa ni kuwa Tanganyika iendelee kutoa tu kwa wznz hadi imefikia wanataka na si kuomba.
Mkandara uchumi hauwezi kuwafanya wznz wawe mahayawani wa kutaka sisi tuwaombe idhini ya kufanya mambo ya maendeleo kwa watu wetu. Na wala muungano usiwe sababu ya Mtanganyika kuwa dhalili.

Nimalizie kwa kukuambia kuwa hoja zako zimejikita katika utetezi wa wazanzibar.
Kama ilivyo kawaida yako, makosa na upuuzi wa wznz kuhusu matatizo ya muungano unapaka manukato kwa kuita changamoto.Tatizo la muungano, ni umimi, ubinafsi na majivuno ya wznz ambayo sasa yametibua nyongo.

Unapozungumzia akina Jusa wanaleta matatizo, unawasahau CCM walioshindwa kutatua miaka 50, ni tatizo la mwanzo.

Kututaka Watanganyika tuendelee kulea nchi, taifa na serikali ya nchi jirani ni kututakia balaa.
Hatuna sababu za kuwa na koloni. Wakoloni walikuwa na sababu za kututawala, sababu hizo hatuna kule znz.

Ni lazima suluhu ipataikane kwa kusema ukweli bila kuoneana haya.
Kuwadekeza wznz ni kukitafutia kizazi kijacho matatizo makubwa.
Miaka 50 inatosha sasa kila mmoja abebe mzigo wake.

Tutakuwaje wameoja na utaifa mmoja tukiwa na ka nchi na taifa lingine miongoni mwetu.
Hatuwezi kuruhusu upuuzi huo kwasababu utajenga hali ya wasukuma au wasambaa kuunda kataifa kao ndani ya Tanzania
 
Back
Top Bottom